Ukweli wa mambo: Tukijisahihisha tunaweza.

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,243
Tafakari kwa kina suala hli,
Maendeleo ktk nchi yoyote ile hujengwa ktk misingi mikuu minne.
(1) Watu (2) Aridhi (3) Siasa safi (4) Uongozi bora
Sasa kwa nini nchi nyingi hazina uchumi madhubuti ilihali ina mahitaji yote hapo juu. Mfano ni nchi yetu kwa nn tunarudi nyuma?
Viwanda vinakufa, fedha zinatoroshwa nje, madini wanachukua bure, wanyama wanachukuliwa kiholela, samaki wanachukuliwa bure na mengine mengi. Hapa ndio tujiulize tatizo ni Rais kushindwa kusimama ktk nafasi yake?
Chama tawala kushindwa kukemea maovu ya viongozi serikalini?
Baraza la mawaziri kutokuwa na watu wenye msimamo?
Bunge legelege lisilojua nguvu yake?
Mahakama, polisi, usalama wa taifa, uhamiaji kukubali kutumiwa nje ya taratibu za kazi?
Vitengo vingine pamoja na halmashauri kutokua na wataalamu makini na wa kutosha? Au
Ni wananchi kwa ujumla wetu kukubali kutumiwa na viongozi wasio makini?
Nini kinatufanya mpaka kusifia chumi za wenzetu ilihali tumebarikiwa kila kitu? Jamani ccm washindwa kutuletea UONGOZI BORA NA SIASA SAFI WANATULETEA SIASA ZA MAJI TAKA TUWAKATAE KWA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU. UONGOZI MADHUBUTI HUZAA TAASISI IMARA HII INAONYESHA KIKWAZO CHETU NI CHAMA LEGELEGE. TAASISI IMARA HUZAA TAIFA IMARA LINALOJITAMBUA.
NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom