Mkuu wangu hata sielewi ndicho nachozungumzia hapa wewe ulitumia namba, mimi nilitumia jina na sina sababu ya kudanganya. Tunachotaka kufahamu hapa ni kujaribu kurekebisha mfumo wa elimu nchini na sio kubishana juu ya udini. Mtu yeyote anayechukulia swala hili ktk udini ndiye anayetuvuruga..maana ukweli unasimama kwamba majina yanatumika na tumeona matokeo haya ya juzi yakionyesha majina ya watu.. Sasa kama ilikuwa tukitumia namba na sio majina ni lini NECTA wameacha kutumia namba wakarudi ktk majina? sipati jibu..Kwa kuongezeda tu mwaka 1969 wanafunzi walikaa mtihani wa darasa la saba kwenda sekondary la nane lilifutwa tokea hapo.Mbona sisi tuliofanya Mtihani wa Cambridge Overseas Schools Cerficate mwaka wa 1952 tulitumia namba na sio majina yetu? Kwani kulikuwa na Waziri aliyefuta utaratibu huo baada ya Uhuru?