Wimbo huu tuliuimba sana tukiwa shule ya msingi, na baadaye hata JKT tukiwa kwenye zile zilizoitwa "ruti machi":
"Kambona aliagiza
Chipaka na Kamaliza,
Pindueni mkiweza,
Nitawapeni mapesa,
Nikitoka safarini Uingereza!"
Ndicho tulichofundishwa kuhusu Kambona. Naye pia alisababisha ionekane kuwa huo ndio uliokuwa ukweli (au labda ni kweli ndo ukweli wenyewe huo), kwani kipindi fulani (sikumbuki mwaka gani), ndege ilidondosha vipeperushi vyenye ujumbe kutoka kwa Kambona vikihimiza wananchi waigomee serikali ya Nyerere. Ilikuwa sikukuu sikumbuki sabasaba au nyingine, lakini baba yangu aliokota kimoja na hadi leo kipo nyumbani nimekihifadhi. Ukisoma kipeperushi hicho, kinaashiria alishawahi kudondosha vingine pia siku za nyuma, kwani ndani yake anadai kuwa Nyerere ni mwoga tu anayekimbia kivuli, kwani yeye (Kambona) angetaka kupindua nchi angelipua tu uwanja ambako Nyerere na kabineti yake walikuwa wanatazama ngoma za kienyeji kwenye sherehe ya uhuru siku alipodondosha vipeperushi vingine mbele yake kwa ndege bila kuguswa na mtu! Ati anadai Nyerere alikuwa anashangaa tu wakati watu wanagombea kuokota vipeperushi vya Kambona mbele yake! Kwenye hicho kipeperushi nilichotunza kuna picha ya Nyerere ameshika kichwa, chini yake kuna maneno "Jamani naomba msaada, mambo yamenizidi kimo". Mwisho wa kipeperushi kuna picha ya Kambona na maandishi "Ushindi kwa wananchi" na saini yake Oscar S. Kambona.
Hizo ndizo kumbukumbu nilizonazo kuhusu huyu aliyejiita wakati huo (alipokuwa mkimbizi), "mkombozi" Oscar Kambona.