Ukweli: Matatizo ya Madaktari na Walimu hayawezi kutatuliwa bila kubadilisha Mfumo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,593
8,734
Watanzania wenzangu ukweli unauma lakini hapa JF tunaambiana ukweli wa wazi.

Serikali haina uwezo wa kutatua tatizo la Madaktari na Walimu bila kubadilisha mfumo kwasababu serikali kwa mfumo wa sasa haiwezi kuwa na uwezo wa kuwalipa mishahara na marupurupu mazuri Madaktari wote nchini na walimu wote nchini. Ni lazima tuelewe pesa yeyote serikali inayotumia ni lazima itoke mahali fulani na kwenye fungu fulani la Budget ya nchi. Je ni sehemu gani tunataka Budget ipunguzwe na itoshe kuwalipa zaidi walimu wote na madaktari wote?kama hatuna jibu tunategemea watalipwaje?. Mimi hapa chini nitaeleza ni jinsi gani mabadiliko ya mfumo yanaweza kusaidia kutatutua Matataizo ya madaktari. Nitaelezea Mfumo wa Afya kama mfano:

Mfumo wa sasa:
Mfumo wa sasa wa Afya Tanzania umetoka kwenye nchi za Ulaya. Ulaya kwasababu ya Nchi zao kuwa ndogo wana barabara ndogo, Vyuo vinakuwa kwenye eneo moja, Hospitali zinakuwa kubwa "Medical Center" kwasababu Ulaya hawana nafasi ya kuwa na Medical Center kama Muhimbili au KCMC nyingi kwasababu ya maeneo. Maisha ya Ulaya kila kitu ni kidogo hata magari ni kwasababu ya udogo wa maeneo yao. Nchi za Ulaya zilivyokuja kutawala Africa zilianzisha huu mfumo ambao wanautumia kwao kwenye nchi za Africa na ndiyo mfumo tulionao hadi sasa.

Tatizo la Huu Mfumo ni nini
Tatizo la huu mfumo ni kwamba (1)Tanzania sio Ulaya ni kubwa sana hivyo hatuna na hatutakuwa na uwezo wa kujenga Medical Center kila mahali (2) Watu wanaishi mbali mbali hivyo ni vigumu kuwa na mfumo wa Medical Center kama ulioko Tanzania (3) Barabara, Maji na Umeme Tanzania kwasababu ya umasikini na ukubwa sehemu nyingi hazina barabara za uhakika, maji ya uhakika wala umeme wa uhakika hivyo ni vigumu kutoa huduma za Afya kwenye maeneo hasa ya vijijini. Kwa ujumla huu mfumo wa Ulaya hauwezi kufanya vizuri Tanzania kwasababu Tanzania inatatizo tofauti na ulaya.

Suluhisho ni nini:

1. Mobile Medical Service:
Mtanisamehe kwa lugha sijapata jina halisi kwa kiswahili lakini Tanzania inatakiwa kuwa na Hospitali ambazo zinatembea kwenye magari kama zinazotumika kwenye Majeshi ya Marekani na Canada hii itasaidia (1) Kutoa Chanjo na huduma nchi nzima (2) Kutumia madaktari wachache kwasababu wanakuwa kwenye magari na wanatembea vijiji hadi vjiji (3) Inapunguza msongamano wa watu kuja kwenye hospitali za mkoa au rufaa (4) Hakuna sababu ya kuwa na Medical Center kila mahali
2. Hakuna Haja ya kujenga Medical Center na Hospitali nyingi
Kwasababu ambazo nimeshazisema Tanzania haina haja ya kujenga hospitali kila mahali kwani pesa ya majengo ambayo tunayaita hospitali bila vifaa wala wataalamu tungeweza kutumia kuongeza mishahara madaktari na vilevile kuhudumisha Mobile Medical Center nchi nzima.

3. Uhusiano wa vyuo vikuu vya Afya
Tanzania iweke utaratibu na vyuo vingine duniani kuweza kuleta wanafunzi wao kufanya Practical Tanzania. Madaktari kabla hawajapewa vibali wanafanya kazi miaka miwili bila malipo na wenye wanalipa wenyewe ili waweze kujifunza namna ya kufanya matibabu mbalimbali. Bugando mfano walikuwa na program kama hii na vyuo fulani nafikiri vya marekani. Hawa madaktari wanatakiwa waende vijijini na vilevile gharama za shule walipe wizara na wizara itumie pesa hiyo kuongeza mishahara kwa walimu, kununua vifaa na kufanya huduma nyingine za elimu. Tanzania inaweza kupata pesa nyingi sana za wanafunzi wa udaktari kutoka nchi za nje.

Hospitali bado zitakuwepo lakini ukufuta ushauri wangu huduma zitaongezeka, gharama zitaenda sehu muhimu na madaktari watalipwa zaidi kwani gharama za ujenzi zinaweza kutumika kwenye mishahara.
 
Ngoja nitarudi baadaye ..ni ndefu lakini nimekuelewa..ntakuja baadaye ku comment

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Serikali..ipunguze ANASA tu.short and clear
"Vox populi,Vox dei"
 
Serikali..ipunguze ANASA tu.short and clear
"Vox populi,Vox dei"

Ni lazima kwa wakati mwingine tueleze matatizo kimfumo ili tuweze kufahamu namna ya kutatua. Hata kama wakiongezewa posho kidogo mwaka kesho watarudi tena!
 
Kamundu, mfumo uliopendekeza hauwezi kufanya kazi bila kubadilisha mfumo wa serikali kuu. Ukitaka kutokomeza Malaria nenda kateketeze vyanzo vya mbu kuzaliana na wala sio kugawa quin na vyandarua, nafikiri umenipata.
 
Kamundu, mfumo uliopendekeza hauwezi kufanya kazi bila kubadilisha mfumo wa serikali kuu. Ukitaka kutokomeza Malaria nenda kateketeze vyanzo vya mbu kuzaliana na wala sio kugawa quin na vyandarua, nafikiri umenipata.

Well said
 
tatizo ni serikali kushindwa kutumia rasilimali zilizopo kuboresha ''mfumo'' huu uliopo.usipotoshe watu.ni upuuzi kushindwa kuwalipa walimu/madaktari wakati unakusanya kodi,unamiliki migodi,mbuga na gesi.
 
nakubaliana nawe mkuu, matatizo mengi ya nchi yetu ni mfumo mbovu, sio ccm/cdm.
Wabunge wetu hasa wa upinzani wanayo nafasi kubwa ku influence changes za kimfumo, kama wameweza
kushawishi serekali ibadili katiba na iakwezekana naamini hata hil wanaweza.
Tunahitaji watu wenye mawazo mapya bila kujali ni ccm/cdm.
 
Back
Top Bottom