Ukweli lazima usemwe: Tanzania siyo English Speaking Country ni Swahili Speaking Country

Mkodoleaji

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
458
138
Kuna siku nilikuwa na rafiki zangu wawili kutoka Kanada. Mmoja ameshawahi kuja Tanzania mara nyingi sana hivyo anaifahamu hii nchi na mwingine ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza. Sasa katika mazungumzo ikafikia mahali tukaongelea siasa za Afrika. Moja ya hoja ilikuwa mgawanyiko wa nchi zile zinazoongea kiingereza (anglophone) na zile zinazoongea kifaransa (francophone). Katika hiyo hoja mimi nilikuwa naeleza tofauti iliyopo kati ya nchi zetu (ikiwamo Tanzania) ambazo ni anglophone na francophone. Yule ambaye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuja alikuwa ananisikiliza kwa makini sana wakati yule mwingine alikuwa ananiangalia kwa jicho la wasiwasi kidogo. Nilipomwuliza kwa nini, aliniambia kuwa Tanzania siyo english speaking country bali ni swahili speaking country. Tukacheka yakaisha.

Jana wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki niliona jinsi wagombea na waulizaji maswali walivyokuwa wanapata taabu basi nikamkumbuka huyo rafiki yangu. Sasa nikawa najiuliza hivi sisi watanzania tuna nini? Kwa sababu tunajua kuwa kiingereza ni lugha muhimu basi tunalazimishana kila mahali? Hivi hao jamaa hata kama wangekuwa wanaweza kutema yai, je wananchi wao wanaweza hiyo kiasi gani? Na kama mikataba ya afrika mashariki inaandikwa kwa kiingereza kwa nini tunakubali wakati tunajua wananchi wetu wengi hawaijui hiyo lugha? Nimejiuliza maswali mengi lakini mwishowe nikafikia hitimisho kama lile la kwenye maongezi na rafiki zangu wale kwamba wengi tunataka nchi yetu iwe english speaking country lakini ukweli ni swahili speaking country. Hivi jenga picha kama lile bunge letu wangesema kuanzia leo mijadala yote ni kiingereza ingekuwaje.

Nawasilisha
 
Mkuu kujua kiswahili.., sio hoja ya kutokujua Kingereza.. (International Language)

Hivyo basi ni vema ukajua kiswahili, Kingereza.., na lugha nyingine yoyote unayoweza (kujua Lugha nyingine hakumaanishi lugha ya mwanzo unaisahau)
 
Kume hiyo lugha yao ni intanational tuu!me nilijua ni world language..lol lugha ya dunia......
Nisikilize sasa nasema hiviii mimi nikiwa mdogo makamo nilikua mwanachama wa scout tulienda nchi flani za afrika tuli furahia sana maisha ya kuongea lugha yako kwani nilipata rafiki toka canada alikua 14yrs lakini ana asiri ya jamaica aliniambia kitu kokote utakapo pita duniani....kikubwa ueleweke tuu coz unaweza fika france ukakuta watu hawajui english lakini wanajua french hata rassia na germany pia ni hivyo hivyo....so msipotoshwe na ushamba huo.
 
Back
Top Bottom