Kidamva
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,580
- 1,981
Nilikuwa naangalia kipindi maalum cha mashujaa kwenye television ya ITV. Wameonyesha vita ya Uganda na siku ya mashujaa baada ya vita hiyo.
Nimekuwa nikifuatilia sana vita hii, kujua sababu yake maana kwa muda mrefu tumekuwa tukipewa taarifa za upande mmoja tu (Tanzania). Lakini ukisikiliza au kusoma upande mwingine utagundua mengi tu.
Nimewahi kusikia kwamba vita hiyo ilisababishwa na uchokozi Wa Tanzania. Nyerere alikuwa hapatani na Idd Amini na alichukizwa na kitendo chake cha kumpindua swahiba wake Milton Obote. Ndio maana Obote alikuja kuishi Dar.
Kwa hiyo Nyerere alikuwa anamtafuta Idd Amin kwa udi na uvumba. Inasemekana kulikuwa na kambi za mafunzo kwa Waganda wasiokubaliana na Idd Amin akiwemo Rais Yoweri Museveni kule Moshi.
Museveni alisoma degree yake University of Dar es salaam. Sasa hao waliofunzwa walikwenda kutest zali kwa kufyatua mabomu upande Wa Uganda.
Ndipo majeshi ya Idd Amin yakajibu mapigo kwa kushambulia Kagera, wakavunja daraja la mto Kagera na kuharibu nyumba na makanisa.
Hapo ndipo Nyerere akapata sababu, akatangaza vita, kweli majeshi ya Tanzania yakavamia Uganda.
Inasemekana hata mataifa ya Magharibi hayakuiunga mkono Tanzania, ila Urusi ndio iliunga mkono na ndio iliyokuwa iki supply silaha.
Ni vita iliyoitia hasara kubwa Tanzania, baada ya hapo ilikuja njaa kali mtakumbuka tulikula unga wa yanga.
Kwa ufupi ndio nilichopata kwenye utafiti wangu mdogo. Wanaojua zaidi watujuze