Ukweli Kuhusu UDOM huu hapa

Ukisikia kumkoma nyani giladi ndio huku.
Kudos kanda2.

Yaani umefunika, umeweka sawa kila kitu. Analysis yako imekuwa very extensive. Duh! kumbe jamaa zetu ndivyo walivo. Nafasi zote wamehodhi wao.

The point ambayo watu wanaikosa humu ni moja tu. Waislamu hawapaswi kuonekana kwenye sehemu zozote za maendeleo na elimu. Wao wameshatengewa kazi zao ambazo ni upishi, usafi na udereva.

Hii inchi sasa inaelekea kubaya na wenyewe wameshasema kama HAWADANGANYIKI. Unajuwa facts kama hizi wakizipata wale jamaa zangu pale Mtambani, Kichangani au Kwa Mtoro bdio watazdi kuchanganyikiwa, si unauwa Jazbii walivyo.

Binafsi napinga udini kwa misingi yeyote ile. Taasisi za umma zinapaswa kuendeshwa na watu wenye sifa bila kujali dini zao. Mtu yeyote anapigia debe udini anapaswa alaaniwe na waTz wa dini zote, kwani leo hii akiwa mkristo atawabagua waislamu, lakini baadaye atakwenda kubagua wakristo wenzake kwa misingi ya madhehebu, baadaye ukabila, ukoo nk nk.

Kuna mtu yeyote ana facts katika nafasi zote walizoshika wakristo ni waislamu wangapi walikuwa denied nafasi hizo based on dini zao? Na tunaweza tukarudi nyuma zaidi, je kwenye mtihani wa darasa la saba ratio ya kufaulu ya wakristo na waislamu ikoje? tukaendelea hivyo hata kufikia vyuo vikuu. Kwa sababu naamini uchaguzi wa kazi zenye kuhitaji utaalamu ni kiwango cha elimu/ujuzi stahili kwa kazi inayoombwa, sasa kama ratio ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu kati ya waislamu wakristo na dini zingine ni mfano 1:7:2, no wonder kwenye soko la ajira rasmi itakuwa katika mtazamo huohuo.

Udini kwa mtazamo wangu ni matokeo vilevile ya kukosekana kwa uzalendo, kunapokosekana uzalendo tunatafuta kitu kingine cha kutuunganisha na ndiyo tunapata dini, kabila, kanda na vitu kama hivyo. Sasa nani wa kulaumiwa kwa kutupeleka watanzania kutokuwa na moyo wa utaifa kama si viongozi wetu ambao na wakristo, waislamu na wapagani.
 
Kazi kweli kweli, Waislam/Muislam kuwepo sehemu huo ni udini, mnatakiwa kuzoea, Tanzania ni yetu sote.
 
Nyie wabongo, Kutumia dini kama kigezo cha kutoa mshahara mzuri kwa mtu mwenye sifa sawa na mtu wa dini yako haikubaliki wether you are christian or Muslim.

Hoja iliyoletwa hapa kubwa ilikuwa ni kutumia CHEO au madaraka aliyonayo mtuhumiwa.

Ila nyie mlioenda "shule saana" mmeshaanza kulete UDINI hapa. Tofautisheni kuwa Mdini na kutumia DINI kama kigezo, I know there is a thin line between the two, but surely there is a line.
Mtoa mada wa awali alidai kuwa UDOM ni chuo cha waislam kimejaa udini na upendeleo. Nilichofanya ni kuonyesha kuwa madai ya awali si sahihi na kutoa data. Kwanza UDOM ni taasisi ya umma. Si rahisi kwa yoyote kutoa mshahara au marupurupu kwa kufuata matakwa binafsi.

Wanaodai UDOM kuwa ni chuo cha Waislam ndio wanaoendekeza Udini. Labda mtoa hoja wa awali angetaja chanzo cha habari yake napia ni vyeo gani wamepewa watu kwa upendeleo kwa sababu orodha ya viongozi imetolewa. Mwenye hoja aitoe kwa data.

Angalizo langu kuu ni juu ya madai yenye chuki juu ya kikundi fulani au mtu fulani. JF ni kijiwe cha wenye busara, hoja zetu zionyeshe busara zetu.

Ubaguzi wa dini, rangi, kabila nk. ni hatari kwa nchi yetu.
 
JF kama ni kijiwe cha watu wenye busara basi na wewe mleta data hizi ulipashwa kutumia busara zako wewe mwenyewe! Je hiki kitu ninacholeta hakitaligawa JF na nchi kwa Ujumla?? siyo kila kitu kinaletwa hapa!! hata kile cha uchonganishi kama huu!

Nasema hivyo humu kuna wachangiaji wa matabaka mbalimbali na wote hawawezi kukuelewa kama wewe unavyoamini.
 
Waungwana Habari za udini hazifai kutajwa na kujadiliwa na jamii ya watu makini kinachotakiwa ni kueleza mapungufu ya mtu fulani mwenye cheo fulani kwani upungufu au uimara wa mtu hauletwi na dini ila ni mtu mwenyewe.

Tukianza na dini tutaelekea kwenye kabila then tumalizie na jinsia.

Huko ndiko tunakoelekea.
 
chuki na udini umekujaa, najua hampendi kuambiwa ukweli hasa pale hila zenu zinapofichuliwa.

Sehemu zote hizo zenye vita ni kwa sababu ya uroho wa wagalatia dhidi ya mali za waislam walizjaaliwa na mola muumba.

Hapa kin achotakiwa ni kujibu hoja kwa hoja sio kushutumu na kutukana kwa sababu tu hoja zilizowasilishwa umeshindwa kuzijibu.

Waleta hoja wakiziwasilisha bila data mnasema uzushi, wakiweka data mnasema analysis zinaboa sasa mnatakaje?????.

Hapo ndo inpodhihirika hila na chuki dhidi ya uislam.

LOL. Umekurupuka.

Nenda kwenye jukwaa la dini kaangalie maandishi yangu. Acha kukurupuka wewe, nyie ndo mnaangusha UISLAMU maana hamna hoja bali jazba na nyie ndo mnaleta VITA.

Sijasema Uislamu unaleta vita nimesema watu wenye mawazo kama wewe ndo wana sapoti Boko haram na kueneza vita kwa jina la Uislamu.

Amka bro umesinzia...
 
Mtoa mada wa awali alidai kuwa UDOM ni chuo cha waislam kimejaa udini na upendeleo. Nilichofanya ni kuonyesha kuwa madai ya awali si sahihi na kutoa data. Kwanza UDOM ni taasisi ya umma. Si rahisi kwa yoyote kutoa mshahara au marupurupu kwa kufuata matakwa binafsi.

Wanaodai UDOM kuwa ni chuo cha Waislam ndio wanaoendekeza Udini. Labda mtoa hoja wa awali angetaja chanzo cha habari yake napia ni vyeo gani wamepewa watu kwa upendeleo kwa sababu orodha ya viongozi imetolewa. Mwenye hoja aitoe kwa data.

Angalizo langu kuu ni juu ya madai yenye chuki juu ya kikundi fulani au mtu fulani. JF ni kijiwe cha wenye busara, hoja zetu zionyeshe busara zetu.

Ubaguzi wa dini, rangi, kabila nk. ni hatari kwa nchi yetu.

Tupo pamoja mkuu.
 
Tatizo la baadhi ya wakristo ni chuki na roho mbaya kwa waislam. Mahala popote wakiwepo waislam kwenye uongozi ndio utaona shutuma na malalamiko ya udini, ukiuliza kivipi utaambiwa viongozi wa juu wawili au watatu wote waislam! Kwa maana nyingine waislamu hawatakiwi kuongoza.

Na haya hilki la stereo type eti waislamu wamesoma madrasa kwa hiyo hawatakiwi kuwa katika uongozi wa juu ni uongo wa mchana kweupe. Kila mwaka maelfu ya waislamu wana graduate kwenye vyuo mbali mbali na bado nafasi hata za kada za chini wamejazana wakristo tu kwa kisingizio eti hamjasoma!

Sasa wakristo mnaumwa ugonjwa wa mazoea alio waambukiza baba yenu Nyerere kuwa kila mahala watawala mue nyie tu. Msahau nchi hii ni yetu sote na wale mnaona kichefu kichefu kuona muislamu yupo katika nafasi fulani mtatapika sana itabidi mzoee tu kwani waswahili nao wameenda shule na sasa wanakalia nafasi, vimbeni mpaka mpasuke!
 
Mamkwe,
Umetbibitisha tu kuwa ni kweli kile chuo cha UDOM kimeshikwa na Waislaam. Huyu Mchaga Kinabo (kama sikosei) kapewa cheo cha Academic. Huko yeye anadeal na wanafunzi, waalimu, masomo, nk wakati huyu anayeshukiwa kuwa MDINI yaani Pro. S. Mlacha na Kikula, ndiyo Maboss wenyewe na ndiyo wameshika MPINI. Hapo ongeza Bilal ambaye ubabe wake ulionekana wakati Mkapa ni Waziri wa Sayari na Elimu ya Juu na yeye ni Katibu Mkuu. Akipata tatizo badala ya kwenda kwa Mkuu wake Mkapa, alikuwa anaenda moja kwa moja Ofisi ya Jirani yaani IKULU.

Hao Waalimu na viongozi Waislaam wanaweza kuwa wachache ila unyanyasaji wao ukawa wa kutisha. Mbona Rwanda na Burundi Watusi walikuwa 10% ila ubabe wao ulikuwa wa kutisha. Wageruman walikuwa wachache tu ila wakatutawala.
Kama jamaa wanapata UBABE kutoka kwa Kikwete basi itakuwa ni too bad. Nasema kama wanatumia huo UISLAAM kujifanyia mambo kienyeji, itakuja kuwa mbaya sana kwao huko miaka ya baadaye. Hii aliifanya Prof. Kigoma Malima wakati akiwa Waziri wa Fedha. Alikuwa akitoa misamaha ya kodi kwa Waislaam kama kawa. Upuuzi huo akaja kuufanya Mkapa na genge lake na matokeo yake akina Mramba tunawaona Kisutu.

JIPANGE na uje hapa UPYA.

Kanda2 na wengine.

Kwanza niseme naungana na ujumbe wa FP kwamba hapa kinachosemwa SI UDINI ila kutumia kigezo cha DINI kwenye mishahara. Mkuu MaMkwe aliweka list kutaka kutuonyesha nini? Kuwa uongozi wa UDOM umeshikwa na Wakristo? Hapo ndipo nilikataa na kumuandikia kuwa hiyo listi aliyoweka inaonyesha kuwa UDOM kweli imeshikwa na WAISLAAM. Ehhh, Stop have a time. Uongozi kushikwa na Waislaam, why not kama wanaweza. Ningelipenda Rais muadilifu hata kama hana dini kuliko Rais Mkristo kama mimi ila ni FISADI. Waziri Fisadi, Mbunge Fisadi, nk hata kama ni Muislaam/Mkristo anatusaidia vipi sisi?
Mbona kuna watu kibao wanamlilia Sallim Ahmed Sallim ingawa jamaa ni Muislaam? Hata mie ningelienda kupiga kura kwa mara ya kwanza kumchagua Sallim ingawa ni MUISLAAM. Kikwete alichaguliwa kwa kura kibao, unafikiri ni Waislaam tu walimchagua? Uchaguzi ujao unaweza kuta wapinzani wake wakubwa wakawa Waislaam.

Someni tena ujumbe wangu, na mrudie tena na hapo muonyeshe UDINI wangu. Msisome harakaharaka na kuanza kumhukumu mtu. Kwanza hilo li-mtandao lenu la dini nashukuru limetengwa na milele huko mie siingii.....

NB: By the way, Mkapa na Mramba nimeandika, mbona hilo hamkuliona? Hawa nao ni Waislaam? Au mnaona tu yale nyie mnataka kuona? WANAFIKI NYIE.....
 
kwanini watu wasibuni Dini zao...!? Uislamu na ukristo sasa imashakua kero....
 
Nadhani mwenzangu wewe ndiye adui wa wakristo. Mbona sie twaishi nao vizuri? Mwenye ilm kama wewe ukiongea kama kina yakhe mittaani badala ya kutujuvya, watupeleka wapi?

Leka
 
Mimi nadhani jambo la udini linakuzwa na watu fulani kwa faida zao wenyewe. Mwenye akili ya kuona mbali hawezi kutukuza udini wala ukabila wala ujinsia ingawa kwa kiasi upendeleo unaweza kukubalika kwa lengo maalum ili hata wanaopenda kulalala wapateamka. Lakini kama hata nafasi muhimu zinazohitaji sifa maalum kitaaluma zitafanyiwa mchezo wa viti maalum ni makosa makubwa. Kama mtu alala na kungojea kupewa ukurugenzi kwa sababu ya uislam wake au ukristo wake au jinsia yake basi akatafute kisiwa chake mwenyewe na kusubiri hilo.

Demokrasia sio domogasia. Twataka maendeleo na waongozi wetu wenye kujua wanafanya nini, wawe firauni au watu gani hatujali.
 
Mngefanya thamini kujua kuna waisilamu wangapi kwenye magereza yetu ikilinganishwa na wakiristo na pia mje na conclusion.
Watakuwa waeonewa/kupendelewa?
 
Sasa wakristo mnaumwa ugonjwa wa mazoea alio waambukiza baba yenu Nyerere kuwa kila mahala watawala mue nyie tu. Msahau nchi hii ni yetu sote na wale mnaona kichefu kichefu kuona muislamu yupo katika nafasi fulani mtatapika sana itabidi mzoee tu kwani waswahili nao wameenda shule na sasa wanakalia nafasi, vimbeni mpaka mpasuke!

Eddie, unamkandamiza Mzee wa watu kwa kuwa keshakufa na hawezi kujitetea?

Ngoja nijaribu kutoa data labda utaelewa: Akina Kawawa na Jumbe/Karume/Mwinyi walikuwa Wakristo kable ya kuwateuwa kuwa makamu wake? Twalipo alikuwa mkristo kabla hajamteua kuwa CDF? Na hao akina Nyang'anyi, Kinana, Seif Hatibu, Malima na ukoo wake, ... list ni ndefu, waliingizwa kwenye system na nani? Mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani.
 
Wanaosema Prof Kikula na Uongozi wake ni wadini ni wapotoshaji na hawamjui Prof Kikula. Kikula ni mtu safi na asiye na matabaka hata kidogo, naweza nikamuita ni mpiganaji wa taaluma ya elimu ya juu. Kihistoria ni mtu anayefanya mabadliko makubwa katika kipindi kifupi. Namfananisha na Excavator Machine kwenye ardhi ya mawe (Consolidated rocky ground). Sote tumemshudia pale alipohamishwa kutoka mlimani (UDSM) na kwenda UCLAS leo hii inajulikana kama "Full Flagged" ARDHI UNIVERSITY. Kipindi anaingia pale PhD zilikua 4 ambazo 2 za kufoji, komputa 2 chuo kizima kwa ajili ya kufundishia wataalamu wa leo. "It was terrible by the time." Tembelea leo ARDHI alafu uliza " whom ones are remarkable to the all of the findings" Watu wenye upeo kama wako ndiyo watakaosita kumtaja Kikula na counterparts akina Prof. Kasseva, Majani, Chaggu, Meshack, n.k.Hao counterparts aliokuwa nao wote ni Christians na yeye ndiyo aliyeawteua, jiulize kulikuwa hakuna Muslim UCLAS, Au ndiyo bado mnasema tumebase sana madrasa? Au Hapa Kikula alikuwa Mkatoliki? Leo hii Ndiyo tuseme amesilmu? Nakuambia ukweli kipindi kikula anafanya kazi ya "transformation" from college to university alikuwa nazungukwa na majority wakirosto. Hakuna aliyewahi kulalamikia udini walakubaguliwa.
Mimi sishangai sana maana "Christians" hasa nyie RC wana tabia za watoto wa kambo, hawana jema. Hata JK na Mzee ruksa mmeshawahi kuwahesabia mawaziri. Leo hii wakuu wa vyuo, kesho wafagia barabara. Angalieni mnaamsha tuliolala!
 
Haruna Mpulaki,

Kwanza karibu sana JF.

Pili ungeliandika BILA ghadhabu, ningelikuwa 99% ila kwa kuweka kebehi kwa mbali napunguza kidogo.
Mwanzo kumewekwa swali, na watu wanataka majibu. Wee umeandika ya kwako na tutasubiri ya wengine. Kama asipokuja mtu kutengua maneno yako basi huyu jamaa TUMUONDOWE kwenye listi ya utumiaji dini kunyanyasa au kupendelea wengine. Inawezekana hata uongozi wote wa UDOM hawako hivyo. Ila pia inawezekana mmoja wao yuko hivyo. Hii kitu haihitaji watu wengi.
Labda niseme kwa niaba yangu mwenyewe, nashukuru kwa maelezo yako. Mie hao wote siwafahamu. Siwezi kuwaita ni WADINI au si WADINI. Nyie mnaowafahamu mwageni data ili siku nyingne mtu akiwashambulia, tujuwe tumtete vipi.

Boss wa Tanesco nilisikia kuwa mchapa kazi, nikawa namtetea. Kuja kuwekwa hapa mambo kumbe ni Product ya RA na anakamkono kwake kwenye tusenti twa Chenge, nikachoka kabisa. Sasa hivi Idris haosheki tena.

Mkuu, mbona unamalizia kwa kututisha kuwa TUANGALIE? Kwani ukiamka ndiyo itakuwaje? Utajaza JF yote kwa siku moja? Hebu AMKA tuone maajabu yako......
 
Nyerere hawezi kupumzika kwa amani kama nyie hamtaacha kufauta itikadi aliyowafundisha, yaani RC Kwanza. Tumieni akili kidogo, kipindi cahke nchi ilikuwa ipo nusu UJIMA nusu UJAMAA. Sasa hivi sivyo. Unakumbuka jinsi alivyomshambulia Maleccela akimwita "wee John!" eti kapata tetesi amesilimu, amehongwa na waislamu na on rewards anagombea urais. Hauoni kama hili linamfanya MWALIMU WA UDINI asipumzike kwa amani? Kulikuwa na dhambi gani ya kiuongozi "John" Kuwa "Ismail" na kuchukua madaraka. Hii safari ya kuunga unga ya taifa letu la wajinga (DANGANYIKA) inaanza kutoa ishara za kikomo. MUNGU nijaalie niwe mmoja kati ya hao watakaoihitimisha hii safari
 
Haruna,
Ulianza vizuri. Ila sasa unaanza KUHARIBU. Sijui kama umefikia HATUA ya kuelewa NYERERE alikuwa anamaanisha nini. Hata mie nilikuwa kama wewe hadi mzee kwenye Tanzanet akaniambia "Kijana, humjui JKN, wewe subiri uone". Nikamuuliza kwanini? Akasema "JKN alimsoma sana Shakespeer." Nilitaka kuvitafuta hivyo vitabu na nivisome ila nikaonywa kuwa "utasoma lakini hutaelewa, labda aje mtu akuelekeze..."

Sasa kama ulimsikia JKN akisema Malecela kasilimu, nafikiri hukumuelewa na pia sidhani kama alisema hivyo. Hii itakuwa ni zile Story za Kawawa funika kikombe ulizokuwa ukisikia mitaani.

Naanza kupata wasiwasi na makala yako ya juu kuhusu UDOM. Sijui kama unaandika ukweli au na wewe ni MDINI na MSHABIKI kwelikweli....
 
Join Date: Sat Aug 2009
Posts: 3
Thanks: 1
Thanked 1 Time in 1 Post
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Karibu mgeni/mwenyeji
 
Nyerere hawezi kupumzika kwa amani kama nyie hamtaacha kufauta itikadi aliyowafundisha, yaani RC Kwanza. Tumieni akili kidogo, kipindi cahke nchi ilikuwa ipo nusu UJIMA nusu UJAMAA. Sasa hivi sivyo. Unakumbuka jinsi alivyomshambulia Maleccela akimwita "wee John!" eti kapata tetesi amesilimu, amehongwa na waislamu na on rewards anagombea urais. Hauoni kama hili linamfanya MWALIMU WA UDINI asipumzike kwa amani? Kulikuwa na dhambi gani ya kiuongozi "John" Kuwa "Ismail" na kuchukua madaraka. Hii safari ya kuunga unga ya taifa letu la wajinga (DANGANYIKA) inaanza kutoa ishara za kikomo. MUNGU nijaalie niwe mmoja kati ya hao watakaoihitimisha hii safari

Unamtisha nani sasa ...

Unadhani utaleta suicide bombers toka Hamas kuja Tanzania?
 
Back
Top Bottom