Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania

mkuu kuna jamaa nipo nao wana elimu nzuri lakini kupata kazi hapa sa ni shughuli

Aaaaaa wapi!! kama wanashule ya kutosha na hawapati kazi hapo kwa JZ si waende Botswana? tena kwa basi tu kama hawana pesa ya kukwea pipa. nisalimie Malema na wimbo wake wa Phula ebulu!!
 
malema kashinda tena urais ancyl,mzee hata botswana not very easy
 
Wapendwa nitatoa maoni yangu binafsi. Wazo la kuwa nje ya nchi au kusettle nyumbani linachangiwa sehemu kubwa na uchumi. Ni sawa na yule aliye-relocate toka Nchinga-Mtwara kuja Dar es Salaam. Lakini pia kuna suala la feeling za ki-binadamu; hebu fikiri.. umeamua kurudi home baada ya kuangaika sana..na hela zako umeweza pata kagari kako kamtumba...umepiga kiyoyozi unapita pale kituoni..watu wamejaa ile mbaya hakuna usafiri..roho inakuuma ..Ok,,, unarudi nyumbani ambako umeweka Kagenerator pale nyumbani..baada ya Tanesco kuishiwa umeme..wakati kagenerator kanaunguruma na unapata mwanga..Nyumba ya jirani hakuna umeme..watoto wachanga wa majirani wanalia unasikia huruma ..dhamira inakusuta.unaangalia utawaze kusaidia jirani..lakini masikini kagenerator kenyewe kadogo..Anyway... una kajumba kako umeweka uzio mzuri..lakini kila siku vibaka wanakusumbua.Unaamua kuchukua wamasai..kesho yake wamasai wanafanya nyumba yako ndio Ngome..wanawaleta wenzao kushinda..Unaona karaha unawatimua..Ok.. Unaanza na ka Investment..uanpata kahela ambako kanakuwezesha kubadili mboga .lakini extended family kuna watoto wanataka shule, ndugu wengi maisha magumu..unajitahidi kusaidia unashindwa... Anayway...Unajaribu kujiliwaza kwa kuangalia TV ..au kusikiliza Taarifa ya habari ..unasikia utumbo wa wanasiasa wanaoshindwa kuwathamini wananchi...wanagombana wenyewe kwa wenyewe chama A and B..Mafisadi na walalahoi..Unaudhika kwani kuna ka chama kanajaribu kuwatetea walalahoi na kuna kachama kanajaribu kuwatumia walahoi hao hao kuwatetea maslahi ya matumbo yao na mafisadi..unakasirika na kuzima TV....Unaamua kuondoka.. unatoka kidogo traffic anakukamata..huna tatizo..lolote..kwani Maisha uliyoishi nje yamekunja ki-discipline..Huyu Traffic anazunguka gari.. ..anajenga hoja,,Fire Extinguisher ni ndogo kwa ukubwa wa gari ..Mnabishana sana..anaishia kukwambia ukweli anataka kahela akapate supu..unakasirika unampa unaondoka huku Moyo ukidunda kama unataka kutoka kwa hasira....Mbele kidogo unasimama ..umeshaamua ku - postpone kurudi settle..home ..Unaandika kwenye Face-book..kwa marafiki zako.. "Aluta -kontinua..Narudi ughaibuni" Binafsi unajipa moyo..wacha nikaangaike kidogo kama miaka miwili au mitatu nitarudi home..Well, ni -round nyingine umeshindwa ku-settle --ingawa ulikuwa na nia ya kweli..

Ndugu zangu, ukiondoka tu Tanzania ..wewe tayari u-second class citizen..hata kama utapata makaratasi, dual citizenship etc. Hasa pale dhamira yako itakapokuwa inakusuta wakati wa lile swali ambalo silipendi... "where r' u from? Unakumbuka ..Nikiwa nyumbani Tanzania hakuna anayeniuliza hilo swali....

Conclusion -- Umasikini wetu watanzania..na mazingira ya siasa na uchumi wetu vinatuchanganya sana kupata wazo la ku-settle home.. Ingawa, ni kweli ni kuna mifano mizuri ya rafiki zetu wengi wamesha-win baada ya kurudi.yaani wameweza kujibadili ghafla na kukumbatia tena maisha ya nyumbani..Lakini kama kweli ulikulia nyumbani kwenye umasikini.na maisha ya dhiki halafu..tukatoka nje ya nchi Uka-experience kwa kuishi kwa utii wa sheria, Kupata hela kwa kipato halali bila kuomba rushwa, kutokuwa na shaka na vibaka, kutosikia Miziki ya mafisadi..Jamani inakuwa ngumu kuchukua maamuzi ya kurudi nyumbani kwani unajua unaenda kutoa rushwa, unaenda kugombana na utii wa sheria..unaenda kwenye umasikini ule ule ambao unajua ni umasikini wa kujitakia...Yaani inachanganya kweli lakini, All in All...Tutarudi tu..kwani ni nyumbani pekee ambako unakuwa "First Class Citizen"
....Ndugu yangu hapo umenena......
 
THABO MBEKI.....unakumbana na upinzani mkali kwa sababu wengi walio nje ambao wamechoka wanajitahidi kwasiliana na ndugu na jamaa zao wakiwahakikishia wako safi......UNAWAVUA NGUO PEUPE...... SEMA KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU
Teh teh teheeee aveta yako ni kiboko.......naona trafiki anapata mshiko toka kwa dereva wa daladala ya Tabata.....
 
mkuu hapa johannesburg kuna watanzania wana miaka mpaka 20 hawarudi tanzania,wengine hawana mawasiliano na ndugu zao kwa sababu ya maisha mabovu
kuna jengo hapa wanaishi watanzania karibu 1000,tunawaita machafuchafu,wamechoka mbaya hawana nyuma wala mbele,nafikiri kwa wengi inaweza kuwa sababu ya kutorudi nyumbani

Wengi hamjalijuwa tatizo la wabongo, sasa weweimagine kijana ana umri wa miaka 15 anajifanya ana uchungu wa maisha! ni uchungu upi huo? kisa kamuona kijana wa jirani katoka south Africa na used BMW.

Miaka 15 ni umri wa kuwa shuleni, through my experince in South Africa sijawahi kumuona mnigeria mwenye chini ya miaka 30, na wapo mpaka wenye 80, wengi wa hawa Wanigeria wameshapata exposure kubwa sana wameshapitapita UK, USA, na Europe in general.
kwahiyo hawa wanajuwa ni nini wanachokifanya na ndio maana South Africa ukikuta mnigeria ameajiliwa basi ni lazima atakuwa anafanyakazi profesional kama Bankers n:k.

Kitu kingine ambacho nimejifunza kwa wanigeria wenzetu kama ni marafiki au ndugu basi ni ndugu wa kweli, hawa kama ana ndugu yake yupo USA yuko tayari kumgharamia ndugu ambae yupo South Africa kwa accomodation na daily nourishment kwa kumtumia pesa kila mwezi hata kwa miaka 3 mfululizo mpaka ndugu yake atakapokuwa amesettle mambo yake.
Hawa huwafanyishi kazi Wanazofanya Watanzania pale South Africa. ogopa sana kukaa nchi ya kiingereza lakini wewe unaweza kuongea kiswahili mwezi mzima, hii ni hatari, Watanzania wanaendekeza maisha ya kukaa pamoja pamoja ndio maana akili zao ziko vile vile.
 
Nyumbani ni nyumbani tu, tena ninyi mnaoishi huko nje eti kwa sababu maisha bongo ni magumu mmekosa uzalendo kwa nchi yenu. Enzi zile za ubaguzi huko bondeni wa-Sauzi walikomaa hadi hizo siasa chafu zikakoma. Vivyo hivyo hata hapa Bongo wapo wazalendo wa kweli tutakomaa hadi kieleweke.
Kila mtu anajua nyumbani ni nyumbani kwa taarifa yako watanzania wataalam wengi wanafanya kazi nje na wanategemewa na sio kama wanapenda kufanya kazi nje wote wangependa kutumia utaalam kuwasaidia ndugu zao wanaoteseka. nawajua wengi tu waliokuwa na mawazo mazuri ya kusaidia ndugu zao wakiwa nyumbani lakini wote wamevunjwa moyo na wanasiasa wa bongo. kwa maoni yangu sababu kubwa inayofanya wengi kushindwa kuutumia utaalam wao nyumbani ni mizengwe ya wanasiasa ambao wengi wako kwa ajili ya matumbo ya matumbo yao kila utakachowaambia watakuwekea mizengwe....nitakupa mfano mmoja...kuna mtaalam mmoja wa magonjwa ya moyo alifungua taasisi sababu kubwa ya kufanya kuwawezesha wagonjwa kutibiwa hapohapo nyumbani sasa basi badala ya serikali (wanasiasa) kumuunga mkono alibambikiwa (yawezekana kweli) kesi mzee wa watu alikuwa anashinda mahakamani tuu mara kodi ya jengo sijui imefanyaje basi mbiringe tu mtindo mmoja....hata muda wa kuwatibu wagonjwa wake akawa hana... nilisikia minong'ono hapo kariakoo kuwa kumbe wale wagonjwa waliokuwa wanaenda kutibiwa nje kuna wazee walikuwa wanapata kamisheni sasa ndio wakaona mzee anataka kukata mirija yao ndio wakampa onyo. Kuna wengi tu waliokuwa na mawazo ya kuwasaidia watanzania kupitia utaalam wao lakini kikwazo kimekuwa ni wanasiasa ndio maana wengi wako huku nje wanafanya kazi huku machozi yanawatoka na huku nje hawana hiyana kwa sababu wanajua thamani yako watakupa upendacho......... Kama wewe ni mtaalam wa jambo fulani na hupendi maudhi na kuvunjwa moja una chaguzi mbili za kufanya moja uingie kwenye siasa au utokomee ughaibuni ...... ........
 
Nimechemka wapi wakati yeye amesema anaishi S.Africa? na hajatoka nje ya Africa. Please read my point b4 hujacomment
Naona alikushauri vile kwasababu mtoa mada amesema kwamba ameishi nchi kumi na moja za Afrika,na kwasasa ndiyo anaishi South Afrika.
 
Hawa huwafanyishi kazi Wanazofanya Watanzania pale South Africa. ogopa sana kukaa nchi ya kiingereza lakini wewe unaweza kuongea kiswahili mwezi mzima, hii ni hatari, Watanzania wanaendekeza maisha ya kukaa pamoja pamoja ndio maana akili zao ziko vile vile.
kumbe mara moja moja unakuwa na akili
 
Wengi hamjalijuwa tatizo la wabongo, sasa weweimagine kijana ana umri wa miaka 15 anajifanya ana uchungu wa maisha! ni uchungu upi huo? kisa kamuona kijana wa jirani katoka south Africa na used BMW.

Miaka 15 ni umri wa kuwa shuleni, through my experince in South Africa sijawahi kumuona mnigeria mwenye chini ya miaka 30, na wapo mpaka wenye 80, wengi wa hawa Wanigeria wameshapata exposure kubwa sana wameshapitapita UK, USA, na Europe in general.
kwahiyo hawa wanajuwa ni nini wanachokifanya na ndio maana South Africa ukikuta mnigeria ameajiliwa basi ni lazima atakuwa anafanyakazi profesional kama Bankers n:k.

Kitu kingine ambacho nimejifunza kwa wanigeria wenzetu kama ni marafiki au ndugu basi ni ndugu wa kweli, hawa kama ana ndugu yake yupo USA yuko tayari kumgharamia ndugu ambae yupo South Africa kwa accomodation na daily nourishment kwa kumtumia pesa kila mwezi hata kwa miaka 3 mfululizo mpaka ndugu yake atakapokuwa amesettle mambo yake.
Hawa huwafanyishi kazi Wanazofanya Watanzania pale South Africa. ogopa sana kukaa nchi ya kiingereza lakini wewe unaweza kuongea kiswahili mwezi mzima, hii ni hatari, Watanzania wanaendekeza maisha ya kukaa pamoja pamoja ndio maana akili zao ziko vile vile.

umenena ukweli aisee, watanzania wengi hatujui kutumia opportunities tunazozipata pindi tunapofanikiwa ughaibuni. Wenzetu wakenya na west africans ni mabingwa wa kuwavuta wenzao kufika ughaibuni. Unakuta mkenya mmoja kavuta nduguze kama kumi hivi. Hao nao kila mmoja anavuta wengine kumi sasa pata picha huo mtiririko. Au ndio kusema watanzania ughaibuni hatupafagilii? tumezoea shida za bongo.
 
mkuu hapo sikupati,je uwezo wako binafsi ukoje mpaka umlete ndugu yako maisha haya?
utakuwa umejizatiti vizuri,sikubaliani na hali ya kumwalika ndugu yako wakati mambo yako bado ovyo,
 
Wengi hamjalijuwa tatizo la wabongo, sasa weweimagine kijana ana umri wa miaka 15 anajifanya ana uchungu wa maisha! ni uchungu upi huo? kisa kamuona kijana wa jirani katoka south Africa na used BMW.

Miaka 15 ni umri wa kuwa shuleni, through my experince in South Africa sijawahi kumuona mnigeria mwenye chini ya miaka 30, na wapo mpaka wenye 80, wengi wa hawa Wanigeria wameshapata exposure kubwa sana wameshapitapita UK, USA, na Europe in general.
kwahiyo hawa wanajuwa ni nini wanachokifanya na ndio maana South Africa ukikuta mnigeria ameajiliwa basi ni lazima atakuwa anafanyakazi profesional kama Bankers n:k.

Kitu kingine ambacho nimejifunza kwa wanigeria wenzetu kama ni marafiki au ndugu basi ni ndugu wa kweli, hawa kama ana ndugu yake yupo USA yuko tayari kumgharamia ndugu ambae yupo South Africa kwa accomodation na daily nourishment kwa kumtumia pesa kila mwezi hata kwa miaka 3 mfululizo mpaka ndugu yake atakapokuwa amesettle mambo yake.
Hawa huwafanyishi kazi Wanazofanya Watanzania pale South Africa. ogopa sana kukaa nchi ya kiingereza lakini wewe unaweza kuongea kiswahili mwezi mzima, hii ni hatari, Watanzania wanaendekeza maisha ya kukaa pamoja pamoja ndio maana akili zao ziko vile vile.

mkuu ukipita mitaa ya jhb utashangaa vitoto vya kibongo vilivyojazana pale,vidogo mno,uwezo wa kupambana na maisha ni mdogo sana kwao
 
mkuu hapo sikupati,je uwezo wako binafsi ukoje mpaka umlete ndugu yako maisha haya?
utakuwa umejizatiti vizuri,sikubaliani na hali ya kumwalika ndugu yako wakati mambo yako bado ovyo,

Mpaka ufikie kumualika nduguyo inamaana hali yako kiuchumi inaruhusu. Kumbuka nchi za wenzetu huwezi kumualika mtu kama akaunti yako imechoka. Hasa nchi za Schengen wanataka wajue una kiasi gani benki, nyumba unayoishi ina nafasi ya kuongeza mtu na kama una uwezo wa kumlipia health insurance kwa kipindi atakacho kaa kwako. Upo hapo. Bila kutimiza haya masharti huwezi kumvuta mtu legally.
 
Dunia ya leo bila elimu hakuna utakalo fanya, japo wapo wachache sana wanaofanikiwa bila elimu. Kuvuta kumleta dunguyo kama si kwa ajili ya shule, yani shule ya ukweli basi utakuwa unampoteza.

ukiangalia wengi wanaovutana mfano wavietnam, wachina, wahidi nk, hawa wanapoletana wanakuwa tiyari wana biashara zao ambazo mtu akifika tu tayari anaiingizwa dukani kuuza ama kufanya kazi anatafutiwa makaratasi. Ni rahisi tu mfano kama wewe una duka lako na unataka kuajili ndugu yako unatangaza kazi harafu qualification zake unaweka awe anajua kuongea na kuandika kiswahili sanifu.

Mnigeria na wacongo, japo huwa kuna sehem naona tunajaribu kuwadharau lakini wanatuacha mbali sana na ndio maana utakuta wengi wanafanikiwa kuliko wabongo.

Kitu nyingine, mfano wachina, kuna nchi wananchi wanapewa makusudi loan na serikali zao kwenda kuwekeza ktk nchi zingine, na ndio maana wanafanikisha hata kuvutana pia kukuza uchumi wa nchi. Mfano kwa bei ya kahawa kwa wakulima wa tz ni kiduchu, basi serikali inatafuta wazaliwa wa tz na wenye makaratasi tuseme ya EU, basi hawa watz-EU wanafungua vijimaduka kwa kama local. Na wanakuwa wanatoa bidhaa moja kwa moja bongo na kuiuza hapa kwa bei nzuri kabisa. Hii inakuwa biashara virtually ya serikali kwa kupitia wazawa.

Mfano kule Tabora kuna asali nyingi kweli wakati ndani ya EU, asali bei yake si haba. Serikali si lazima iingize pesa kwa kutengeneza maviwanda makubwa. Kwa hiyo kwa mtaji huo, ukiwa na vijisehem vya namna hiyo ulaya kote, kinachofuata unahakikisha fedha haipotei kwa kuwalipa watu wa nje mshahara, basi unawavuta watz wafanyakazi, kwa namna moja ama nyingine unakuwa na uhakika hizo pesa lazima atamtumia shangazi , binamu yake nk.
 
wakuu, tunapenda kurudi nyumbani sema matatizo ya huko yamezidi

1. umeme
2. foleni
3. kazi za kujuana
4. maisha bado magumu sana

nitaendelea kubeba box bwana..
 
Wapendwa nitatoa maoni yangu binafsi. Wazo la kuwa nje ya nchi au kusettle nyumbani linachangiwa sehemu kubwa na uchumi. Ni sawa na yule aliye-relocate toka Nchinga-Mtwara kuja Dar es Salaam. Lakini pia kuna suala la feeling za ki-binadamu; hebu fikiri.. umeamua kurudi home baada ya kuangaika sana..na hela zako umeweza pata kagari kako kamtumba...umepiga kiyoyozi unapita pale kituoni..watu wamejaa ile mbaya hakuna usafiri..roho inakuuma ..Ok,,, unarudi nyumbani ambako umeweka Kagenerator pale nyumbani..baada ya Tanesco kuishiwa umeme..wakati kagenerator kanaunguruma na unapata mwanga..Nyumba ya jirani hakuna umeme..watoto wachanga wa majirani wanalia unasikia huruma ..dhamira inakusuta.unaangalia utawaze kusaidia jirani..lakini masikini kagenerator kenyewe kadogo..Anyway... una kajumba kako umeweka uzio mzuri..lakini kila siku vibaka wanakusumbua.Unaamua kuchukua wamasai..kesho yake wamasai wanafanya nyumba yako ndio Ngome..wanawaleta wenzao kushinda..Unaona karaha unawatimua..Ok.. Unaanza na ka Investment..uanpata kahela ambako kanakuwezesha kubadili mboga .lakini extended family kuna watoto wanataka shule, ndugu wengi maisha magumu..unajitahidi kusaidia unashindwa... Anayway...Unajaribu kujiliwaza kwa kuangalia TV ..au kusikiliza Taarifa ya habari ..unasikia utumbo wa wanasiasa wanaoshindwa kuwathamini wananchi...wanagombana wenyewe kwa wenyewe chama A and B..Mafisadi na walalahoi..Unaudhika kwani kuna ka chama kanajaribu kuwatetea walalahoi na kuna kachama kanajaribu kuwatumia walahoi hao hao kuwatetea maslahi ya matumbo yao na mafisadi..unakasirika na kuzima TV....Unaamua kuondoka.. unatoka kidogo traffic anakukamata..huna tatizo..lolote..kwani Maisha uliyoishi nje yamekunja ki-discipline..Huyu Traffic anazunguka gari.. ..anajenga hoja,,Fire Extinguisher ni ndogo kwa ukubwa wa gari ..Mnabishana sana..anaishia kukwambia ukweli anataka kahela akapate supu..unakasirika unampa unaondoka huku Moyo ukidunda kama unataka kutoka kwa hasira....Mbele kidogo unasimama ..umeshaamua ku - postpone kurudi settle..home ..Unaandika kwenye Face-book..kwa marafiki zako.. "Aluta -kontinua..Narudi ughaibuni" Binafsi unajipa moyo..wacha nikaangaike kidogo kama miaka miwili au mitatu nitarudi home..Well, ni -round nyingine umeshindwa ku-settle --ingawa ulikuwa na nia ya kweli..

Ndugu zangu, ukiondoka tu Tanzania ..wewe tayari u-second class citizen..hata kama utapata makaratasi, dual citizenship etc. Hasa pale dhamira yako itakapokuwa inakusuta wakati wa lile swali ambalo silipendi... "where r' u from? Unakumbuka ..Nikiwa nyumbani Tanzania hakuna anayeniuliza hilo swali....

Conclusion -- Umasikini wetu watanzania..na mazingira ya siasa na uchumi wetu vinatuchanganya sana kupata wazo la ku-settle home.. Ingawa, ni kweli ni kuna mifano mizuri ya rafiki zetu wengi wamesha-win baada ya kurudi.yaani wameweza kujibadili ghafla na kukumbatia tena maisha ya nyumbani..Lakini kama kweli ulikulia nyumbani kwenye umasikini.na maisha ya dhiki halafu..tukatoka nje ya nchi Uka-experience kwa kuishi kwa utii wa sheria, Kupata hela kwa kipato halali bila kuomba rushwa, kutokuwa na shaka na vibaka, kutosikia Miziki ya mafisadi..Jamani inakuwa ngumu kuchukua maamuzi ya kurudi nyumbani kwani unajua unaenda kutoa rushwa, unaenda kugombana na utii wa sheria..unaenda kwenye umasikini ule ule ambao unajua ni umasikini wa kujitakia...Yaani inachanganya kweli lakini, All in All...Tutarudi tu..kwani ni nyumbani pekee ambako unakuwa "First Class Citizen"

Aisee... Nani ka-comment na hii Topic imerudi tena jamvini... Hahahahah .. Ni mwaka umepita baada ya Tulizo kukata shauri na kurudi Home kujenga Taifa letu .. It has been a unique experience kujibadili na kujifundisha ki-saikolojia na mawazo ili kukumbatia mazuri na mabaya ya hapa Home...Kama Ukiweza ni maisha ya furaha..hata kama itabidi kila siku utatenga buku mbili kuhonga Traffic njaa au kuwaza Sight Mirror ya gari yako itaibiwa lini au kuvunjwa na vijana waosha magari kwenye Traffic lights..Sweet n' Sour life in Bongo!
 
Bora umewapa vijana angalizo. Wengi hufikiri ukitoka sawa na kupata diploma, ukifanikiwa umepata degree. Ni vema mtu kwenda ughaibuni ukiwa na mpango mahsusi sio kuzamia tu.
 
Bongo tatizo njaa imekua kali sana watu wanashindia mlo mmoja...mbuzi,ng'ombe hadi mbwa wanagombea kula magazeti ya uhuru na mzalendo.......piga ,ua,garagaza au ikibidi weka kwenye sanduku la chuma fungia na kufuli la Yale ...lazima nitoke niishi ulaya au huku nilipo....sirudii bongo ng'ooooo maisha ni magumu...nilikua huko hamna lolote watu wanaongea tuuu na sifa za kijinga!!!mtu unamkuta na magari yao cjui verosa au gx 110 kila siku gauge iko empty ila anajidai ana gari....kwenye mlo ndo balaaa.....nyama nyama kila sehemu ..vyakula gani hivyo unhealthy food...ndo maana utaona wanaume na wanawake wote wana mimba(vitambi)....piga ua garagaza bongo sirudiii banaaaaa.
 
Back
Top Bottom