Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania

Nikimuona kocha wa taifa starz ama the vice president himself daaah nachoka hata mawazo ya kurudi böngo yanatoweka!nimewataja wachache 2 sema kuna vizee kibao kila sector wanang'ang'ana kama kupe!!ful uchawi!itabaki historia tu kwamba nilizaliwa tanzania!inatia sana uchungu hadi landlockd country rwanda,malawi,burundi,uganda zambia wana2acha kila kitu,sio tu kiuchumi!

Nyumbani ni nyumbani tu, tena ninyi mnaoishi huko nje eti kwa sababu maisha bongo ni magumu mmekosa uzalendo kwa nchi yenu. Enzi zile za ubaguzi huko bondeni wa-Sauzi walikomaa hadi hizo siasa chafu zikakoma. Vivyo hivyo hata hapa Bongo wapo wazalendo wa kweli tutakomaa hadi kieleweke.
 
Asante kwa kutuwezesha kujua kumbe hapa nyumbani Tz tuna neema sana. Kuolewa na kibibi kizee?? Ngongongafu!!!!!

"........iyo kupata kazi inakuwa Tabu sana matokeo yake wanakuwa ni wezi,majambazi, Wauza unga, kuna watu wengine wanalal nje kwa sababu hawana pesa za kulipa kodi ya nyumba na kodi ya nyumba kwa mwezi ni dola 300 au Dola 500 kwa mwezi ,na mengineyo mengi tu.

Jamani mimi nimeishi nchi nyingi sana na kutembelea baadhi,ninachojiuliza hawa wanaoshindwa yote wakati wamefika kwenye nchi yenye neema zaidi kidogo ya nchi uliyotoka,yaani unashindwa hata kuoa,kuolewa au kufanya chochote ukawa na maisha yaliyo bora kuliko uliyokuwa nayo TZ?Mimi nimeishi Sweden,Finland,UK, Japan,Poland, US kote huko ukitangaza kuolewa na mama Kibonge yaani ni mara moja au kama ukitangaza kumuoa bibi kizee ni mara moja,ukivumilia 10 years huwezi kurudi mtupu,nimeuliza Pretoria kuna mtu anaunganisha watu ingawa bahati mbaya ni kina bibi wa ki Israel wakikuooa inabidi ufanye kazi sana on the bed na yeye kazi ya kupika,kuosha mbwa nk ni juu yako lakini mvumilivu hula mbivu,lakini kwa wali soma nina imani kazi sio shida ila kazi ya kulipwa kiasi gani ndio shida-njooni huku Iceland,ukiingia ni pm,niliolewa 7 yrs lakini sasa mambo yangu si haba na nimerudi nikamuoa mswahili na mambo si mabaya. Ugali na maharage ndio vilivyonifanya nikapata akili-nyumbani pazuri lakini kwa mwenye kujua akiamka anaelekea wapi na ni bora kibaka wa SA au dunia nyingine kuliko wa TZ ukishikwa hata jela hufiki jamaa wameisha kuchoma moto.Mimi popote ninapoweza kuishi bila kubaguliwa au kubaguliwa kwa %ndogo naishi tu kuliko kujidai uzawa ukaenda kufa na njaa.
 
Mzee East Europe hujanipeleka,bora nifie hapahapa ,wapo kibao hapa sa wanauza unga,wengi wanatoka yugoslavia!wamechoka mbaya!
Mimi hata kama nipo Eastern Uerope nafanya biashara baina ya Estern Uerope na Tanzania mambo

yangu sio mabaya hivyo namshukuru Mwenyeezi Mungu natia mkono kinywani bora huku nilipo kuliko Tanzania nasikia hukon kwetu hata Umeme wa Mgao? Maji Safi hakuna njaa ya kumwaga ukiumwa tu unalichungulia Kabuari hamunioni n'goo jamani ingawa Nyumbani ni Nyumbani lakini

Shida tupu uongozi bora hakuna kila siku matatizo huku hakuna siku umeme ukakatika ovyo ovyo kama huko kwetu nyumbani nasikia kariakoo ikifika wakati wa usiku Vin'gora vya Generator za umeme kila mahali utafikiri mupo viwandani Maisha yamekuwa magumu Viongozi bora hamna wizi mtupu jamani hakuna maendeleo hapo nyumbani kwetu . Huwezi kufananisha Tanzania na nchi za Eastern Uerope? Tanzania ni nchi Masikini na haina maendeleo kabisa.
 
Nyumbani ni nyumbani tu, tena ninyi mnaoishi huko nje eti kwa sababu maisha bongo ni magumu mmekosa uzalendo kwa nchi yenu. Enzi zile za ubaguzi huko bondeni wa-Sauzi walikomaa hadi hizo siasa chafu zikakoma. Vivyo hivyo hata hapa Bongo wapo wazalendo wa kweli tutakomaa hadi kieleweke.
Mtakomaa na kuzidi kuahribikiwa kimaisha maisha ya nyumbani yamekuwa magumu sana jua kali hakuna maendeleo yoyote yale ujambazi huku nyumbani umezidi wizi wa simu ndio usiseme njaa tupu bongo imekwisha kufa tangu miaka ya 1980 Tangu alipojiuzulu uongozi Baba wa Taifa Mwalim nyerere viongozi walibakia wamekuja kuiuza nchi na kuimaliza kaeni mpaka mujionee wenyewe mwisho wake.
 
nimebakia na miaka mitatu,wakinipa uraia hapa sirudi tena,bora niendelee na safari kwenye nchi kubwa zaidi,
 
Maisha Tanzania kwa ujumla wake ni mazuri sana kama mtu ukijipanga vizuri, kwa kuwa kuna kila aina ya vianzio vya maisha kama ardhi nk, na ni rahisi kuanzisha biashara hata ndogondogo kuliko hizi nchi za nje ambazo ni vigumu sana kujikwamua.
Lakini huo msingi wakuanza hiyo Biashara utaupata wapi?
 
nina miaka 9 sijaja tanzania mkuu

Kutoka Johanesburg mpaka Dar es salaam ni kilomita 5000 tu, sasa mkuu kukaa miaka 9 nje ya kwenu kwa umbali wa km 5000 huoni kama unachekesha!
South Africa wapo wanaokwenda kwa baiskeli kutokea Dar es salaam, sasa ni aibu kuongea hilo mbele ya wanaume wenzako. wewe kimbia tu ukirudi utakuta sisi wengine ndio shemeji zako, tumeshazalisha dada zako.
 
Mkuu thabo mbeki mimi nilianzisha thead hii https://www.jamiiforums.com/habari-...u-kurudi-nyumbani-tuwasaidiaje.html?highlight= nikatoa na sababu kwa nini wengi hawataki kurudi, si kwa sababu wanamaisha mazuri ila ni matatizo mbalimbali waliyonayo pamoja na aibu wanayoona wataipata wakijilinganisha na wenzao waliowaacha nyumbani miaka 10 iliyopita. Unajua wakifika nje wakipata ki vauxhall cha miaka 10 na mziki mzito wanaona maisha ndiyo hayo.
 
Njooni US.
US kuna shida zake na raha zake. Ukiingia shule make sure unaachana na ungwini. Ukisoma ungwini ndio hayo ya kuwa na PhD halafu huna kazi ya maana. Ila ukipiga medicine/science/tech majors katu hufi njaa. Uzuri wa US mwenyeji, mgeni mhamiaji mzamiaji kule makazini kodi mtakatwa sawa, benefits mtapata sawa, na salary ni wewe mwenyewe utakavyonegotiate wakati ukipewa job offer. Sheria zipo na hakuna atakayekunyanyasa as long as you are legal. Nimekuja hapa sina mbele wala nyuma, nikaingia shule (BSc-Computer Science na baada ya graduation IBM walinifailia HB1 then nikajapata greencard na sasa ivi ni raia. Bongo ni home na huwa nakuja every December. Bado niko na IBM. Offers zinakuja kila siku nazikimbia.
Mshahara unanitosha nalipa mortgage na bills zoootee na bado ninakuwa na hela ya kuchezea. Nyumbani nimeshajenga kulee Bunju na nimepangisha.
Msiwatishe watu, njooni kutest american dream bado US ina opportunities. Kila mtu na bahati yake. Ni akili yako tu. ukilaza akili basi utapiga box maisha yote. Karibuni sana. Msiogope. Watu wa mataifa yoote duniani kila kukicha wanapiga mitkasi ya kuingia hapa. Karibuni sana na anaewatisha basi ndio hao watu wa Europe na S. Africa. USA is USA. Karibuni sana msiogope
 
...kuna ukweli mwingi sana...

maisha ni popote, muhimu ni malengo. Chukulia mfano wa wamachinga!
kuna waliokuja Dar na kunufaika sana na biashara na mbinu nyingine za maisha. Hao
walijiwekea malengo.

Labda leo hii nao wameweza ajiri japo banda la mitumba, nk...lakini kuna
walioshindwa kabisa mbinu za maisha mjini, wakaishia kuwa vibaka....wengine wateja wa unga. maisha yao yamekwama, kurudi vijijini wanaona haya, au utamu wa mataa na magari mjini yeshawanogea japo usiku wanalala stendi.

Chukulia mfano wa vijana wa kimassai waliojaa mjini sasa. 'Morani' wengi wamekimbilia Dar na Zanzibar kwa matarajio ya maisha matamu ya mjini, wengi wao wameishia kazi za ususi, ulinzi, na kuzurura mjini wakiokoteza kazi ndogondogo...wengi wamesahau thamani ya ng'ombe zao huko vijijini kwa tamaa ya maisha bora mjini,....naamini kuna wengi wanaona hata haya kurudi kwao.

Wachagga ni Issue nyingine...LOL!

Huku nje ndio hivyo hivyo...
it's all about someone's vision na jinsi anavyojipanga kufikia malengo yake,
bila kusahau bahati (being at the right place, at the right time with clear goals!)

Kutoka Johanesburg mpaka Dar es salaam ni kilomita 5000 tu, sasa mkuu kukaa miaka 9 nje ya kwenu kwa umbali wa km 5000 huoni kama unachekesha!
South Africa wapo wanaokwenda kwa baiskeli kutokea Dar es salaam, sasa ni aibu kuongea hilo mbele ya wanaume wenzako. wewe kimbia tu ukirudi utakuta sisi wengine ndio shemeji zako, tumeshazalisha dada zako.

miaka 9 ni mingi sana
 
Mkuu thabo mbeki mimi nilianzisha thead hii https://www.jamiiforums.com/habari-...u-kurudi-nyumbani-tuwasaidiaje.html?highlight= nikatoa na sababu kwa nini wengi hawataki kurudi, si kwa sababu wanamaisha mazuri ila ni matatizo mbalimbali waliyonayo pamoja na aibu wanayoona wataipata wakijilinganisha na wenzao waliowaacha nyumbani miaka 10 iliyopita. Unajua wakifika nje wakipata ki vauxhall cha miaka 10 na mziki mzito wanaona maisha ndiyo hayo.

mkuu hapa johannesburg kuna watanzania wana miaka mpaka 20 hawarudi tanzania,wengine hawana mawasiliano na ndugu zao kwa sababu ya maisha mabovu
kuna jengo hapa wanaishi watanzania karibu 1000,tunawaita machafuchafu,wamechoka mbaya hawana nyuma wala mbele,nafikiri kwa wengi inaweza kuwa sababu ya kutorudi nyumbani
 
...kuna ukweli mwingi sana...

maisha ni popote, muhimu ni malengo. Chukulia mfano wa wamachinga!
kuna waliokuja Dar na kunufaika sana na biashara na mbinu nyingine za maisha. Hao
walijiwekea malengo.

Labda leo hii nao wameweza ajiri japo banda la mitumba, nk...lakini kuna
walioshindwa kabisa mbinu za maisha mjini, wakaishia kuwa vibaka....wengine wateja wa unga. maisha yao yamekwama, kurudi vijijini wanaona haya, au utamu wa mataa na magari mjini yeshawanogea japo usiku wanalala stendi.

Chukulia mfano wa vijana wa kimassai waliojaa mjini sasa. 'Morani' wengi wamekimbilia Dar na Zanzibar kwa matarajio ya maisha matamu ya mjini, wengi wao wameishia kazi za ususi, ulinzi, na kuzurura mjini wakiokoteza kazi ndogondogo...wengi wamesahau thamani ya ng'ombe zao huko vijijini kwa tamaa ya maisha bora mjini,....naamini kuna wengi wanaona hata haya kurudi kwao.

Wachagga ni Issue nyingine...LOL!

Huku nje ndio hivyo hivyo...
it's all about someone's vision na jinsi anavyojipanga kufikia malengo yake,
bila kusahau bahati (being at the right place, at the right time with clear goals!)

What about wale (ambao ndio majority) wenye vision ila hawajaweza kufikia malengo yao, bila kusahau wasio na bahati (being at the wrong place, at the wrong time even with no clear goal?). Nadhani hawa tuwaencourage warudi kwenye nchi yao. Waje wajaribu nako huku pengine ndipo bahati yao ilipo.
 
THABO MBEKI.....unakumbana na upinzani mkali kwa sababu wengi walio nje ambao wamechoka wanajitahidi kwasiliana na ndugu na jamaa zao wakiwahakikishia wako safi......UNAWAVUA NGUO PEUPE...... SEMA KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU
 
mkuu kuna kweli zaidi ya hiyo niliyoweka hapa jamvini?
 
Back
Top Bottom