Tanzaniaist
Senior Member
- Nov 29, 2011
- 161
- 156
Habari wanaJF..!
Kwa muda sasa kumekuwa na mijadala mingi ikiilenga Rwanda, Paul Kagame na hususani kabila la Watutsi..!
Na hili suala limekolezwa zaidi na mch.Christopher Mtikilia ambaye ni mwanasiasa hodari hapa nchini Tanzania na pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha DP.,kupitia waraka wake ambao mimi nauona ni wa kichochezi,uwongo,chuki na propaganda
Zisizokuwa za msingi ambao wenye malengo ya kupotosha ama kuleta uchochezi na mauji.
Najua kuna baadhi watapingana na mimi lakini kwa wale waliosoma historia watanielewa.
Nianze kwanza,..nini chanzo cha uhasama baina ya Wahutu na Watutsi..?
Kabla ya Ukoloni makabila haya mawili walishabihana na hata kuwa na lugha moja Kinyarwanda upande wa Rwanda
na Kirundi upande wa Burundi ingawa watutsi ndio walikuwa watawala kwakuwa walikuwa na utajiri mwingi wa ng'ombe maarufu "ankole" na hata pia tukiangalia hapa Tanzania Ufalme wa Karagwe ulikuwa na mchanganyiko wa Watutsi, Utawala wa Bachwezi na tawala mbali mbali kanda ya ziwa kulikuwa na mchangiko wa watutsi kabla ya ukoloni mwaka 1885..!
Wakoloni waliikiingi na Mkakati ulioitwa "Wagawanye na uwatawale".,na ulifanikiwa sana Kama nchini Nigeria baina ya Wakristo na Waislamu, Kenya baina ya wakikuyu na wajaluo,wakalenjin. ndio maana hata hapa Tanzania mikoa yenye wakristo wengi ilipata sana fursa ya elimu,miondombinu kuliko mikoa yenye waislamu wengi.
Tukija Rwanda huko zilianza taratibu za kuangalia pua,muonekano ambako waligawanywa kama Watutsi na Wahutu na hata kuvalishwa vibao.,ambako wale walioitwa watutsi walipewa fusra kubwa sana kwenye elimu na utawala na wakoloni ambao walikuwa wajerumani kisha wabeligiji..! mwanzo hawa watu walikuwa kama familia,ukoo na kabila moja paka kuweza kuwa na lugha moja na hata pia vinasaba vinaonyesha watutsi wana mchanganyiko na wenzao wahutu..!
Uhasama mkubwa uliibuka pale mwaka 1959,..ambako watutsi wengi walihamia Uganda,Congo na Hata Tanzania mpaka mwaka 1994 ambako yalitokea mauji ya kimbari na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000,000. kwa kifupi hii ndo historia fupi ya watutsi unaweza ukapata habari nyingi zaidi ya hapa.
Tuje kwenye waraka wa Mchungaji Christopher Mtikila,..ambao hauna tofauti na waraka uliosambazwa mwaka 1994 na
kusababisha mauji ya kikatili, wanawake na watoto kubakwa, miondombinu ya uchumi kuharibiwa vibaya..,na mtu kama huyu mahali pake hapa duniani ni Jela tena kifungo cha Maisha na hata peponi ni Jehanamu. ni kitu kibaya sana kuona Binadamu anapenda kuona vifo au mvurugano wa nchi ambayo sasa hv ina amani wakirudi tena katika mapigano. Mchungaji Mtikila ametumia mifano mfu na ya uongo kutetea hoja zake.
1.Suala la wafugaji kuingia bonde la Burigi, hili ni tatizo la serikali yenyewe kutolinda mipaka yake kuanzia maafisa uhamiaji, na hata kuliibuka baadhi ya tuhuma wafugaji kuonga wenyeviti wa vijiji ili waweze kupitisha ngombe. na hili suala limekuwa sugu sana, mfano tukiangalia hata kwenye ziwa letu Victoria Wakenya na Waganda wanakuja kuvua kwenye maeneo yetu na hata mbunge wa Ukerewe Mh.Machemli alishawahi kuja kulalamika bungeni, na hata baharini tukikumbuka wale samaki wa Magufuli walikuja kuvua kwenye mwambao wetu wa Bahari., hili tatizo la wageni kuvamia Rasilimali zetu ni Tatizo la Serikali kushindwa kulinda mipaka yake dhidi ya wavamizi ndio tatizo la wafugaji wengi kutoka Rwanda na Hata Burundi kuvamia maeneo yetu ya hifadhi. ndio maana imekalia kimya waraka wa Mch.Mtikila
kwani kwenye maeneo ya mipaka kuna tatizo kubwa sana la Rushwa.. na ningependa nimdahamishe Mch.Mtikila wanaovamia Rasilimali zetu sio tu watutsi hata pia Wakenya na Waganda ziwa Victoria,Wachina Bahari ya Hindi ni muhimu Serikali kuzidisa ulinzi kwakuwa wana Polisi na Jeshi.
2.Suala la Kagame Kupendeza Wanyarwanda 35,000. hivi nchi yetu haina usalama wa Taifa, haina idara ya uhamiaji, haina idara ya intelejensia polisi. kumbuka kuna makabila ya wahaya,waangaza,muha na wanzinza ambao wamenyangika na watutsi hata kabla ya Ukoloni mwaka 1885. na kumbuka nchi yetu imetoka uraia kwa baadhi ya wakimbizi kutoka makambini ambao walikuwa wahanga wa vita. ndio maana nchi kama Canada,Norway na Sweden wametoa uraia sana kwa wasomali ambako kwa akili ya mch.Mtikila angemaanisha wale wametumwa na Al shabaab. Mch.Mtikila hujui maana ya vita.
3.Suala la ''Black Apartheid" na kufanisha watutsi na nyoka., hapa sitaki kuongea sana lakini Mzungu ama Mhindi atamcheka sana Mwafrika kama anambagua mwenzake kisa kabila,ama rangi au dini.,
4.Mwisho ni nikija kwa PAUL KAGAME, Historia yake inasemakana amwaka 1979 alihshiriki vita ya TANZANIA dhidi ya nduli IDD AMINI DADA chini ya YOWERI MUSEVENI akiwa upande wa Tanzania kisha kushirikiana na Museveni mwaka 1985 ambako alikuwa mkuu wa Intelejensia wa jeshi la Museveni, hadi kujiunga na jeshi la Uganda Museveni alipokuwa Rais na kupelekwa Grand Rapids Nchini marekani kwa mafunzo zaidi ya Kijeshi, ambako aliiwezesha jeshi lake la RPF kutumia mbinu mbadala kuliteka jiji la Kigali dhidi ya serikali ya kipindi hicho.., Mchungaji Mtikila una habari kwamba WATUTSI wengi ambao wewe unawaita NYOKA walishiriki kwenye vita ya Ukombozi wa Watanzania mwaka 1979 dhidi ya IDD AMINI akiwemo hayati mtutsi FRED RWIGEYMA na hata baadhi ya Kufa kwaajili ya Taifa letu wakati wewe ukiwa kwenye handaki umejificha. mwenzio PAUL KAGAME alizaliwa ndugu zake wakichinjwa na kujikuta amekulia kambini., its fair kumuita muuaji bila ushahidi wakati wewe umefaidi matunda ya amani chini ya mtu unayemdharau Baba wa Taifa., think twice Mtikila huku ukikumbuka maumivu ya kupigwa jiwe huko Tarime kwa uchochezi wako.
Ningependa Watanzania Tusishabikie vitu visivyokuwa na Msingi wakati nchi yetu ikiwa na Matatizo makubwa ya Ajira,Afya,Umeme,Maji,Miondombinu na N.k juzi wenzetu Brazil walipinga Matumizi makubwa ya maandalizi kombe la Dunia Nchini mwao,..sisi leo tunafurahia Serikali kupeleka Jeshi Nchini Congo.,wakati nyumba za Polisi zikiwa katika hali mbaya mfano zile kota za kariakoo msimbazi. ni masuala ya kujiuliza kitu gani kina faida nchini mwetu. kuna mtu hapa jamvini alitoa hoja watutsi watimuliwe nchini kwa msingi hiyo basi mikoa ya Kagera,Kigoma tuindoe kwenye ramani ya Tanzania kwani watutsi ni ndugu zao na hata lugha moja wanaongea. ikiwemo kirundi na kinyarwanda.
Tukiangalia Nchini zilizoendelea Kama MAREKANI,UMOJA WA FALME ZA KIARABU NA AFRIKA KUSINI, hizi nchi ni mchanganyiko wa mataifa mbali mbali, ww Mtanzania hujishughulishi anakuja Mkenya,Mnyarwanda anafanya maendeleo kwenye Nchi yako then unaaznisha maneno ya uchochezi wakati ni udhaifu wako wa kutojiendeleza. Tanzania ni nchi yenye rasimali kubwa sana ya ardhi lakini hatuitumii vizuri kuzalisha na kuongeza pato la Taifa kwanini wageni wasitutolee macho, mi naona waje tu kutusaidia kwasababu tumeshindwa.

Naona nianze na historia kwanza kwa faida ya wasomaji coz' naona hii ya kwako haija-expose vizuri chanzo cha uhasama kati ya Wahutu na Watusi!
HISTORIA FUPI: Hapo awali eneo ambalo hivi sasa ni Rwanda na Burundi hapakuwa na watu ambao wanafahamika kama Watusi hivi sasa; kwa maana hiyo, asili ya watu wa eneo hilo ni Wahutu!
Watusi walitokea Ethiopia, na kama ilivyokuwa enzi hizo, walipofika eneo ambalo sasa ni Rwanda na Burundi, Watutsi waliwavamia na kuwashinda vita wenyeji; Wahutu! Kimsingi, the guys(Tutsi) ni warriors since then kama yalivyo makabila mengi ya wafugaji....labda ni kwavile wameshazoea kufukuzana na wanyama wakali katika kulinda mifugo yao; tofauti na mkulima; yeye akimuona simba au chui atakimbia; by the way si simba wala chui anayekula mahindi lakini ukisusa mifugo kwa hao jamaa, imekula kwako (Hapo kwenye RED, tafsiri ni yangu kwahiyo msinidai ushahidi kwavile sina)!!!
Wakati wa ukoloni, Wakoloni waliwatumia sana Watusi kuwa-oppress Wahutu coz' Watutsi wao ndo walikuwa watawala. Inasemekana oppressing ya Watusi kwa Wahutu ilikuwa kubwa sana pengine kuliko sehemu zingine barani Afrika. Na wata Walipoingia Wabelgiji baada ya WWI, wakaendeleza hali hii, ya kuwatumia Watusi kuwa-opress Wahutu!
Lakini cha ajabu, wakati Wabelgiji wanakaribia kuondoka, wakaanza kuwaingiza baadhi ya Wahutu madarakani. Later on, kwa ushawishi wa kanisa Katoliki, Mchungaji wa Kihutu akatoa Waraka wa kuitaka Ubelgiji kukabidhi madaraka kwa Wahutu! Sujui kwanini RC waliwa-favor Wahutu, sina uhakika labda kwavile Wahutu walikuwa ni oppressed community or kutokana na ukweli kwamba kwa kawaida Wakulima walikuwa na muda wa kushiriki dini za wazungu kuliko Wafugaji na hivyo bila shaka Wakulima(Wahutu) wengi zaidi walikuwa wamempokea YESU kuliko Wafugaji Watutsi na hivyo RC kuamua kutoa upendeleo kwa waumini wao Na in fact, labda hapo ndipo unaweza kuona ni kwa vipi Kanisa lilihusika na mauaji ya kimbali kwa namna moja au nyingine!(Kwa mara nyingine, hapo kwenye RED, tafsiri ni yangu kwahiyo msinidai ushahidi kwavile sina)!!!!
Aidha, kufuatia Waraka huo, Wahutu wakaanzisha vyama vya kisiasa kama njia ya kujiandaa kutwaa mamlaka kutoka kwa Mkoloni Mbelgiji. Na historia inasema kwamba hata uanzishwaji wa vyama hivi ulisimamiwa na Kanisa!
Wakati Wabelgiji wamekaribia zaidi kuondoka, ukaitishwa uchaguzi ambapo (wengine wanasema wa kimagumashi) na chama cha Kihutu kikashinda! To make things even worse, pakapigwa kura ya kama Ufalme uendelee kuwapo au ufutwe! Tusisahau, ufalme ulikuwa unashikiliwa na Watusi wachache ambao ndo walikuwa wenye nguvu...this means that, mshindi huyu wa Kihutu alikuwa chini ya Ufalme wa Kitutsi! Hata hivyo, kama ilivyotarajiwa, wengi waka-vote against Monarch na hivyo Mhutu aliyechaguliwa akapata wasaa wa kujinafasi!! Na hivyo, mwanzoni tu mwa utawala wake akaanza kuwashighulikia Watutsi ambao walikuwa madarakani! Na katika kipindi kifupi, Watusi wakaonja joto ya jiwe kwani walishughulikiwa kila idara na wengi waliuawa na wengine wakaikimbia Rwanda! In short, ni kama walikuwa wanalipiza kisasi cha kuwa oppressed for centuries!
Hali hii ya uhasama iliendelea na kuja kuzalisha mauaji ya kimbali ya 1994 ambayo chanzo chake ni kutunguliwa kwa ndege ambayo ndani kulikuwa na Rais Habyarimana ambae alikuwa ni Mhutu!
SASA TURUDI KWENYE MADA:
Kwanza ni kweli kabisa uvamizi wa wageni ndani ya ardhi ya Tanzania unatokana na udhaifu ulio ndani ya uwezo wetu wenyewe! Hata hivyo, hilo hali-justify wageni kuingia na kutoka watakavyo! Huwezi kufika kwenye duka la mtu kisha ukaiba kwavile tu mwenyewe hajafunga! Ukikamatwa, utahukumiwa kwa wizi na wala hakuna atakayejali kwa utetezi kwamba ulikuta duka halijafungwa!!
Ni kweli pia kwamba mataifa uliyotaja ni ya watu wa mchanganyiko lakini kote huko kuna utaratibu wa mtu kuingia na sio tu kuingia utakavyo! Ukifanya hivyo na ukagundulika utawajibishwa! Na kama serikali imelala, raia wema wa nchi husika watapandisha sauti kulalamikia wahamiaji haramu! Labda tatizo la Mtikila ni aina ya lugha aliyotumia lakini kwa anayemfahamu hawezi kumshangaa!! Binafsi ningeshangaa endapo angetumia lugha ya kiungwana, lakini mtu ambae alipata kuita Mwili wa Baba wa Taifa kwamba ni mzoga sijui kama ni ajabu kuwaita Watusi ni nyoka! Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita Mtikila huyu huyu alipata kum-refer Mkapa kwamba ni Mmakonde wa Musumbiji ambae anatakiwa kutiwa kwenye lori na wamakonde wenzake kisha wakamwage mpakani! Lakini tukichuja maneno yake mabovu na ya kibaguzi, bado hoja yake inabaki kuwa ya msingi na katu uozo wa mipakani usiwe justification!
Mwisho ningependa kuzungumzia hilo la eti Kagame alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Tanzania! Hebu jisikie aibu kwa hoja kama hiyo kwani hata kama ni kweli Kagame alishiriki kwenye vita vya Kagera, katu hakufanya hivyo kwa maslahi ya Tanzania bali alifanya hivyo kwa maslahi ya Museveni....ilikuwa ni lazima Museveni apate nchi ili nae (Kagame)apate nafasi ya kuendeleza harakati zake!