Ukweli kuhusu Rwanda na Kagame kwa ujumla (tofauti na wengi wajuavyo)

Wewe ni muongo kama shetani! Mimi nilifanya kazi Ngara katika makambi mbalimbali ya wakimbizi wa Rwanda na kulikuwa na kambi maalum ambazo zimetengwa kwa ajili ya watusi na wahutu waliooana!

Kuanzia leo nitakuogopa kama ukoma!
Mwongo ni nani kati yako na yeye. Uliona wakimbizi ukafikiri ndio hali ya Rwanda!! you are insane if you are serious!!
 
Kaka acha kuposha watu, usidhani wewe ndo umefika rwanda tu!mambo mengi uliyoyaandika sio kweli!

Kaka unapokanusha taarifa yoyote ambayo unadhani si ya kweli, unatakiwa wewe usibishe kwa kutoa taarifa ambazo unadhani ni za kweli!. UKWELI UNAOJUA WEWE NI UPI?
 
Mkuu Madesa,

Nimejaribu kufuatilia thread yako kuhusu Rwanda nimeona umejaribu kukielezea kile ulichokiona Nchini Rwanda lakini ni vizuri nikuweke wazi ktk mambo ambayo nimeona umezidisha mno chumvi....

Kwanza mimi ni Mtanzania ambaye nimeishi Rwanda kwa zaidi ya Miaka 15...(Remera Jirani na Meg Gen Rwahama).na pia huwa naenda sana Rwanda kwa sababu kuna vitega uchumi vyangu..

1. Mradi ule wa Laptop haukufeli sababu ya Rushwa...Nadhani kwa sababu umekaa Rwanda utakuwa umepata picha kamili kwamba Rwanda nayo ikiwa kama mojawapo ya nchi za kiafrika ina Idadi kubwa ya maskini (Wahutu ni wengi na ndio maskini) kuliko watu wa Tabaka la kati na la juu..Hivyo ilifika kipindi uhalisia ukajitenga na njozi.

Nakusisitizia kwenye suala la Rushwa Rwanda iko makini na usiifananishe na hiki ki-nchi chetu ambacho kimefikia hatua kwamba ukiwa kiongozi ambaye si mla rushwa wala mtoa rushwa unaonekana kitu cha ajabu...

2.Kuhusu kutokujua ilipo wizara ya elimu hilo linaweza kutokea popote pale na ktk nchi yoyote ile...Mfano hapa Tanzania watu wengi hawaifahamu ilipo wizara ya elimu...Lakini Taasisi kama Baraza la Mitihani la Taifa na Chuo kikuu cha Dar es salaam hususani kampasi ya mlimani vinafahamika sana...Ina maana kwa mtu ambaye yupo Rwanda na hajui wizara flani ilipo anaweza akakuelekeza uende MINISTERI..sehemu ambayo kuna wizara karibu zote za nchi hiyo.

3.Kuhusu kutapakaa kwa wanajeshi jijini Kigali..sidhani kama ni Issue...Kwani Rwanda wamejifunza kutokana na makosa ikifika saa 12 jioni kuna Doria zilizo serious...Tofauti na hapa kwetu ambapo unakuta Majambazi wanakusanya fedha mchana kweupe na kituo cha polisi kipo umbali ambao hauzidi hata mita 500...Na ni nadra sana kukuta walevi wanaendesha magari Rwanda kwani ndugu yangu lazima utapimwa Alcohol uliyonayo..

Hawa jamaa wametuzidi...wao wapo serious kwenye mambo yaliyo serious....full stop.
 
Acha kuchanganya mada hapa! Kinachojadiliwa hapa ni maendeleo ya Rwanda katika sekta mbalimbali na si Kagame alimuua Habyarimana au wahutu kuuwa watusi. Jadili elimu, kilimo, viwanda nk

Bora umeliona ilo mkuu,alafu anakimbilia kuwaita wenzake zero brain,sasa sijui yeye atakua nani!mada inazungumzia maendeleo ya rwanda kwa sasa yeye amerukia mambo ya ictr,kweli kilaza hauwezi jijua kua ni kilaza
 
Kuna swali 1 ambalo Kagame hapendi kuulizwa. Nalo ni; Ulikuwa wapi wakati vita/mauaji ya kimbali yanaanza? Ni kwamba -alikuwa msituni akiipinga serikali ya Juvenali Habyalimana.
-mauaji yalianza baada ya ndege aliyokuwemo Habyalimana kuangushwa na waasi akina Kagame
-hivyo yeye Kagame ndiye aliyeanzisha mauaji ya kimbali ingawa anajitahidi kuizuia historia isisomeke hivyo.
Huo ndio ulikuwa ugomvi wake na Ufaransa, mkoloni wa zamani wa Rwanda.
 
Jamani kuchangia hapa siyo kwamba ninataka kuwasifia CCmagamba wa hapa!
Ahsante mkuu kwa ulivyodadavua.
Bado yapo mengi nyuma ya pazia! Je unajua jamaa hawana Ardhi na wamejaa!! Je unajua hata vyakula vyote vinatoka nje!!
Je unajua Kagame anafukuza maskini mijini kwenda "reserve" ili kuonyesha majengo yanayojengwa na makampuni ya kigeni?! Nilikuwepo walikuwa wanafukuzwa pasi kufidiwa! Je unajua Kagame anafadhili uharamia wa madini ya DRC?!
Je unajua wahutu ni bado tabaka la chini kwa serikali ya Kagame. Ninakwambia hata NGOs zinazoongozwa na wazungu wanalazimishwa kuteua watutsi kuziongoza mifano ipo kibao.

Je unajua kuwa mwaka jana Kagame aliwaita watutsi wote wanaosoma vyuo vikuu vya ndani na Nje ya Nchi kuwanong'oneza kuhusu kutawala daima na kuwapa mafunzo ya kijeshi?!!
Kagame na serikali yake wanatawala NGOs zote Rwanda kila NGOs lazima iwe registered kila mwaka! na kueleza wanafanya nini! Anawalazimisha NGOs watoe "handouts" misaada midogo midogo kwa wananchi nchi ili kuwapumbaza. NGO moja imelazimishwa kununua ng'ombe wa maziwa kwa wananchi.
Dictator Kagame amegundua namna ya kuishi na wazungu ili kujenga umaarufu.

lete source zilizobeba ushahidi wa hizo tuhuma ulizotoa mkuu
 
Wewe ni muongo kama shetani! Mimi nilifanya kazi Ngara katika makambi mbalimbali ya wakimbizi wa Rwanda na kulikuwa na kambi maalum ambazo zimetengwa kwa ajili ya watusi na wahutu waliooana!

Kuanzia leo nitakuogopa kama ukoma!

Kwanini walitengewa kambi maalumu? Mimi nimeishi Kigali kwa mwezi mmoja. Hali yao ni mbaya kuliko inavyoongelewa na vyombo vya propaganda. Wanachotuzidi ni usafi tu. Kwa kweli mji wa Kigali ni msafi sana
 
Mkuu Madesa sasa sijui tu rely kwa nani kati yako au kwa hao wasomi wa kimataifa ambao link yao imewekwa na mkuu Wambadambwa!ebu ipitie hiyo link alafu uje na mapungufu au kasoro juu ya wachambuzi hao,nilikua Kigali june 2011 japo nilikaa 9 days tu ila kikweli nilivutiwa sana na maendeleo ya mji ule!sasa sijui yaliyojificha nyuma ya pazia,ila maendeleo na ustaarabu wa kigali upo wazi kwa yeyote anaefika pale,wale haujifichi
 
Madesa wewe ni researchers wa ukweli au magumashi.

Ni kama una lako jambo vile, maana usingekuwa nalo story ingebalance, now its a one sided story from a 'researcher' ....

Ntakubishia si kwa sababu nimefika Rwanda bali taarifa yako haikidhi mizania ya mtafiti, ingawa pia mie sio mtafiti.

Kwa mfano:

1. Watu kujua wizara ya elimu iko wapi researcher Madesa anahusisha na kuelimika kwao???? Zaidi ya nusu ya watu mliowauliza walikiwa hawajui wizara iko wapi.
Ilikuwaje watu karibu ya nusu (wanaopajua wizarani) mliowauliza na bado hamkufika wizara ya elimu. Kama sio urongooo!!

2. Reseacher unashangaa enrolment rate ya 97%. Ulipata kujua gross enrolment rate ya Tanzania miaka ya 70?? Ulipata kusikia UPE?? Je sasa enrolement ya Tz ni ngapi ktk MDGs??? Unakimbilia kutupa story za marekani (eti hata marekani haijafikia 97%) ambako sie tunaona kwenye Tv tu.

3. Unasema swala la laptop haliwezekani kwa vile hakuna umeme wakati kuna samsung za kutumia sola hata kampuni ya Tigo wanagawa siku hizi.

4. Ni kweli wanyarwanda hawajui kinachoendelea serikalini?? Je watanzania tunajua kinachoendelea serikalini na kama twajua imetusaidiaje???

Sasa badala ya kuleta matokeo ya utafiti wako unaleta story za mtaani, mara mia wanaotujuza viota vya maraha ndani ya Kigali kuliko taarifa ya msomi ambaye hakuelimika....watafiti kama wewe ndio mmejaa Ikulu yetu ndio maana mambo hayaendi.

Samahani kama nitakukwaza...........
 
Maendeleo Wanafanya vizuri,ila chuki kati yao haitakaa iishe kamwe.Kagame ni mnafiki kama watutsi walivyo.Kagame analipa kisasi kwa Wahutu.Wahutu nao walikuwa washenzi na ten commandiments zao,sasa yamewarudia
 
Wadau ni mara yangu ya kwanza kuchangi madokezo yanayoletwa katika majukwaa tofauti tofauti humu!na ki msingi hili la leo limenipa msukumo!mimi sikubaliani kabisa na mdau aliyeleta hizi details!na ni kosa kubwa sana kutoa maelezo kwa jamii kama huna ushahidi wa kutosha!siwezi sema lolote kiundani kuhusiana na rwanda!lakini ninachoweza kusema Rwanda mimi binafsi nimefika!na ninaijua historia ya nchi ile kwa undani sana!walipo fikia na kazi ambayo serikali ya kagame imeifanya toka kupatikana kwa amani au kuingia madarakani!ni hatua ni hatua ya bayana kabisa ambayo hata kipofi anauwezo wa kutoa ushahidi ya kwamba wamejitahidi!mdau aliyeleta maelezo haya!anakosea kuangalia mapungufu ya wenzake badala ya ku focus on the positive side!tuna vitu vingi vya kuiga kutoka Rwanda!na tunamapungufu mengi zaidi ya Rwanda!kama wao wanadumisha urafiki wao na nchi yetu na hawatangazi ubaya wowote kuhusiana na taifa au jamii ya kitanzania kwa ujumla!sidhani kama kunasababu ya sisi kufanya hivyo!siku nyingine mdau ukiingia nyumbani kwa mtu!utakayoyakuta!yaache pale pale!hekima ndogo sana.Asanteni..napita tu.
 
Wewe ni muongo kama shetani! Mimi nilifanya kazi Ngara katika makambi mbalimbali ya wakimbizi wa Rwanda na kulikuwa na kambi maalum ambazo zimetengwa kwa ajili ya watusi na wahutu waliooana!

Kuanzia leo nitakuogopa kama ukoma!

According to huyo msichana aliyemuuliza ndo kajibu hivyo, sijaona sehemu aliyosema Watutsi na Wahutu hawawezi kuoana.
 
Ukweli wa machache nnayo yajua mimi ni huu,

ELIMU:

Ule mradi wa laptop moja kwa kila mwanafunzi umefeli kwa sababu ya Rushwa na ilikuwa ni ndoto kutimia kwani zaidi ya nusu ya shule zao hazina umeme, walikuwa wana system kama ya kwetu kutoa mikopo lakini kuanzia mwaka jana serikali imejitoa kudhamini wanafunzi wa elimu ya juu hivyo basi wazazi wanatakiwa wawalipie watoto zao sual hilli limeleta mtafaruku mkubwa Rwanda ila kwa kuwa sheria zao haziruhusu maandamano hakuna aliyepinga hadharani,Wanyarwanda wengi hawajui chochote kinachoendelea kwenye serikali yao, ntafafanua,

Mwaka juzi nilikuwa Rwanda tukiwa tunafanya research ni kuhusu elimu chini ya NGO moja iliyokuwa inataka kujenga shule vijijini.
Maajabu ni kwamba zaidi ya nusu ya watu tuliowauliza watuelekeze wizara ya Elimu ilipo walikuwa hawajui ilipo na cha zaidi vijana wa Kigali wengi wao walitupoteza na kutupeleka mahali ambapo sio au wizara tofauti kabisa, mwisho wa siku kwa tabu sana na hapo napo tulipata ajabu la pili, tulikutana na naibu waziri wa elimu mama mmoja mrembo sana na tulichotaka kutoka kwake ni kutaka kujua ni wapi kuna uhaba wa shule ili tukajenge huko, mama yule akasema kwa yeye Rwanda ni moja hawezi akataja eneo kwani akisema kusini watu wa mashariki watakasirika?!! Mwisho wa siku akasema hajui ni maeneo gani twende ila akatushauri twende kwa wa kuu wa viijij au tewnde ubalozi wa Marekani kuna mtu wa USAID anaye husika na elimu huyo ana data zote za Rwanda, tukasema haya, swali la pili kwake likawa je ni asilimia ngapi ya wanafunzi wanaandikishwa shule kwa mwaka akasema 97% na hiyo 3% inayobaki ni ya watoto ambao wanamapungufu akimaanisha vilema, jamani hata nchi za ulaya na Marekani hawajafikia 97% huo ni uongo mtupu na hakujua kuwa zaidi ya mwezi mzima tulikuwa viunga vya Kigali tukiwahoji watoto wa mitaani ambo hawasomi, Jamani Rwanda si kama tusomavyo kuna omba omba wengi kama miji yetu watoto wa mitaani wapo kila kituo cha daladala wakisumbua abiria kuomba pesa.

Turudi ubalozi wa USA, huko tukakutana na huyo jamaa wa elimu, ofisa yule akasema yeye naye kusema ukweli hajawahi kutembelea kijiji chochote kile analetewa data tu hivyo basi tutafute njia nyingine ya kupata data hizo, nikajua labda ni mpango wa kutokutaka kutupa data lakini si kweli wale watu wanashinda ofisini tu hawajui nini kipo mtaani na hata Kagame nae yupo hivyo hivyo.

UHALISIA WA RWANDA:

Ni nchi mojawapo ambayo wananchi wake wanaishi kwa hofu vibaya mno, ukiwa Rwanda huruhusiwi kuongelea vita ya wahutu na watutsi eti serikali imekataza inataka isahau ila makabila haya mawili yana chuki ambayo si rahisi kusahauluka kuna siku nilikuwa kwenye daladala na rafiki yangu mmoja toka Kenya nikawa namuuliza maswali kuhusu Wahutu yule jamaa hakunijibu na abiria wote walinigeukia kutaka kujua nani kataja neno hilo ikanibidi niongee kiswahili ili kuonyesha mimi ni mgeni na nikasameheka kwa hilo,siku nyingine nikamuuliza msichana wa Kitutsi kama ipo siku anaweza akaolewa na Mhutu akasema hilo halitatokea kamwe kwa chuki aliyonayo na nikagundua kuwa hata NGO iliyonipeleka pale members wote ni watutsi!!! na wakasema kama wahutu walishawahi kuongoza NGO hiyo na hakukuwa na Mtutsi, pata picha, kila ikifika saa kumi jioni Kagame anapeleka majeshi mtaani eti kulinda amani mpaka kesho yake, utaona matruck ya jeshi ya kimwaga askari mitaani wakiwa kwenye mstari mmoja na mikononi wana AK47, fingers on the triger, staili hiyo Kigali inaitwa SINGLE FILE SYSTEM hasa na vijana.

Rwanda naweza kusema ni koloni la Marekani na nchi inayopumua kwa misaada ya USA hakuna nchi East & Central Africa yenye international NGOs kama ile, wananchi wengi wameajiliwa huko, kuna kampuni kubwa chache sana na makampuni hayo yanamilikiwa na wamarekani na hata maofisa wake wengi wamesomea huko akiwa yeye mmoja wapo na kwa taarifa yenu ni kuwa raisi na rafiki zake wanamiliki kampuni karibuni zote kubwa za Rwanda kupitia kampuni yao ambayo kazi yake ni kununua kampuni nyingine.hivyo basi ni miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa nchini kwake.

Jamani Rwanda kumetapakaa umasikini mambo yote mnayosoma kutoka Rwandan media yote yamekuwa screened by the government, Rwanda hakuna freedom of media, na sidhani kama kuna private tv/radio zaidi ya mbili,kama moja ipo, ile nchi inaendeshwa na misaada zaidi ya 80%,kodi zao ziko juu zaidi ya kwetu, kuna stori nilipewa kuwa wahisani walikuja kukagua mradi wa barabara na serikali haikutekeleza hilo walichokifanya ni kufumua lami nzuri na kuweka nyingine ili kuonyesha pesa ilipoenda, mpaka mwaka juzi walimu walikuwa wanalipwa wastani wa 42$ kwa mwezi,mpo hapo?

Mpaka leo hakuna anayemjua mrithi wa Kagame ila kuna tetesi anaweza akawa mtoto wake ambaye yupo USA in one of the best millitary academy ambako amesomea baba yake, kama umeshawahi kusikia kule kuna upinzani wa kweli basi tujadili, ana kashfa ya kuwapoteza wapinzani wake na juzi juzi Uganda ililalamika kuwa anatuma majasusi wake nchini humo.

Kwakuwa muda umenitupa kwa leo naishia hapa, ila ukipatamuda vuka mpaka hata kwa wiki 1 tu ukajionee nilichosema ila jiandae kwa matumizi kwani chakula ni gharama nadhani mara tatu ya hapa na hapa sizungumzii kwenye hotel kubwa, asante.

Ningekuamini ulichokiandika hapa kama ningekuwa siifahamu Rwanda na pia ningekuwa sina uwezo wa ku-reason rationally na kuchanganya ninachoambiwa na akili zangu. Kwa kuwa vyote hivyo havipo hivyo nitakupa data chache kuonyesha kuwa wewe ama umehadithiwa au umeamua kutupotosha kwa makusudi. Nina-refer kwenye reds mostly.


  • Unashangaa kuona askari wanaolinda Rwanda kuwa na bunduki? Ni wapi ulipoona askari analinda mikono mitupu? Mbona polisi wa hapa wanaranda randa na bunduki wakiua raia wasio na hatia huku majambazi yakitamba mtaani? Unaweza kutuambia hali ya usalama ya sasa Rwanda (nchi iliyokuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya karibuni tu?
  • Hebu tupe data sahihi kwa mtazamo wako za watoto wanaoandikishwa shule Rwanda halfu tulinganishe na hizo unazozikataa wewe. Kwa taarifa yako enrollment ya primary education in Schengen States ni 100% na elimu hiyo ni ya bure.
  • Kutoza kodi kubwa si tija, HOJA NI KUWA KODI KUBWA INAYOTOZWA INATUMIKAJE! Norway kodi ni 50% kwa watu wa kipato cha chini na kati na ni almost 70% kwa high income earners (muulize yule mchezaji wa Simba aliekimbia huko akuambie) lakini Norway ni ya tatu duniani (kama si ya pili) kwa social welfare.
  • Ni uzushi kusema mradi wa kuwapa wanafunzi wa shule za msingi laptop kuwa umeshindwa. Rwanda haijasambaza umeme nchi nzima lakini umesahau kuwa mradi wa laptop haukuwa based on the availability of electricity rather it wa based on SOLAR-POWERD laptops. Soma hapa (na ni the Guardian la Uingereza lililoandika sio gazeti linalomilikiwa na serikali ya Kagame. http://www.guardian.co.uk/technology/2010/mar/28/rwanda-laptop-revolution.
  • Ni uongo na uzushi mkubwa kudai eti habari zoote Rwanda zinakuwa screened kabla ya kutangazwa. Proof: The East African Standard (linachapishwa Kenya) na linauzwa freely Rwanda, au unataka kutuambia Kagame analimiliki?
  • Mwalimu anaenza kazi Rwanda analipwa RWF 29,000 plus grants (kumbuka USD 1 ni sawa na RWF 595), na wanapata 10% increase every year. Soma hapa: Rwanda's teacher's salary to increase - In2EastAfrica - East African news, Headlines, Business, Tourism, Sports, Health, Entertainment, Education.
  • Nakubaliana na wewe kuwa demokrasia Rwanda haijakomaa, lakini hebu niambie ni nchi gani yenye demokrasia ambayo mrithi wa kiongozi hujulikana kabla ya hata uchaguzi wenyewe kufika? Tetesi (kama ulivyokiri mwenyewe) unaziita UKWELI? Give us a break!

And what was your point? Ku-justfy uozo wa kina Kikwete? Kajipange upya kabla hujatueletea vitu vinavyoonekana kuwa ni uzushi hata kwa mtoto wa darasa la tano anaejishughulisha kusoma magazeti na kuangalia TV/kusikiliza radio. Au unadhani kila mtu humu husoma magazeti ya udaku?
 
Mtoa mada umesema bei ya vyakula ipo juu zaidi yetu, nakumbuka wakati Tanzania ikiwa na mfumuko wa bei 16.9%, Rwanda ilikuwa 6%. Kiwango ambacho ni kidogo kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Je vyombo vyetu vya habari vinao uwezo wa kusema ukweli wa Uganda, Tanzania... kisha kuogopa Rwanda?
Kuna mtu amesema jaji Mwaikasu hatunaye kwa kuwa alisema ukweli kuhusu serikali huko ICTR, je ni jaji Mwaikasu yupi? Kwani Ruaha University College kuna jaji Mwaikasu (ambaye ni maarufu kwa kuongea hali halisi) anayefundisha sheria.
 
Kuna swali 1 ambalo Kagame hapendi kuulizwa. Nalo ni; Ulikuwa wapi wakati vita/mauaji ya kimbali yanaanza? Ni kwamba -alikuwa msituni akiipinga serikali ya Juvenali Habyalimana.
-mauaji yalianza baada ya ndege aliyokuwemo Habyalimana kuangushwa na waasi akina Kagame
-hivyo yeye Kagame ndiye aliyeanzisha mauaji ya kimbali ingawa anajitahidi kuizuia historia isisomeke hivyo.
Huo ndio ulikuwa ugomvi wake na Ufaransa, mkoloni wa zamani wa Rwanda.

Mkubwa, umekuwa usingizini kwa miezi mitatu iliyopita? Mahakama ya Ufaransa majuzi tu imetoa hukumu inayom-exonorate Kagame kutokana na tuhuma za mauaji ya Habyarimana. Soma habari, Kagame keshahojiwa juu ya suala hilo mara nyingi tu na BBC, CNN n.k.
 
Mtoa mada umesema bei ya vyakula ipo juu zaidi yetu, nakumbuka wakati Tanzania ikiwa na mfumuko wa bei 16.9%, Rwanda ilikuwa 6%. Kiwango ambacho ni kidogo kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Je vyombo vyetu vya habari vinao uwezo wa kusema ukweli wa Uganda, Tanzania... kisha kuogopa Rwanda?
Kuna mtu amesema jaji Mwaikasu hatunaye kwa kuwa alisema ukweli kuhusu serikali huko ICTR, je ni jaji Mwaikasu yupi? Kwani Ruaha University College kuna jaji Mwaikasu (ambaye ni maarufu kwa kuongea hali halisi) anayefundisha sheria.

sio Mwaikasu....ni Mwaikusa.
 
Mwongo ni nani kati yako na yeye. Uliona wakimbizi ukafikiri ndio hali ya Rwanda!! you are insane if you are serious!!

Ninawafahamu Wahutu waliooa/kuolewa na watusi and vice-versa, na wanaishi huko huko Rwanda. Na usichokijua ni kuwa Utusi na Uhutu essentially ni more of economic status than tribal division. Umeshasikia lugha inayoitwa Kihutu au Kitusi?
 
umenifurahisha sana mdau!wasomi wanatakiwa kwenda hivi kama wewe!maelezo yenye ushahidi na vielelezo!asipoekewa na hapa!atakuwa na lake!nadhani skunyingine hata tujaribu uelewa wetu!
 
Back
Top Bottom