Ukweli wa machache nnayo yajua mimi ni huu,
ELIMU:
Ule mradi wa laptop moja kwa kila mwanafunzi umefeli kwa sababu ya Rushwa na ilikuwa ni ndoto kutimia kwani zaidi ya nusu ya shule zao hazina umeme, walikuwa wana system kama ya kwetu kutoa mikopo lakini kuanzia mwaka jana serikali imejitoa kudhamini wanafunzi wa elimu ya juu hivyo basi wazazi wanatakiwa wawalipie watoto zao sual hilli limeleta mtafaruku mkubwa Rwanda ila kwa kuwa sheria zao haziruhusu maandamano hakuna aliyepinga hadharani,Wanyarwanda wengi hawajui chochote kinachoendelea kwenye serikali yao, ntafafanua,
Mwaka juzi nilikuwa Rwanda tukiwa tunafanya research ni kuhusu elimu chini ya NGO moja iliyokuwa inataka kujenga shule vijijini.
Maajabu ni kwamba zaidi ya nusu ya watu tuliowauliza watuelekeze wizara ya Elimu ilipo walikuwa hawajui ilipo na cha zaidi vijana wa Kigali wengi wao walitupoteza na kutupeleka mahali ambapo sio au wizara tofauti kabisa, mwisho wa siku kwa tabu sana na hapo napo tulipata ajabu la pili, tulikutana na naibu waziri wa elimu mama mmoja mrembo sana na tulichotaka kutoka kwake ni kutaka kujua ni wapi kuna uhaba wa shule ili tukajenge huko, mama yule akasema kwa yeye Rwanda ni moja hawezi akataja eneo kwani akisema kusini watu wa mashariki watakasirika?!! Mwisho wa siku akasema hajui ni maeneo gani twende ila akatushauri twende kwa wa kuu wa viijij au tewnde ubalozi wa Marekani kuna mtu wa USAID anaye husika na elimu huyo ana data zote za Rwanda, tukasema haya, swali la pili kwake likawa je ni asilimia ngapi ya wanafunzi wanaandikishwa shule kwa mwaka akasema 97% na hiyo 3% inayobaki ni ya watoto ambao wanamapungufu akimaanisha vilema, jamani hata nchi za ulaya na Marekani hawajafikia 97% huo ni uongo mtupu na hakujua kuwa zaidi ya mwezi mzima tulikuwa viunga vya Kigali tukiwahoji watoto wa mitaani ambo hawasomi, Jamani Rwanda si kama tusomavyo kuna omba omba wengi kama miji yetu watoto wa mitaani wapo kila kituo cha daladala wakisumbua abiria kuomba pesa.
Turudi ubalozi wa USA, huko tukakutana na huyo jamaa wa elimu, ofisa yule akasema yeye naye kusema ukweli hajawahi kutembelea kijiji chochote kile analetewa data tu hivyo basi tutafute njia nyingine ya kupata data hizo, nikajua labda ni mpango wa kutokutaka kutupa data lakini si kweli wale watu wanashinda ofisini tu hawajui nini kipo mtaani na hata Kagame nae yupo hivyo hivyo.
UHALISIA WA RWANDA:
Ni nchi mojawapo ambayo wananchi wake wanaishi kwa hofu vibaya mno, ukiwa Rwanda huruhusiwi kuongelea vita ya wahutu na watutsi eti serikali imekataza inataka isahau ila makabila haya mawili yana chuki ambayo si rahisi kusahauluka kuna siku nilikuwa kwenye daladala na rafiki yangu mmoja toka Kenya nikawa namuuliza maswali kuhusu Wahutu yule jamaa hakunijibu na abiria wote walinigeukia kutaka kujua nani kataja neno hilo ikanibidi niongee kiswahili ili kuonyesha mimi ni mgeni na nikasameheka kwa hilo,siku nyingine nikamuuliza msichana wa Kitutsi kama ipo siku anaweza akaolewa na Mhutu akasema hilo halitatokea kamwe kwa chuki aliyonayo na nikagundua kuwa hata NGO iliyonipeleka pale members wote ni watutsi!!! na wakasema kama wahutu walishawahi kuongoza NGO hiyo na hakukuwa na Mtutsi, pata picha, kila ikifika saa kumi jioni Kagame anapeleka majeshi mtaani eti kulinda amani mpaka kesho yake, utaona matruck ya jeshi ya kimwaga askari mitaani wakiwa kwenye mstari mmoja na mikononi wana AK47, fingers on the triger, staili hiyo Kigali inaitwa SINGLE FILE SYSTEM hasa na vijana.
Rwanda naweza kusema ni koloni la Marekani na nchi inayopumua kwa misaada ya USA hakuna nchi East & Central Africa yenye international NGOs kama ile, wananchi wengi wameajiliwa huko, kuna kampuni kubwa chache sana na makampuni hayo yanamilikiwa na wamarekani na hata maofisa wake wengi wamesomea huko akiwa yeye mmoja wapo na kwa taarifa yenu ni kuwa raisi na rafiki zake wanamiliki kampuni karibuni zote kubwa za Rwanda kupitia kampuni yao ambayo kazi yake ni kununua kampuni nyingine.hivyo basi ni miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa nchini kwake.
Jamani Rwanda kumetapakaa umasikini mambo yote mnayosoma kutoka Rwandan media yote yamekuwa screened by the government, Rwanda hakuna freedom of media, na sidhani kama kuna private tv/radio zaidi ya mbili,kama moja ipo, ile nchi inaendeshwa na misaada zaidi ya 80%,kodi zao ziko juu zaidi ya kwetu, kuna stori nilipewa kuwa wahisani walikuja kukagua mradi wa barabara na serikali haikutekeleza hilo walichokifanya ni kufumua lami nzuri na kuweka nyingine ili kuonyesha pesa ilipoenda, mpaka mwaka juzi walimu walikuwa wanalipwa wastani wa 42$ kwa mwezi,mpo hapo?
Mpaka leo hakuna anayemjua mrithi wa Kagame ila kuna tetesi anaweza akawa mtoto wake ambaye yupo USA in one of the best millitary academy ambako amesomea baba yake, kama umeshawahi kusikia kule kuna upinzani wa kweli basi tujadili, ana kashfa ya kuwapoteza wapinzani wake na juzi juzi Uganda ililalamika kuwa anatuma majasusi wake nchini humo.
Kwakuwa muda umenitupa kwa leo naishia hapa, ila ukipatamuda vuka mpaka hata kwa wiki 1 tu ukajionee nilichosema ila jiandae kwa matumizi kwani chakula ni gharama nadhani mara tatu ya hapa na hapa sizungumzii kwenye hotel kubwa, asante.