Mimi nimesoma wildlife nilipokuwa chuo, lkn tunamsoma Nguva kama mnyama anaeishi katk maji na haswa baharini, na mtu alie eneza uvumi huu alikuwa ni Christopher Columbus aliegundua bara la America ndo alisema akiwa safarini ktk bahari alionana na samaki mtu mara 3, hapo ndo ikaanza dhana nzima ya uwepo wao, lkn hakuna mpaka leo sehemu yeyote duniani walipoweka kumbukumbu ya mwili wake zaidi ya picha na filamu za kufikirika, Nguva sio samaki mtu, ukienda pale makumbusho ya taifa ya hapa kwetu Dar es salaam unamkuta nguva yupo lkn sio samaki mtu, ni mnyama na hata hafanani na binadamu