Ukweli kuhusu mgomo na madai ya madaktari Tanzania

Haki hupiganiwa endapo tu inamanufaa kwa uma na inalenga kupata suluhusho la KUDUM kwa faida ya kizazi chasasa na kijacho bila kuwagawa watanzania.

Wasipogoma madakitari kunafaida gani guendelea kuhudumu

1. Hakuna madawa
2. Hakuna vitendea kazi, (vifaa vya kazi, mikasi, x ray machines, utrasound, vitanda, nk
3. Vifaa vichache na duni vya mawasiliano na uchukuzi(sim, magari, ambulace- eti bajaji zibebe wajawazito, kule bungeni wanasafiri na magari yasioendana na uchumi HAFIFU.
3. Majengo mabovu ya hospitali, maabala nk
5. Mishahara duni isiyokidhi viwango, doctor anafanya operation akijiuliza atapatawapi pesa za kulipia pango na ada za watoto- matokeo watu kufanyiwa operation za vichwa au mikasi kubaki matumboni HAWA NAO SIWANAKUFA? KUNAFAIDA KUFANYA KITU CHENYE MATOKEO HASI? HAPANA BORA KUGOMA

Kwa maana hiyo ni bora wagome tufunge mikanda serikali iboreshe mazingira ya kazi, vifaa, majengo na madawa ilitufaidi sote kodi tulipazo.

Sasa hivi ni kawaida serikali kututoza kodi halafu wanagawana huko juu na sisi tunapata shida kila idala huku chini

-Afya DUNI kwa walalahoi wanasiasa na watoto wao matibabu India, Ujerumani, Sweeden nk
-Elimu DUNI kwa walalahoi wanasiasa na familia zao elimu nje ya inchi watatukolonaizi vipi kama kama hawajatuhujumu?
-Miundombinu DUNI ambapo wanasiasa na familia zao hupita humo kwa magari ya kifahari bila kuhisi maumivu, wala shida
-MISHAHARA YA TRA, MAWAZIRI NA WABUNGE JUU walalahoi mishahara duni, mfumuko wa bei na hudma duni zikituangamiza na familia zetu
-FEDHA ZA JK KUTALII, FUNGU LA KUTOSHA LIPO MPAKA ZINAIBIWA KWANINI SISI MASKINI WALAU WASITUBORESHEE MATIBABU

Haiwezekani inabidi tujikomboe na mikono hatari ya wanasiasa wachumia tumbo, wavivu kufikili, wazito kutoa maamuzi na wasio na VIPAUMBELE, DHARURA WALA MIKAKATI YA MUDA MREFU

YOTE HAYA NI MATOKEO YA KUWA NA RAIS ASIEWEZA KUSIMAMA KWA MIGUU YAKE NA KUAMUA KWA FAIFAIDA YA TAIFA
 
Sasa ni wakati muafaka kuwafunglia kesi za mauaji kila daktari ataepangiwa kazi kama hakuwepo wakati huo na kimetokea kifo kwa daktari huyo kutokuwepo sehemu yake ya kazi na kaenda kwenye mgomo. Hakuna zaidi.Mimi siwaungi hata kidole wacha mkono.
mimi nawaunga mkono na mguu! ukhanisi huu wabunge wachukue pesa kama vile nchi hii ni yao wenzao wenyekufanya jambo la maana wawapangie watakavyo! madokta hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke.
 
Mimi niliye mgonjwa mtarajiwa nawaunga mkono wadaktari!, na sekta nyengine nyanyukeni mdai maslahi yenu! kwani Selikali tuliyonayo ni puuzi na haitendi bila kusukumwa!
 
Sasa ni wakati muafaka kuwafunglia kesi za mauaji kila daktari ataepangiwa kazi kama hakuwepo wakati huo na kimetokea kifo kwa daktari huyo kutokuwepo sehemu yake ya kazi na kaenda kwenye mgomo. Hakuna zaidi.

Mimi siwaungi hata kidole wacha mkono.
wangapi wamefunguliwa kesi kutokana na ubadhilifu ulioibuliwa na cag? je kupangua baraza la mawaziri ndo mwisho wa saga?
 
Sasa ni wakati muafaka kuwafunglia kesi za mauaji kila daktari ataepangiwa kazi kama hakuwepo wakati huo na kimetokea kifo kwa daktari huyo kutokuwepo sehemu yake ya kazi na kaenda kwenye mgomo. Hakuna zaidi.

Mimi siwaungi hata kidole wacha mkono.

Je unaiunga serikali mkono ama upo neutral?
 
Tunawaunga Mkono hatutaki kusikia eti wameenda kunywa juice pale IKULU hagombee haki yao hadi wapate hata kama si pesa basi waraka utolewe
 
wangapi wamefunguliwa kesi kutokana na ubadhilifu ulioibuliwa na cag? je kupangua baraza la mawaziri ndo mwisho wa saga?

Tena ngoja CAG afike na huko, ndio tutajuwa vifo vingapi vimesababishwa na ubadhirifu na uzembe wa madaktari. Wasubiri, siku yao itafika.
 
mimi nawaunga mkono na mguu! ukhanisi huu wabunge wachukue pesa kama vile nchi hii ni yao wenzao wenyekufanya jambo la maana wawapangie watakavyo! madokta hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke.

Na wao nani aliwazuia kuwa wabunge, mbona na wao wanafanya kazi za private na hawaingiliwi? madaktari wengi hospitali za Serikali ukienda wana kudirect uende private hospital wenye maslahi nazo na wanafumbiwa macho, au hilo hulijui?

Sioni tatizo la madaktari kulipwa hata million 10 kwa mwezi kwa basic salary, lakini basi na sisi raia tukubali kulipia hizo gharama ipasavyo au unaonaje?
 
Na wao nani aliwazuia kuwa wabunge, mbona na wao wanafanya kazi za private na hawaingiliwi? madaktari wengi hospitali za Serikali ukienda wana kudirect uende private hospital wenye maslahi nazo na wanafumbiwa macho, au hilo hulijui?

Sioni tatizo la madaktari kulipwa hata million 10 kwa mwezi kwa basic salary, lakini basi na sisi raia tukubali kulipia hizo gharama ipasavyo au unaonaje?

Kweli huyu Zoba as his/her name implies!
 
madai ya madaktari yameanza tangu MKAPA akiwa rais...kwa hiyo serikali inajua kila kitu iache usaniii...iwasikilize tu
 
Hata kama sio jambo la Muungano haujui kuwa kuna Madaktari wa Kizanzibari Muhimbili, Mnazi Mmoja na hata kwingineko?

Sasa hata kama sio Jambo la Muungano ungependa waondoke waende Zanzibar hata kama wanatoa Huduma bora

kwa Wananchi wa Tanganyika? na Unajua Nchi ina Upungufu wa Madaktari...

Natambua hivo na nadhan madai yanayodaiwa ni kwa ajili ya madaktari wote wanaotibu Tanganyika iwe Wacuba au Watanzania na kama wakirise concern kuhusu wale wa Zanzibar itakuwa invalid Coz madaktari wanaotibu Zanzibar watadai huko huko kene serikali ya Umoja wa Kitaifa ila ni iman yangu kama hawa watafanikiwa basi wale wa Zanzibar hawatakuwa na Safari ndefu but wanapaswa kudai na sio kusubiri kitu ambacho sio Utamaduni wa Zanzibar kwa Sababu Wazanzibar wanajisimamia wenyewe.
 
Tena ngoja CAG afike na huko, ndio tutajuwa vifo vingapi vimesababishwa na ubadhirifu na uzembe wa madaktari. Wasubiri, siku yao itafika.
Pale mzumbe,IFM na TIA nasikia wameanzisha somo la death auditing.
 
Wanaoona mishahara haiwatoshi kwanini wasiache kazi na wakaingia kwenye biashara zao binafsi?
 
Hili ni jambo gumu ambalo linahitaji kujadiliwa kwa umakini.

Ni kweli kwamba serkali ilikaa na madaktari kujadili juu ya madai yao, na kutekeleza baadhi, lakini ni vizuri kujiuliza waliyatekeleza hayo madai kwa hiari au kwa kushinikizwa, maana baada ya kuwa na mgomo wa muda mrefu ndiyo walikuja kutekeleza.

Si kweli kwamba madaktari tu ndiyo wanaofanya kazi katika mazingira magumu, walimu, maaskari nk nao wanaishi katika mazingira magumu. Na nadhani hoja iliyopo mbele yetu ni madaktari kudai mazingira bora ya kufanyia kazi na malipo stahili ya kazi zao, wao kudai maslahi bora haimaanishi wao ni bora kuliko wengine, nadhani walimu na watumishi wengine pia wana wajibu wa kudai maslahi na mazingira bora kutoka kwenye serkali yao.

Ni kweli tunaambiwa hali ya uchumi ni mbaya na nchi yetu ni maskini, tujiulize ni kweli utendaji wa serikali yetu unaonyesha hali hiyo ya umaskini, je matumizi ya serikali yetu yanaakisi umaskini wetu. Kama sivyo kweli ni haki akina mama wajawazito walale sakafuni, na wagonjwa walale wawili wawili wakati mawaziri wetu wanatembelea magari ya sh milioni 200 kila mmoja, je ni haki hospitali zetu zikose dawa, vifaa vya kufanyia kazi nk

Madaktari wana jukumu la kuwatibu wagonjwa, na ni knyume na maadili yao kukataa kuwatibu wagonjwa, na kitendo cha kutokuwatibu wagonjwa kinaashiria ukatili. Kweli madaktari wameshindwa kujadiliana na kukubaliana na serikali mezani???? inabidi tueleweshwe ni nini kilijiri katika majadiliano hayo...!!!!

Serikali kwa upande wake ina jukumu la kuandaa mazingira bora ya kufanyia kazi na kuwasaidia hao madaktari na watumishi wengine katika sekta nyingine. Serkali imetangaza juzi kuwa imetenga chanjo ya Hepatitis B kwa watumishi wote wa sekta ya Afya, na hili limetangazwa baada ya mgomo kutangazwa, embu tujiulize ni watumishi wangapi wa sekta ya afya ambao wamepta maambukizi ya hepatitis mapaka leo, na serkali ilikuwa wapi siku zote kuwakinga watumishi hawa. Je madai ya kutokuwa na vifaa vya kutolea huduma yakoje, juzi nilisikia CT scaner za Muhimbili na Bugando hazifanyi kazi karibu mwaka mzima sasa, nimeambiwa mashine za Xray kwenye hospitali hazifanyi kazi mfano Bombo, je haya ni mazingira bora ya kufanyia kazi.

Nadhani tukiangalia pande zote mbili utaona kila upande utaonekana kuwa na makosa kufuatia mizania ya mtoa hoja, wapo watakoona serikali ina makosa na wapo watakaoona madaktari wana makosa. Lakini siku ya mwisho ni lazima tujiulize kweli hali tuliyo nayo hapa nchini inaonyesha utawala bora na uwajibikaji? na je ni kweli rasilimali za nchi hii zinatumika kumsidia mwananchi, na kama kweli tunaambiwa hali ni mbaya ni kweli hiyo hali ni mbaya kwetu sote, au kuna tabaka la watu ambao hawajui hali mbaya tuliyo nayo.

Kimsingi kila upande utabeba lawama na siku ya mwisho sisi kama watanzania tunajifunza nini kutokana na huu mgogoro???????!!!!!!!Nadhani kila mmoja atakuwa na jibu lake................
 
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni:-

1. Hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini,
2. Ongezeko la mishahara,
3. Posho za kufanya kazi katika mazingira magumu,
4. Posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi
5. Posho za kuitwa kazini.



Yaliyotekelezwa kwa mujibu wa PINDA Bungeni ni:-

1. Kuongeza malipo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa madakari ambapo wasaidizi sasa watalipwa Sh50,000 na madaktari Sh100,000.
2. Serikali ilikubali kuwaondoa mawaziri na
3. Watendaji wengine wa wizara hiyo,
4. Imeongeza malipo ya kuitwa kwa dharura
5. Mengine kadhaa.


Pima mwenyewe nani msanii hapo, kwani haya madai ni kwa muda wa miezi 3 sasa.

Mimi nadhani suala la madaktari liangaliwe kwa mapana zaidi. Hawa ni watumishi wa umma sawa na watumishi wengine. Kunaweza kuwa na tofauti kadhaa kufuatana na taaluma na hilo linakubalika.

Mishahara ya watumishi wa umma wote Tanzania ni midogo mno. Serikali inaogopa pindi ikiongeza mishahara ya madaktari na watumishi wengine watafuata huo mfano. Mwisho nchi haitatawalika hii

Suala la msingi ni uwezo wa serikali kulipa hiyo Kinachojificha nyuma ya madai hayo ni ufisadi ukiokubuhu ndani ya serikali. Hata wakisema haina uwezo, je hizo wanazochota zinatoka wapi? Watu wakiamini kuwa serikali ni safi hata ukiwambia uwezo wa kulipa madai yao haupo wataelewa.

Kuna njia moja tu ya kupata mishahara inayokidhi. Lazima kuwa na serikali inayoweza kuaminika kwanza. Hatua ya kwanza basi lazima iwe kuondoa hii serikali iliyoshindwa kazi. Ni wizi mtupu. Balozi Wa Swiss alisema na kuiomba serikali yetu ipeleke maombi katika serikali ya Uswiss ili fedha zilizoibwa na waTanzania zikafichwa huko zirejeshwe. Mpaka leo kimya. Maana ndio hao hao wezi! Sasa tunaabiwa kuna mabilioni huko! Tukumbuke hiyo ni Swiss pekee. je USA, UK na kwingineko? Na hapa kwetu bado.

Leo ukirogwa kuongeza mishahara madaktari, kesho waalimu, keshokutwa wahandisi na itaendelea kama kula nyama ya mtu!

Mimi nadhani tuwaunge mkono madaktari kwa maana hiyo tu. Madai yao ni njia ya kusema hii serikali fisadi itoke!
 
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni:-

1. Hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini,
2. Ongezeko la mishahara,
3. Posho za kufanya kazi katika mazingira magumu,
4. Posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi
5. Posho za kuitwa kazini.



Yaliyotekelezwa kwa mujibu wa PINDA Bungeni ni:-

1. Kuongeza malipo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa madakari ambapo wasaidizi sasa watalipwa Sh50,000 na madaktari Sh100,000.
2. Serikali ilikubali kuwaondoa mawaziri na
3. Watendaji wengine wa wizara hiyo,
4. Imeongeza malipo ya kuitwa kwa dharura
5. Mengine kadhaa.


Pima mwenyewe nani msanii hapo, kwani haya madai ni kwa muda wa miezi 3 sasa.

Hapo kwenye GREEN

Kweli Pinda mwongo sana!!!

Mawaziri wameondolewa si kwa sababu ya kutimiza matakwa ya maDr, bali wameondolewa kwa sababu ya ufisadi wao ulioibuliwa na CAG!!!

Kweli serkali dhaiifu inaongoza kwa ulaghai!!!
 
Hawa Madaktari sio wazalendo yaani bora wagonjwa wafe wao waongezewe maslahi, mbona ni Madaktari wa DSM tu hasa Muhimbili mm naamini wapo kisiasa wakifikiri Serikali inaondolewa kwa mgomo wa Madaktari
Manesi, Ustawi wa Jamii, Tanesco, POLISI JWTZ nao wadai maslahi hayo sisi tutapona
Suluhisho WASIONGEZEWE chochote hadi Mahakama ipembue
 
hivi kwa mawazo yako unadhani kwa kutishia na kutoa lugha chafu ndio madaktari hawatagoma?! hivi umeahajiuliza ni Nchi gani East and Central Africa or Africa for that matter ina working enviroment na poor salary katika taaluma ya Afya...Rwanda juzi hapa(1994) walikuwa wana vita lakini doctor analipwa 1500USD, unadhani madaktari hawa hajui kuwa kuna nchi jirani na mbaki pia wanalipwa vizuri na mazingira mazuri, au ni uzalendo wao wa kubaki hapa nchini(ignore Brain drain) kuhudumia na kubadilisha hali iliyopo? sasa watu wanaanza kuleta siasa eti kama fani zingine wasipogoma na madaktari wasigome"kwani wenyewe ni nani"..kumbuka jumla ya madaktari wa binadamu(GP,Specialist) haifiki hata 15,000! sasa bado umuhimu wao hauonekani bado?! wao wameamua kusimama kwa pamoja despite upotoshwaji wa taarifa n vyombo vya habari, sasa kama kada nyingine wamezoea tabu hizi, ni wao lakini kwa taaluma yao sasa ni kikomo.
 
Back
Top Bottom