Ukweli Kuhusu Kilichotokea Ndago Singida

Kwa hiyo hao vijana wote walimrushia mawe Mnyika lakini hana hata mchubuko. Na mtu akirusha jiwe wewe unachofanya ni kumuuwa.
 
Nilijua lazima iwe Mwigulu............kawafungisha tela polisi na OCD,hivi Mwigulu ulishindwa nini kugombea kwako Tegeta mpaka unakuja kuchonganisha vijana huku kwetu..........wewe wanao kina Joshua umewaandalia maisha mazuri, tuache na sisi kina Mnyika, watuandalie/watupiganie maisha mazuri..............leka kua pa-luula.....
mwigula! huyu mtu mbona anavuma sana kuliko matendo yake mema? yaani anavuma kuliko hata Coffi Annan, je kwa lepi zuri?
 
mema yapo yapo mkuu ila sio kivile, ujue kila shetani na wakati wake......walikuwepo kina Malechela wakituibia kura, kina Makamba wakitukashifia kina Slaa wetu, sasa ni ujio wa shetani mwingine tena ila tutampakata tu, vuta subra
 
Aliye uawa labda sacrifice ili ccm isogeze hata ka mwaka kamoja na nusu mbele
 
Imebidi unasema mnyika alikuwapo kwenye huo mkutano na tumaini makene alisema njia ya mwongo ni fupi mnyika hakuwepo so propaganda wekeni pembeni kidogo mtupe fact
 
Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese. Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.

Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi. Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.

Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda.

Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.

Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo.

Pamoja na yote haya, Mwigulu watu wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili.

Bahati mbaya ndiyo nimejiunga na hii JF rasmi leo na sina uhakika kama nitapata sehemu na mtandao niweze ku-post tena.

karibu mwana kwetu
 
Cha muhimu wananchi wa jimboni kwa Mwigulu wanajua exactly kilichotokea na muhimu hawamtaki tena huyu jamaa na uhuni wake. Lakini kama ilivyosemwa Mwigulu ni mtu mbaya sana kwa ustawi wa Taifa letu, yuko tayari kuchochea fujo na kumwaga damu kwa maslahi yake maovu si mtu wa kum entertain hata kidogo
 
Kwa mtu mwenye uwezo wa kutafakari na kufuatilia mambo kwa kushirirkisha ubongo atagundua kuwa ulichokiandika ni povu tupu...

Mkuu huyo marehemu alikuwa kutumika wasio juwa wajibu wawo ndani ya ccm ni watalam wa kuwatumia wapumbavu ukitumiwa unatupwa kama tishu
Nakuhurumia usije ukawa miongoni mwahao watumikao
 
Karibu JF, hiyo ndo kaz yako kwa leo lete updates za matukio yote hapo na wala huna haja ya kupost pengine, hapa panatosha sana. Naikubar taarifa yako coz Mwigulu ndo fikra zake zilipoishia, hana ujanja mwingine. Nadhan hao baadh ya wanaIramba hawawez kuwachukia viongoz wa Chadema bila sababu za msing. Wali2mwa kaz ngum dhid ya NGUVU YA UMA.
 
No matter nani mchokozi na nani kachokozwa maskini kutumika kisiasa si sahihi, kwa nini watutumie sisi na sio watoto wao! Kweli walioandika BIBLE hawakukosea, .... Mpe maskini kileo asahau shida zake,... Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese. Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.

Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi. Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.

Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda.

Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.

Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo.

Pamoja na yote haya, Mwigulu watu wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili.

Bahati mbaya ndiyo nimejiunga na hii JF rasmi leo na sina uhakika kama nitapata sehemu na mtandao niweze ku-post tena.

Karibu sana mkuu hakuna bahati mbaya kujiunga na Jf tunahitaji updates za mikutano yote ya singida huo utakuwa mchango mkubwa sana katika ukombozi wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom