SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
- Thread starter
- #81
Naomba mdau ukiweke hicho cha MZEE PUNCH bwana maana laaahh CHA MZEEE PANCHI mzee wa fuvu...kweli wewe noma
Mzee NYENJENKURU,
Ningetaka hata sasa kukiweka nitakiweka isipokuwa ninataka kwa kuwa-user tag wote mlioshiriki kwenye thread hii ya G211 na Mutungirehi maana nyinyi sitaki mkose uhondo huo. Hivyo, ndani ya masaa 24 nitakuwa nimeshakitoa.
Kwa kifupi ni kwamba kilitungwa na jamaa ambaye alikuwa anarekodi matukio yote ya ule mgomo wa mwaka 1990 hadi tarehe kilipofungwa Chuo yaani Saturday, May 12, 1990.
Mimi likipata mwaka 2003 alipokitoa lakini inaelekea kulifanyika njama ili kisijulikane mtaani. Kikapotea kama kilivyopotea kile cha Nyerere yaani (Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania).
Nilipokipata hiki cha PUNCH na kile cha NYERERE nikaamua kuvi-scan vyote viwili na hadi leo vipo kwenye online database yangu, hata wakikamata computer zangu hawanipati labda waende kwenye servers za Yahoo au Google.
Sikuwahi kufikiri kuvitawanya mitandaoni kama hivi kwa sababu wakati ule 2003 internet haikuwa shida kwangu lakini online forum kama hizi kwa watanzania zilikuwa hazijazoeleka sana na hata Jamii Forum naamini ilikuwa haijazaliwa.
Forum zilipoenea siku moja nadhani miaka mitatu iliyopita nikaona humu JF wanauliza sana kuhusu kitabu cha NYERERE na ikaelekea watu wameshakata tamaa ya kukipata. Nilichofanya nikaamua kukisambaza humuhumu JF hadi kikakaa kwenye sticky kwa muda kama wa miezi mitatu na ushee.
Sasa kwa sababu mmetaka hiki cha PUNCH basi sina masaa zaidi ya 24 nitawashushia, lakini kwa masharti kwamba kinakuwa kwenye separate thread ili tuendelee kuchambuana huku kwa hili la G211 na Mutungirehi na kule kuwa na thread nyingine ya PUNCH.
Naamini watakuja members wengi maana kama walivyojitokeza kwenye hii na wengine hata kujiunga rasmi JF.
Keep in touch. Long live JF
Kusuhu cha g211 niwazo zuri tukagawana page kama ulivyosema ni wazo zuri sana. Anyway endelea kutupa uhondo wa enzi hizo
Ngoja kwanza tuendelee kupashana humuhumu kwanza, unajua watanzania wengi vitabu hawasomi. Ungeandika kitabu si ajabu ungechelewa sana kupata wasomaji kuhusu hii ya G211 na Mutungirehi ambapo kwa hizi siku mbili utaona kwamba imeshasomwa na watu 1,653 hadi natuma post hii. Ni watu wengi sana hao kusoma jambo moja, ukipata usomaji wa aina hii basi ni kweli meseji ime-spread.
.Anyway endelea kutupa uhondo wa enzi hizo...za FOE hivi Makoleo yupo jamani yule jamaa wa ME
Mkuu,
Nimemaliza Civil Engneering mwaka 1997 na hivyo Makoleo tuliachana naye first year kwenye Engineering Mechanics, hakuendelea kutufundisha. Atakuwa aliendelea kufundisha wenzake wa Mechanical Engineering.
asikia yule SUZY alikuwa anafundisha electronics workshop course kwa fist year ana Phd kwa sasa?
Aisee yule dada alikuwa mtulivu na smart. Walioendelea na Electrical Engineering watakuwa wanamjua zaidi. Si unajua tuliingia pale karibu wengi wetu ni ma-bachelor, aisee alikuwa anavutia wengi. Lakini hata tukiwa palepale alikuwa ameshaolewa na lecturere mmoja kule Electrical na hivyo wakawa naye Deprtment moja.
Prof. Mbwete nasikia ndiye Mkuu wa Open University hayuko tena pale. Prof. Materu wa kule Electrical tulimkuta akiwa Dean of Faculty alishaondoka zaidi ya miaka sita iliyopita, yuko either America au Europe kwenye international organisation. Hakutaka kusumbuana na serikali kugomagoma kama wanavyosumbuliwa madaktari ikibidi na wasomi wote.
Wapo list ya wengi tu ninaowakumbuka na walishaondoka pale. Mfano Dr. Nsekela aliondoka mwaka 2000 akawa mbunge wa jimbo moja huko Tabora. Kisha baadaye akawa Mkuu wa Mkoa Mwanza, akahamishiwa Dodoma na hivi majuzi akachaguliwa kuwa Balozi nchini Italy.
Dr. Yonnah nasikia yuko inayohusika na Mawasiliano na ni mtu mkubwa huko. Ila sina uhakika na hilo.