SubiriJibu ijapokuwa unataka kuweka historia sawa, unatumia nafasi hiyo kujitakasa kwa dhambi ya U-TRAITOR. Dhambi ile ni kubwa na itaendelea kukutafuna sana, kama usipokiri na kurudi kundini kama wenzio. Nimesoma kwa masikitiko maelezo yako mareeefu yenye ujanja ujanja mwingi. Nimelazimika kujiunga na JF leo kwa ajili yako, ili niweke kumbukumbu sawa. Mimi ni G211 mpaka kifo.
- SIO KWELI hata kidogo kuwa G211 ndio tuliompiga maleva pale Nkurumah, kama unakumbukumbu nzuri siku hiyo tulivaa zile Tshirt zetu usizozipenda, tukakaa kule nyuma darini, muda wote tulikuwa pamoja na ki ukweli tulishangilia sana. Mutungirehi aliangushwa na ma ngwini wenzie na FoE 3rd yr uliowataja.(ndio u traitor wenyewe huu)
- Nikirudi siku ya tukio SIO KWELI kuwa viongozi wetu walikuwa na kikao na Prof Masenge, Mbona wao hawakufanya mtihani ??? na mpaka leo ni G211?? na wala hawakutushauri tufanye mtihani. Mimi nilikuwepo darasani nikijiandaa na mtihani wa Chemistry, Masenge alilazimisha watu kwa kutugawia mitihani sisi wengine tukakataa. U-taitor tu ndio uliowasumbua.
- Ukweli ambao hutaki kuusema ni kuwa mtihani ulishelewa toka saa 2.00 mpaka 5.40 kwa sababu walimu wa Math dpt walikuwa wamegoma kutoa mtihani kwa sababu ya vurugu tulizofanya na wewe wakati wa ile test ngumuuu. Hivyo Dean wa Engineering aliwabembeleza sana ndio maana wakachelewa.
- ukweli mwingine ni kuwa wote tulikuwa na mtihani wa Chemistry siku ile saa 8.00 hivyo ilipofika saa 5 tulikubaliana kutawanyika na kujiandaa na mtihani wa mchana kwa kuwa ktk hali ya kawaida tusingeweza kuanza mtihani saa sita na tufanye na mwingine saa nane kwani mitihani ilikuwa ni ya masaa matatu.
- Hii habari ya Yustus si ya kweli, alikuwa mtu wangu wa karibu.
- Usichokijua ni kwamba baadhi yetu G211 tulipanga mpango mahsusi wa kimapinduzi wa kuongoza chuo mpaka tumalize, ni mpango huu ndio uliomuweka Sweke madarakani na mwaka uliofuata akafuatia mwenzetu mwingine (room mate wa Sweke) aliyekuja kuwa Vice President ambaye kimsingi ndiye aliyeongoza kwani kama unavyojua President wake alikuwa mtu kilaji sanaa.
- Prof Masenge alikasirika sana na hamasa yetu, hasa kitendo cha kuingia darasani na Tshirt(I LOVE G211-1994) alitunga UE ngumu ajabu na akakamata 70 kati ya 211 kwa ajili ya sup. (Nyie Ma traitor alikamatwa mmoja tu kati ya 70)
- Kwa ushirikiano wetu tulikataa kwenda field ili tusome na wenzetu waliokamatwa na matokeo wote 70 walifaulu akanyakwa TRAITOR na ku DISCO.
- Prof Masenge alipopata nafasi na kwa ushahidi wa uongo wa ma TRAITOR kama wewe akiwa VC ADMIN alitukandamiza na kutuchelewesha kumaliza shule kwani kwenye displinary hearing G211 hawakutukuta na makosa.
- Niseme tu ijapokuwa alikuwa mahiri kwa mahesabu, Prof Masenge hakuwa mtawala mzuri, laiti angekuwepo Prof Mkude mambo yangekuwa tofauti.
- Pamoja na kuwa tulichelewa kumaliza chuo, tukio lile wengi wetu lilitujengea ujasiri unaotusaidia mpaka leo, TAABU ile ilitufundisha mno kuhusu maisha na tuliporejea tulisoma kama watu wazima tukijua dunia ya nje ikoje, MSHIKAMANO ule ulituacha tukiwa watu wenye kuamini katika utafutaji wa haki kwa umoja, tukijua kwa hakika uchungu wa kusalitiwa katika mapambano.
- ALUTA continua mapambano yanaendelea.