Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

Subirijibu acha ku expose Uoga wako. Hivi hata mkeo akisoma hapa si atakudharau sana. FOE SPIRIT Forever

Nimekuwa mwoga kwa miaka mingi ku-expose ukweli wa hii issue kwa sababu najua mna washabiki wengi. Sasa nimeondoa woga huo.
 
Hivi hii thread imelenga kutukumbusha hili jambo kwa faida ipi? Au ni kama story za vijiwe vya kahawa tu!!? Naon unaandikwa utitiri wa maneno weeeeee halafu sioni la maana hata moja.
 
Hivi hii thread imelenga kutukumbusha hili jambo kwa faida ipi? Au ni kama story za vijiwe vya kahawa tu!!? Naon unaandikwa utitiri wa maneno weeeeee halafu sioni la maana hata moja.

Ukiwauliza waliotoa LIKE na wasiokuwa wavivu wa kusoma hadi waka-applaud kwa topic hii watakujibu hivi:
*****

01
: Kama ni Radio hulazimiki kusikiliza stations zote!!!!
02: Kama ni Kitabu hulazimiki kusoma pages zote!!!!
03: Kama ni Gazeti hulazimiki kusoma pages zote!!!!
04: Kama ni TV hulazimiki kuona stations zote!!!!
05: Kama ni Emails hulazimiki kufungua folders zote!!!!
06: Kama ni Internet hulazimiki ku-browse website zote!!!!
*****

Hayo yote sita yanakufanya ujichagulie kujikita kwenye topic zaidi ya 1000 za humu JF na hii ungewaachia watu 786 ambao hadi sasa wamesoma thread hii ambapo ukiondoa mmoja yaani wewe wanabaki 785 hadi dakika naandika post hii!​
 
  • Thanks
Reactions: GP
Japokuwa miaka hiyo nilikuwa bado kindergarten but nimeisoma hii story na kuielewa kiasi chake na ku conclude. SUBIRI JIBU ni traitor japokuwa mtu mzima, kitendo cha kuandika wenzako wafukuzwe chuo ni usaliti na umeonesha ulivyo selfish wa kiwango cha juu na sitoshangaa ukimuuza hata mkeo hali ikiwa tete, yaani kupata kaka au baba traitor hatari sana, wanaume huwa wanasimamia misimamo yao hata iweje...
 
Nimekuwa mwoga kwa miaka mingi ku-expose ukweli wa hii issue kwa sababu najua mna washabiki wengi. Sasa nimeondoa woga huo.

Jamaa walikuwa na sababu za Msingi na ndio maana Walishinda KESI na Inaonekana TRAITORS Mliumia sana kwa sababu USALITI wenu ULITHIBITISHWA NA MAHAKAMA
 
Wewe SubiriJibu utasubiri sana na wala huta pata hilo jibu ndo maana mambo ya aibu yaliyokutokea yanakusumbua kwa miaka 18 sasa, nakusoma kwa harakaharaka utakuwa ni mnafiki sababu hii thread yako unaileta kinafiki huku ukijifanya kuwachambua wabaya wako na viongozi mashughuli wa CDM. Najua mwisho wa hadithi yako ya kinafiki unataka kusema wale waliokuwa viongozi wa migomo ambayo wewe unaiona haikuwa na tija ndo wamekuwa makamanda wa CDM. Wajanja hatuko tayari na unafiki huu, kama mnataka kuchambuana nendeni mkaanzishe FB page muelezane za uso ndo tutakuona kweli wewe shujaa. Tuachie JF yetu na uchambuzi wa mada zenye ujazo acha kuleta mada zako zenye wepesi hapa ni eneo lingine. Go far you Traitor even Shetani anakukataa nakukuona umemzidi usaliti. Mwanaume gani huna lakukumbuka miaka yote unaleta hadithi isiyo ya kizalendo namuhurumia mkeo sana na hili ndo tatizo la idadi ndogo ya wanaume akaolewa na wewe na zaidi tatizo wazazi walipeana mahari ndo akaolewa na wewe mchunguze atakuwa anajuta sana
 
Last edited by a moderator:
Ka story kazur, si wengine tulikuwa kipindi cha mtatiro, mwita mwikabe, na mwita mdogo wa FOE. Viongoz wengi daruso (hasa marais wa daruso) walikuwa wakimaliza chuo wanaenda ccm e.g mwita mwikabe na mwita mdogo.
 
Japokuwa miaka hiyo nilikuwa bado kindergarten but nimeisoma hii story na kuielewa kiasi chake na ku conclude. SUBIRI JIBU ni traitor japokuwa mtu mzima, kitendo cha kuandika wenzako wafukuzwe chuo ni usaliti na umeonesha ulivyo selfish wa kiwango cha juu na sitoshangaa ukimuuza hata mkeo hali ikiwa tete, yaani kupata kaka au baba traitor hatari sana, wanaume huwa wanasimamia misimamo yao hata iweje...

Mkata Kiu,

Unaona sasa mnaojiingiza kichwakichwa bila kujua uhalisi wa hii story. Kama umesoma story yangu ungegundua mambo mawili. Kuna suala la G211 na suala la Benedict Mutungirehi.

Sina haja ya kurudia soma tena na tena na kama hayakunasa kichwani labda wewe ni mtu wa kusoma hata mara nane ndipo uelewe.

Suala la kubatizana jina la TRAITOR au G211 ni lile la April 1994 likakamilika May 1994. Suala la Mutungirehi ni lile la October 1994.

Ukisoma utaona kwamba yote mawili yanahusisha hako ka-kikundi kanakoitwa G211.

Hata suala la G211 halikuwahusu Faculty of Engineering wote. Liliwahusu wale ambao hadi May 1994 walikuwa First Year na ilipofika October 1994 wakawa second year.

Suala la Mutungirehi lunatakiwa ujue kwamba Mutungirehi alikuwa President wa DARUSO, kachaguliwa na Chuo kizima. Hivyo move yoyote for or against him ilitakiwa iwe ya Chuo kizima.

Lakini pale Nkrumah mipango ya kumpiga ilikamilishwa na kikundi kidogo cha wanachuo wakiwemo hawa G211, tena hawa G211 wakiwa hawana wiki zaidi ya tatu wameshinda kesi yaop ya kurudishwa Chuoni baada ya kufukuzwa.

Sasa pima hapa mwenyewe, kwa nini haka ka-kikundi kahusike kote, kule Engineering na kwenye Chuo kizima.

Wewe hapa unaniita traitor kiasi kwamba hata G211 anayekusoma hapa angekujua angekulaumu kwamba unawavurugia propoganda yao ya miaka mingi.

Rudia kusoma uone kwamba hata hao G211 hawakutuita TRAITORS kama unavyotuita. G211 walituita sisi TRAITORS kwa kile kitendo cha kufanya mtihani ile May 1994. Pale wakadhani wametunyoosha.

Lakini haohao G211 hawakuwahi kutuita TRAITORS kwa jambo jingine. Wewe unatuita TRAITORS kwa tukio la Mutungirehi maana yake umekurupuka kwani hata hao G211 hawakutuita TRAITORS kwa hilo tukio bali lile la May 1994 kule kwetu FOE kwa masuala ya Mathematical test and Exams.

Kuandika ilibidi niandike ukweli kwamba siku Mutungirehi anapigwa masumbwi wao walikuwa ni washiriki. Soma hoja zao humu uone kama hili la kumpiga Mutungirehi kama wanalikana. Hakuna hata mmoja anayelikana.

Kwa definition yako ukiondoa finalists, basi TRAITORS tulikuwa ni wanachuo wote ambao hatukuadhibiwa kukaa mwaka mmoja nyumbani tukarudishwa mapema December 1994.

Yale masumbwi na viti alivyopondwa Mutungirehi maana yake uliona alipata adhabu ndogo kwani ulitaka wamuue kabisa!
Asiyetaka hilo unamuita TRAITOR.

Lakini kasoro moja huioni. Katika yote haya hata wenzako ambao ni washiriki rasmi wa G211 na wako humu JF hawasemi kwamba kuna mahala tuliwahi kukaa na kukubaliana jambo halafu kukatokea ma-TRAITOR wa jambo hilo.

Kwa taarifa yako matukio haya hawa G211 walijfunza adabu kwamba ukitaka uungwe mkono kistaarabu basi fanya jambo moja. Ita kikao lete agenda yako tuijadili basi hata kama hatuipendi tutajiunga nayo kwa sababu tumesikiliza maoni ya wote na demokrasia imechukua mkondo wake.

Mbona walipojirekebisha na kuanza kufuata utaratibu huo hakukutokea mzozo wowote. Na sanasana tulikuwa tunaadhibiana ki-demokrasia.

Mfano, kule Engineering (FOE) kuna wakati walitaka tumchague mpinzani wa Maleva apite awe President wa DARUSO.

Kule FOE kulikuwa ni major campaign block, ukiletwa wakaku-approve basi umeukwaa u-President wa DARUSO. Mgombea akaletwa akashangiliwa sana. Aliletwa na jamaa wawili yaani Loti na Chapa.

Kumbe sasa hawa mabwana wakapata upinzani mwingine mlemle FOE. siyo wa sisi second year. Siyo wa sisi waliotuita TRAITORS mwaka uliopita. Bali upinzani mpya wa first year.

Hoja ya First year wakaona kwa nini watayarishiwe uongozi na watu wa third year. First year wakaunda umoja mpya kimyakimya wakamnyima kura yule mgombea na badala yake wakampa kura MALEVA. Hakika hata MALEVA na campaign yake walipata surprise maana hawakutegemea.

Hapa ndipo majina TRAITOR yangeweza kutumika maana ni kukiuka jambo ambalo awali mlikubaliana.

Jambo jingine ni pale ambapo tukiwa fourth year Sweke akawa anaachia ngazi ya u-President of DARUSO. Engineering wakakusanyika wote wakasema this time wasichukue u-President lakini wachukue u-Vice President wa DARUSO.

Wakakusanyika FOE wote wakakubaliana kwamba wamchague third year aitwaye Yustus Primus ambaye ni electrical Engineering. Wakakubaliana wote.

Imepita wiki moja kukatokea uvumi kuwa kuna kampeni ya chinichini kwamba Loti, Chapa, na Sweke hawamtaki tena huyu Yustus. Yustus hakuwa na tabia ya unafiki akaitisha kikao cha students wote FOE.

Tukajadili, bwana wakamgeuka wote. Campaigners wake kama Letinan Pasian wakamgeuka. Mimi hadi leo sijui kwa nini walimgeuka. Ikabidi Yustus Primus ajitoe.

Kumbe ile move imewaudhi FOE wengi. Wakakaa kimya hadi siku ya kupiga kura. Siku ya kupiga kura haohao Engineering wakamtosa yule chagua la Loti, Chapa na Sweke.

Nimeweka matukio haya mawili kuwa ndiyo yalifaa kuitana traitor na si yale ambayo hatukuwahi kukaa kikao cha kukukubaliana ajenda yoyote kama kumpiga Mutungirehi au kuchanachana mitihani.

Hata lile tukio la kiongozi wa G211 yaani Ladislaus Malima kukemewa na Prof. Masenge halafu akanyewa akawageuka wenzake wasigome hilo ndilo lilistahili kumpa jina TRAITOR maana alikiuka makubaliano ya wenzake ya kuongoza mgomo halafu anawaletea hadithi za kuwabembeleza kutogoma!
 
Jamaa walikuwa na sababu za Msingi na ndio maana Walishinda KESI na Inaonekana TRAITORS Mliumia sana kwa sababu USALITI wenu ULITHIBITISHWA NA MAHAKAMA

Hawakwenda kushitaki kwa sababu wengine tulifanya paper. Walienda kushitaki kupinga kitendo cha kufukuzwa chuo.

Kama walikuwa na sababu mbona hawakufungua kesi mara baada ya kitendo cha kuchanachana mitihani na kututoa nje.

Ok, hata kama walikuwa na sababu au haki, toka lini unapokuwa na haki umlazimishe mwenzako ajiunge na kundi lako la haki.

Ingeleta tofauti gani kama wasingetuvuruga wakaamua kwenda kortini. Ni wazi msingi wa kesi ungekuwa tofauti. Kesi ingekuwa ni madai ya kucheleweshwa kwa mtihani. Kwa kutokufanya hivyo matokeao yakafanya kesi yao iwe kupinga kufukuzwa chuoni.

Wangefanya vile, sisi tungenfanya mtihani wetu na wao wakaenda mahakamani. Full stop. Wangekuwa tayari wameweka court-injuction wasifukuzwe chuoni wakati wakiendelea kudai kudai mtihani kama sisi.

Mbinu hii ndiyo wanayotumia watu kama Hamad Rashid (CUF) na David Kafulila (NCCR) na hadi leo wamefanikiwa kuendelea kuwa wabunge maana mahakama imesitisha hatua zaidi za kuwafukuza. Tofauti na kesi ya wale madiwani watano wa Arusha wa CHADEMA utaratibu wa kuwafukuza ulishatimia kama ulivyotimia kwa hawa G211.

Ona hata reaction yao. Ok hata kama tungetoka kwenye mtihani. Je, kweli moyoni tungeungana na madai yao? Hivi u-TRAITOR uko wapi, moyoni au kwenye vitendo? U-Traitor uko moyoni hata kama utaninyooshea bunduki bado nikitaka kukusaliti nitatafuta njia na nitaipata.

Unapowashangilia kwamba G211 kwamba ni mashujaa basi ni kwa wale ambao hawakuujua mlolongo mzima wa matukio. Huwezi kujisifia kuchanchana mitihani ya wenzako halafu ukataka tukukumbuke kama shujaa. Huwezi kumpiga Mutungirehi karibu ya kufa halafu tukuite shujaa halafu anayepiga hilo tumuite TRAITOR.

Ni kweli nimeandika mengi lakini hawa walioanzisha ile thread ya Mutungirehi wamenilazimisha niseme haya yote ambayo ilifika mahala nilishayapuuza kwamba ni mambo ya utotot wa Chuoni.
 
Wewe SubiriJibu utasubiri sana na wala huta pata hilo jibu ndo maana mambo ya aibu yaliyokutokea yanakusumbua kwa miaka 18 sasa, nakusoma kwa harakaharaka utakuwa ni mnafiki sababu hii thread yako unaileta kinafiki huku ukijifanya kuwachambua wabaya wako na viongozi mashughuli wa CDM. Najua mwisho wa hadithi yako ya kinafiki unataka kusema wale waliokuwa viongozi wa migomo ambayo wewe unaiona haikuwa na tija ndo wamekuwa makamanda wa CDM. Wajanja hatuko tayari na unafiki huu, kama mnataka kuchambuana nendeni mkaanzishe FB page muelezane za uso ndo tutakuona kweli wewe shujaa. Tuachie JF yetu na uchambuzi wa mada zenye ujazo acha kuleta mada zako zenye wepesi hapa ni eneo lingine. Go far you Traitor even Shetani anakukataa nakukuona umemzidi usaliti. Mwanaume gani huna lakukumbuka miaka yote unaleta hadithi isiyo ya kizalendo namuhurumia mkeo sana na hili ndo tatizo la idadi ndogo ya wanaume akaolewa na wewe na zaidi tatizo wazazi walipeana mahari ndo akaolewa na wewe mchunguze atakuwa anajuta sana

Suala la kuongoza migomo vyuoni si issue hata kidogo. Yoweri Museveni akiwa UDSM alishiriki kuipindua landrover ya serikali iliyokuwa imekuja ama kutuliza ghasia zilizokuwepo pale.

Cha muhimu ni kwamba tuliweka msingi kwamba huwezi eti kuwa na kikundi kikubwa kinataka lolote dakika yoyote kije kitueleze jambo bila kukubaliana halafu tukifuate. Ndivyo G211 walivyotaka.

Walitaka iwe hivyo kule FOE yaani May 1994. Wakapitiliza wakataka iwe hivyo Chuoni kote yaani October 1994. Yaani walitaka kuleta G211 itawale chuo kizima kama G55 ilivyotikisa nchi nzima hadi Julius Nyerere akashtuka.

Lakini tofauti ni kwamba G55 chini ya Njelu Kasaka, Generali Ulimwengu na wenzao walikuwa wanatumia hoja zenye ushawishi kwenye vikao.

Hawa G211 hawakutaka habari ya vikao. Walikuwa wanatumia masumbwi kama yale waliyomtwanga Mutungirehi na mikono kama walivyoitumia kuchanachana mitihani yetu. Wapi na wapi??????????!!!!!!!!!

Sishangai wanapojitetea humu maana niliona live matukio yote. Bali ninashangaa ambao hawakuwepo na wanashangilia kikundi ambacho kama kisingedhibitiwa basi hakka kungetokea mauaji kama ya yule msichana Mukasa aliyejiua wakati wa kunji (mgomo) wa mwaka 1990.

Binafsi huwa najiuliza hivi nini kilimfanya Mutungirehi asife pale, maana imagine viti vya Nkrumah Halla vinarushwa alipolala kama vile mtu anatupa takataka jalalani.

Binafsi niliona wasichana wengi wakilia siku ile wakidhani amekufa. Hata yeye Mutungirehi aliwahi kujieleza gazetini kwamba alidhani atakufa na ikabidi arusherushe miguu na waliomshambulia wakadhani anakata roho wakakimbia na ikawa ponapona yake!

Sasa, kama una akili timamu, utawezaje kushangilia au ku-support wahuni wa aina hii.
 
Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.

{https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rehi;-mwanasiasa-mahiri-kazimikia-wapi-3.html}

Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.

Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.

Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.

Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.

Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.

Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.

Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.

Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.

Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.

Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.

Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.

April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.

Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.

Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.

Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.

Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.

Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.

Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.

Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!

Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.

Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.

Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje”

Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.

Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.

Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.

Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.

Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.

Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.

Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.

Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.

Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.

Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.

Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.

Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.

Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.

Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri

Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.

Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.

Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.

Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.

Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.

Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.

Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.

Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).

Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.

Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.

Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.

Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.

Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.

Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.

Hakika wewe ni mwandishi mzuri mkuu..ni nadra sana kwa mhandisi,nina imani hujakalia tu hii talent..vinginevyo sisi tumepita hapo miaka ya 2000 na kwa kweli matukio kama hayo ndiyo yanayoleta ule utamu wa chuo hasaa..
 
Mkata Kiu,

Unaona sasa mnaojiingiza kichwakichwa bila kujua uhalisi wa hii story. Kama umesoma story yangu ungegundua mambo mawili. Kuna suala la G211 na suala la Benedict Mutungirehi.

Sina haja ya kurudia soma tena na tena na kama hayakunasa kichwani labda wewe ni mtu wa kusoma hata mara nane ndipo uelewe.

Suala la kubatizana jina la TRAITOR au G211 ni lile la April 1994 likakamilika May 1994. Suala la Mutungirehi ni lile la October 1994.

Ukisoma utaona kwamba yote mawili yanahusisha hako ka-kikundi kanakoitwa G211.

Hata suala la G211 halikuwahusu Faculty of Engineering wote. Liliwahusu wale ambao hadi May 1994 walikuwa First Year na ilipofika October 1994 wakawa second year.

Suala la Mutungirehi lunatakiwa ujue kwamba Mutungirehi alikuwa President wa DARUSO, kachaguliwa na Chuo kizima. Hivyo move yoyote for or against him ilitakiwa iwe ya Chuo kizima.

Lakini pale Nkrumah mipango ya kumpiga ilikamilishwa na kikundi kidogo cha wanachuo wakiwemo hawa G211, tena hawa G211 wakiwa hawana wiki zaidi ya tatu wameshinda kesi yaop ya kurudishwa Chuoni baada ya kufukuzwa.

Sasa pima hapa mwenyewe, kwa nini haka ka-kikundi kahusike kote, kule Engineering na kwenye Chuo kizima.

Wewe hapa unaniita traitor kiasi kwamba hata G211 anayekusoma hapa angekujua angekulaumu kwamba unawavurugia propoganda yao ya miaka mingi.

Rudia kusoma uone kwamba hata hao G211 hawakutuita TRAITORS kama unavyotuita. G211 walituita sisi TRAITORS kwa kile kitendo cha kufanya mtihani ile May 1994. Pale wakadhani wametunyoosha.

Lakini haohao G211 hawakuwahi kutuita TRAITORS kwa jambo jingine. Wewe unatuita TRAITORS kwa tukio la Mutungirehi maana yake umekurupuka kwani hata hao G211 hawakutuita TRAITORS kwa hilo tukio bali lile la May 1994 kule kwetu FOE kwa masuala ya Mathematical test and Exams.

Kuandika ilibidi niandike ukweli kwamba siku Mutungirehi anapigwa masumbwi wao walikuwa ni washiriki. Soma hoja zao humu uone kama hili la kumpiga Mutungirehi kama wanalikana. Hakuna hata mmoja anayelikana.

Kwa definition yako ukiondoa finalists, basi TRAITORS tulikuwa ni wanachuo wote ambao hatukuadhibiwa kukaa mwaka mmoja nyumbani tukarudishwa mapema December 1994.

Yale masumbwi na viti alivyopondwa Mutungirehi maana yake uliona alipata adhabu ndogo kwani ulitaka wamuue kabisa!
Asiyetaka hilo unamuita TRAITOR.

Lakini kasoro moja huioni. Katika yote haya hata wenzako ambao ni washiriki rasmi wa G211 na wako humu JF hawasemi kwamba kuna mahala tuliwahi kukaa na kukubaliana jambo halafu kukatokea ma-TRAITOR wa jambo hilo.

Kwa taarifa yako matukio haya hawa G211 walijfunza adabu kwamba ukitaka uungwe mkono kistaarabu basi fanya jambo moja. Ita kikao lete agenda yako tuijadili basi hata kama hatuipendi tutajiunga nayo kwa sababu tumesikiliza maoni ya wote na demokrasia imechukua mkondo wake.

Mbona walipojirekebisha na kuanza kufuata utaratibu huo hakukutokea mzozo wowote. Na sanasana tulikuwa tunaadhibiana ki-demokrasia.

Mfano, kule Engineering (FOE) kuna wakati walitaka tumchague mpinzani wa Maleva apite awe President wa DARUSO.

Kule FOE kulikuwa ni major campaign block, ukiletwa wakaku-approve basi umeukwaa u-President wa DARUSO. Mgombea akaletwa akashangiliwa sana. Aliletwa na jamaa wawili yaani Loti na Chapa.

Kumbe sasa hawa mabwana wakapata upinzani mwingine mlemle FOE. siyo wa sisi second year. Siyo wa sisi waliotuita TRAITORS mwaka uliopita. Bali upinzani mpya wa first year.

Hoja ya First year wakaona kwa nini watayarishiwe uongozi na watu wa third year. First year wakaunda umoja mpya kimyakimya wakamnyima kura yule mgombea na badala yake wakampa kura MALEVA. Hakika hata MALEVA na campaign yake walipata surprise maana hawakutegemea.

Hapa ndipo majina TRAITOR yangeweza kutumika maana ni kukiuka jambo ambalo awali mlikubaliana.

Jambo jingine ni pale ambapo tukiwa fourth year Sweke akawa anaachia ngazi ya u-President of DARUSO. Engineering wakakusanyika wote wakasema this time wasichukue u-President lakini wachukue u-Vice President wa DARUSO.

Wakakusanyika FOE wote wakakubaliana kwamba wamchague third year aitwaye Yustus Primus ambaye ni electrical Engineering. Wakakubaliana wote.

Imepita wiki moja kukatokea uvumi kuwa kuna kampeni ya chinichini kwamba Loti, Chapa, na Sweke hawamtaki tena huyu Yustus. Yustus hakuwa na tabia ya unafiki akaitisha kikao cha students wote FOE.

Tukajadili, bwana wakamgeuka wote. Campaigners wake kama Letinan Pasian wakamgeuka. Mimi hadi leo sijui kwa nini walimgeuka. Ikabidi Yustus Primus ajitoe.

Kumbe ile move imewaudhi FOE wengi. Wakakaa kimya hadi siku ya kupiga kura. Siku ya kupiga kura haohao Engineering wakamtosa yule chagua la Loti, Chapa na Sweke.

Nimeweka matukio haya mawili kuwa ndiyo yalifaa kuitana traitor na si yale ambayo hatukuwahi kukaa kikao cha kukukubaliana ajenda yoyote kama kumpiga Mutungirehi au kuchanachana mitihani.

Hata lile tukio la kiongozi wa G211 yaani Ladislaus Malima kukemewa na Prof. Masenge halafu akanyewa akawageuka wenzake wasigome hilo ndilo lilistahili kumpa jina TRAITOR maana alikiuka makubaliano ya wenzake ya kuongoza mgomo halafu anawaletea hadithi za kuwabembeleza kutogoma!

Huyu Malima najua alipo ngoja nikamkurupue aje hapa JF ajibu hoja za SubiriJibu
 
Last edited by a moderator:
Hakika wewe ni mwandishi mzuri mkuu..ni nadra sana kwa mhandisi,nina imani hujakalia tu hii talent..vinginevyo sisi tumepita hapo miaka ya 2000 na kwa kweli matukio kama hayo ndiyo yanayoleta ule utamu wa chuo hasaa..

Nashukuru Mkuu, Nachukia upotoshaji hasa wa historia ambayo binafsi ninaijua na sintakaa niisahau. Kuna dada humu anadhani ninawasakama CHADEMA kwa sabu ya kutaja wawili watatu. Sasa nutmie hii reply yako kumuonyesha ninavyokumbuka mambo yale kiundani.

Kwanza nisema ninamtaja sasa mtu aitwaye BENSON KIGAILA yaani Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo wa CHADEMA.

Kwa nini namtaja BENSON KIGAILA? Popote aliko sidhani kama ataisahau May 21, 1996. Kwa nini nimeitaja hii tarehe May 21, 1996? Ni kwa sababu watanzania wengi mnaikumbuka kama siku meli ya MV Bukoba ilipozama lakini tuliokuwa students pale UDSM akiwemo BENSON KIGAILA hatuikumbuki kwa hilo tu. Kuna zaidi ya hapo. Sikiliza story!

Unajua wale mabwana G211 walivyoshikishwa adabu ni kwamba walikaa nyumbani mwaka mzima na ikawabidi warudi Chuo October 1995. Nadhani kipindi hicho wakiwa nyumbani ndipo wakapata fursa ya kuingia kwenye vyama vya siasa na ndiyo maana sishangai kuwasikia baadhi ni wanasiasa maana wakiwa wanatumikia adhabu huko nyumbani ndipo Augustine Mrema akaondoka CCM akajiunga na NCCR-MAGEUZI na kuwa moja kwa moja mwenyekiti na baadaye mgombea urais.

Mrema alikuwa tumaini jipya kwa nchi nzima. Ndiyo maana hao wote niliowataja na nisiowataja sishangai kusikia political history yao ikianzia NCCR-MAGEUZI mwanzoni mwa 1995 mara baada ya Mrema kuwa Chairman wa NCCR.

Mrema, Lamwai na Marando walikuja Chuoni Jumamosi June 10, 1995 kama viongozi wakuu wa NCCR na watu wakakosa nafasi Nkrumah Hall. Alipotoka tulisukuma gari lake. G211 walikosa tukio hili kwani walikuwa wanatumikia kusimamishwa kwa mwaka mzima.

Turudi kwenye story ya kama BENSON KIGAILA na ile May 21, 1996. Wakati huu G211 wamesharudi Chuoni baada ya adhabu kumalizika. Karungubare hakurudi maana aliamua kuacha kabisa Chuo akaanza Chuo kingine yaani Dar Technical ambacho sasa ni DIT.

G211 wakarudi wakiwa wakiwa sasa na adabu kwamba hata likiletwa jambo hakuna haja ya kutumia masumbwi bali ni vikao vya majadiliano pale Revolution Square.

Kuthibitisha hili natoa mfano mmoja kwamba ikaletwa Chuoni kwamba Sylvester Sweke awe President wa DARUSO kum-succeed Lenganasa. Vikao vikafanyika tukakubaliana na Sweke akaukwaa uongozi. Hiyo ndiyo adabu na si mabavu kama ya mwaka 1994.

Nimeanza na mfano huo sasa tuje kwenye ile May 21, 1996. Wiki moja kabla kulikuwa na mfululizo wa vikao pale Rev. Square kuhusu allowance yetu ambayo tulikuwa hatujapewa. Ona sasa hili lilivyoendeshwa. Tukagawanyika ama tugome au tuandamane hadi Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu.

Mwisho wa majadiliano tukakubaliana kwamba tusigome wala tusiandamane. Tukiandamana hatutafika mbali bali kila mtu apande daladala na tujikute wote tuko Wizarani.

Pendekezo hili likakubaliwa na kushangiliwa na Chuo kizima. Walioogpa walitoa mawazo yao wakasikilizwa na wakaondolewa hofu na wakashindwa hoja kwamba sasa tutaishije wakati hatuna hela. Unaona hii ndiyo democracy.

Asubuhi ya siku yenyewe yaani May 21, 1996 tukakutana kidogo na safari ya daladala ikaanza. Tukajikuta tuko wote pale Wizarani, imagine kundi la chuo kizima kwenye mtaa mwembamba ule nadhani ni Jamhuri Street.

Kumbe kule chuoni walidhani mzaha waka-panic walipopigiwa simu na watu wa Wizarani kwamba tumejikusanya Chuo kizima pale Wizarani. Wote Wizarani na Chuo wakajua kwamba sasa hii imekuwa public issue na lazima itoke magazetini na wakati huo ITV au DTV.

Walichofanya Wizarani ni kuzipeleka zile pesa kimyakimya bila sisi kujua na kule Chuoni hakuna wanafunzi labda wenye sababu maalum. Wote tuko Wizarani hadi Nkrumah Street imefungwa haipitiki. SI kwa fujo bali kwa wingi wa wanafunzi waliojirundika nje ya jengo la Wizara.

Baada ya saa nzima FFU wakaja na Landrover tatu wakitokea kwenye junction inayotenganisha NBC na Mkapa House. Ee Bwana tulivyowaona FFU wakatoa kile kitambaa chao chekundu na wakatangaza tutawanyike.

Ona sasa umoja uliotokea tukaambiana palapale tutumie handkerchief ili yakipigwa mabomu yasitudhuru sana na wote tukaambiana tushikane mikono na tuchuchumae na wala hata mmoja asikimbie kwa amri ile.

Na kweli tukashikana mikono tukachuchumaa badala ya kutawanyika kama walivyotaka FFU. Na wakati huo hakuna anayejua kumbe tayari ITV wapo wanachukua tukio lote.

FFU wakaona sasa watashindwa hivyo wakatoa amri ya kutupiga mabomu ya machozi. Mabomu yakarushwa hapa tukatawanyika maana moshi ule hauvumiliki.

Askari wakaja wakakamata wachache. Sweke hakukimbia ilibidi akae asubiri kukamatwa.

Je, BENSON KIGAILA anahusikaje hapa?

BInafsi nilishuhudia mabomu yaliporushwa watu walikimbizana na kukanyagana hadi BENSON KIGAILA akapoteza viatu vyake akabaki na sox.

Benson alibaki mjini kwa masaa kadhaa walau aweza kuona namna ya kuvitafuta viatu vyake. Ikashindikana maana FFU walibaki wanalinda mtaa ule karibu siku nzima.

Sasa aijui kama Benson alipata hela ya kununua viatu toka kule mjini hadi UDSM au ilibidi atembee na sox tu njia yote ile ama kwa daladala.

Tulivyorudi chuoni tukakuta tayari wamezifikisha hela zile japo walikaa nazo mwezi mzima.

Usiku habari ile ya mabomu ikatangazwa kwenye Radio na TV lakini bahatai mbaya sana taifa zima lilikuwa limejikita na habari mbaya zaidi kujua ni nini itakuwa hatima ya meli iliyokuwa inazama yaani MV Bukoba.

Ni haya ya kukumbushana.

Utaona hapa tumefundisha adabu kuwa masumbwi kama yale ya G211 hayatakiwi na hoja ikiletwa mezani na ikaelezwa vizuri haiwezi kukosa kuungwa mkono na itazaa mashujaa zaidi kama ilivyomzaa BENSON KIGAILA ambaye tukio lake la kupoteza viatu tunalijua kwamba ni ujasiri aliouanza tangu siku zile na leo ni mtu mkubwa ndani ya CHADEMA
 
Huyu Malima najua alipo ngoja nikamkurupue aje hapa JF ajibu hoja za SubiriJibu

Namkaribisha kwa furaha aje kwa ID yoyote hata anonymous. Kama si member wa JF mfundisheni jinsi ya kujiunga maana naona wengine humu wanapapasa juujuu na mimi nataka kujibizana na mtu anayeijua the core events ya hii subject.
 
Your main aim is to try and clear you conscious after being with that TRAITOR label since then, no one will let you off the hook by debating with you on events that clearly shows you are a top down TRAITOR!!Deal with it with your wife and family you TRAITOR!
 
Mimi nimefuatilia sana hii habari na kwa mara ya kwanza ndio leo nimejua hasa kilitokea nini wakati ule, mimi nasikia fahari kusema kwamba nilisoma udsm lakini miaka mingi kabla yenu. Hapa kiini kikubwa cha tatizo kilikua unafiki wa faculty ya engineering, nadhani huu ulikua ni wakati wakina Mbwete wameshaondoka wakalundikwa maprofessa njaa walioanza kujikomba kwa serikali. Hizo enzi zetu za ealry 90s, ma spana boys walikua wanaheshimika chuo kizima na wanafanana na heshima hizo, isingekua rahisi eti vijitu vya mathematics, tena somo la units tu kadhaa vikawe sababu ya wanafunzi wenye akili na tarajio la nchi hii 211 kufukuzwa shule yote yote yote warudi nyumbani. Huu ni upumbavu kabisa enzi zetu dean wa faculty angetoka tu nje na kusema hatufany upumbavu huu kwa hiyo yeye ndio ange deal na hao wapumbavu wa mathematics. Lakini huyu mwalim aliyesababisha hili nae angekoma dean angesema simtaki na ikibidi sitaki tena kuchukua hili somo toka maths, na ndipo ingebidi mathematics kama support course waanza kuwabembeleza engineers. Sisi tulikua kwenye mgomo wa matusi ya nguoni na wote tukafukuzwa kwenda nyumbani na wanafunzi wa engineering walikua wanatutoa maholini kwa viboko na mabasi hayaruhusiwi kuja chuoni wote tulilazimika kuwa Nkrumah, hii ndio vita sio kuleta demokrasia kwenye maamuzi ya kufa na kupona. Ninaloliona lingine ni kwamba viongozi hawakuwa na muda wa kuwajengea wafuasi nguvu ya kuwaamini. Ila swala la mutungirehi kupokea offer ya safari toka serikalini huku akijua kwamba wanafunzi wa udsm walikuwa ndio primarity sauti ya umma, alikosea. Sasa tusameheane tusonge mbele tunahitaji kuungana ili kupambana na serikali ile ile iliyowaonea miaka ile shuleni, itoke madarakani maana kugawanyika kwetu ndio ushindi wao.
 
Your main aim is to try and clear you conscious after being with that TRAITOR label since then, no one will let you off the hook by debating with you on events that clearly shows you are a top down TRAITOR!!Deal with it with your wife and family you TRAITOR!

Kiraka,

If you would keep silence on this specific longtime subject then definitely non would care to revisit it.
Some from your so called G211 keep storytelling it as one of the heroic event but hiding a lot of truth behind the scenes, like initial presenters in this forum.
 
Mimi nimefuatilia sana hii habari na kwa mara ya kwanza ndio leo nimejua hasa kilitokea nini wakati ule, mimi nasikia fahari kusema kwamba nilisoma udsm lakini miaka mingi kabla yenu
Mkuu, heshima zako mkuu,

Ndipo hapo ujue kwamba propoganda za hawa mabwana zilivyoathiri wengi ambao hawakuwepo. Kama wewe tu mfuatiliaji wa masuala ya alumni yao hukupata ukweli na leo ndiyo unaupata basi ndivyo walivyotaka hawa jamaa. Tushukuru JF kuwepo kwa JF is the place we dare talk openly. Watu wanadhani wa mtishaji ni serikali tu lakini yeyote mwenye tabia za kutisha watu ili ama wasiseme ukweli ama wafuate wanayotaka wote ni sawa tu.

Hapa kiini kikubwa cha tatizo kilikua unafiki wa faculty ya engineering, nadhani huu ulikua ni wakati wakina Mbwete wameshaondoka wakalundikwa maprofessa njaa walioanza kujikomba kwa serikali

Concept yako ni ni sahihi kidogo labda kurekebisha mambo kidogo kama majina na events. Ukimtaja Mbwete napata hisia kwamba ulikuwa Civil Engineering.

Kipindi yanatokea haya Mbwete alikuwa hajaondoka kwenda Open University. Hii ilikuwa ni April 1994 na Civil Engineer kulikuwa na timu ya watu kama Branike yule mzungu verry brilliant. Pia walikuwepo pia kina Dr. Chamuliho, Boggy nk.

Mechanical Engineering alikuwepo bado Prof. Masuha akisaidiwa na akina Dr. Nyichomba. Electrical Engineering alikuwepo Prof. Peter Materu na ndiye alikuwa Dean of Faculty, akiwa na timu ya akina Dr. Chambega, Mr. Manyahi, Mr. Ishengoma, Dr. Mwinyiwiwa n.k.

Faculty of Engineering (FOE) was so strong. Tatizo ni issue ilivyokuja. Ukipuuza tukio la kufanyiwa fujo yule Mathematical lecture ile April 1994, basi unapoteza concept nzima ya suala hili na unakuwa umeliingilia kwa juu na ndivyo hawa G211 walifanikiwa miaka mingi chanzo hiki kisisimuliwe na kujulikana.

Nimeeleza sana kuwa Faculty of Maths walimwandikia Dean of Faculty of Engineering kuhusu fujo walizomfanyia yule lecture siku ya test. Maths Dept. walitaka walau student wa-apologise kwa sababu lecturers wa Maths waliogopa sasa kwenda kufundisha kule Engineering. Vinginevyo walieleza mapema kwamba bila hivyo hakuna sababu ya kuwa-risk lectures wao katika mazingira ambayo watadhurika ama kwa kupigwa au kudhuriwa zaidi.

Sasa, sijaeleza na sijui handling ilikuwaje baada Dean wa FOE kupata barua ya Maths.

Sasa kama Maths walishaandika barua kwa Dean. Foe ndiyo maana hata siku ya mtihani hawakuwa na sababu kuingia darasani na kugawa mtihani wakati issue yao bado iko ofisini kwa Dean of FOE.

Hadi hapa huwezi kuwalaumu Maths. Hivi hata wewe ungefanyaje kwa eneo ambalo mara ya mwisho ulienda na ukapone chupuchupu kupigwa halafu unaambiwa uende tena na watu ni walewale na hawajaomba radhi au kukana kwamba kitendo chao kilikuwa cha kihuni.

Hii ndiyo mantiki usiyotakiwa ku-ignore unapoliangalia suala lile

Sisi tulikua kwenye mgomo wa matusi ya nguoni na wote tukafukuzwa kwenda nyumbani na wanafunzi wa engineering walikua wanatutoa maholini kwa viboko na mabasi hayaruhusiwi kuja chuoni wote tulilazimika kuwa Nkrumah, hii ndio vita sio kuleta demokrasia kwenye maamuzi ya kufa na kupona.

Mkuu,

Tofauti yenu ni kwamba mgomo wenu ulikuwa na maandalizi na mkabishana wiki kadhaa ama mgome au msigome. Suala hili la G211 ni tofauti. Ukiliacha bila masimulizi kama haya unaweza kudhani kwamba kulikuwa na vuta nikuvute ya kwamba tuingie darasana au la.

Hakukuwa na hilo. Situation yawamba wengine wao darasani na wengine hawamo ilikuja kwa kuvamia sana yaani mazungumzo yalipomalizika kati ya Dean wa FOE, Maths na Student representative ndipo mitihani ikagawiwa kwa waliokuwamo darasani.

Hapa mimi simlaumu Prof. Masenge kuwakuta watu darasani. Kwa sababu kwanza asingeweza kujiamlia vyovyote peke yake wakati hata wanafunzi tumekubaliana kwa kupitia viongozi wetu yaani Class reps.

Kilichowashtua class reps ni kuona kwamba wakati wao wanatuwakilisha kule ndani kumbe kuna wengine hata hawakutaka kusubiri outcome wakaondoka kabisa chuoni!

Hivyo, hojja kubwa na ya kwanza kabisa ilikuwa JE, MBONA WENGINE WAMESHAONDOKA NA HATIMA YAO ITAKUWAJE?

Kwa mtu aliyebaki darasani muda wote, hoja hii isingekuwa rahis kwake kujua maana asingejua kuwa kuna watu waliondoka kabisa bali alijua kuna watu nje wanasubiri outcome ya kikao cha wawakilishi wetu.

Ila swala la Mutungirehi kupokea offer ya safari toka serikalini huku akijua kwamba wanafunzi wa udsm walikuwa ndio primarity sauti ya umma, alikosea.

hakuna anayebisha kwamba Mutungirehi alikosea. Taabu ilikuwa ni jinsi ya ku-deal na lile kosa lake. Yaleyale ya May 1994, move ya kumuondoa Mutungirehi kwa kumtwanga masumbwi pale Nkrumah Hall, ilisukwa kisiri sana na watu wachache wakapata support ya hawa G211.

Hapa G211 na waliomchukia Mutungirehi walikosea mahesabu. Inawezekana walihisi kuwa ingepigwa referendum angeshinda na kubaki kitini. Si hivyo. tuliporudishwa kutoka nyumbani na G211 wakazuiwa nyumbani tukapewa referendum tena kama questionnaire kama tunataka kuendelea na Mutungirehi au la.

Kampeni ikatembea chuo kizima kuhusu mabaya ya Mutungirehi, na waliompenda walimsifia. Tukapiga kura majority ikamkosa, ikabidi a-resign u-President wa DARUSO.

Kumbe, hakukuwa na sababu ya kumpiga kwa magumi na mateke bali tungempiga kwa sanduku la kura na history isingekuwa kama hivi ya aibu ambayo kwa aibu yake wameificha kwa miaka kadhaa.

Sasa tusameheane tusonge mbele tunahitaji kuungana ili kupambana na serikali ile ile iliyowaonea miaka ile shuleni, itoke madarakani maana kugawanyika kwetu ndio ushindi wao.

Tulishalisamehe siku nyingi na kulisahau. Ukiangalia mfululizo wa thread kuhusu Mutungirehi si mimi niliyeanzisha. Tatizo watu wanajibizana kwenye thread ile kwa kusifu ubabe wa ngumi za G211 bila kufafanua uhalisi wake kitu ambcho binafsi sikiungi mkono na kuona ninawajibika kuuweka ukweli ili tupambane kwa hoja za kihistoria na si kupambana kupotosha waliolisikia kwa mbali tukio hili.

Serikali tunapambanay anayo kwa njia nyingi tu. Fuatilia thread zangu humu jamvini. Unadhani ikiniona na kunijua nitabaki salama?
 
Back
Top Bottom