Deus F Mallya
JF-Expert Member
- Jul 28, 2011
- 705
- 440
Ni wazi kuwa CCM ni chama kikongwe kulinganisha na Vyama vyote vya siasa hapa Nchini; Ukongwe huu wa CCM umedhihirika hasa miaka takriban saba iliyopita kwa baada ya wengi maelfu kukihama chama hicho.
Waliobaki ndani ya CCM kwa sasa hawana tena Credibillity ya kuitwa viongozi kwa sababu hawaaminiki,Hawajui miiko ya Taifa wala Mila na Desturi za Chama cha Mapinduzi. Tumeshuhudia Baraza la Mawaziri likivunjwa kama mara nne hivi kwa kipindi cha miaka Saba, Tumeshuhudia hata wale ambao ni wateule wa Chama cha Mapinduzi wakiwatusi wananchi kwenye majukwaa ya Kisiasa, Wengine walidiriki kuwachapa viboko waalimu, Wengine wakapigana ngumi kule Arusha (Muulize Ole Sendeka), Wengine wanadiriki kuwatukana waajiriwa (Proffesionals) Matusi ya nguoni hadharani kuwa usomi wake ni wa Degree ya Chupi, Wengine sasa wananyukana kwa kutoleana Bastola kugombea nafasi za 'Uongozi' na wengine kuamua kuwahonga wananchi vitumbua kwa ajili ya kuomba wachaguliwe!..Wengine wanalalamika kupewa nafasi wakiwa wadogo, Wengine kuua kwao si ajabu!.
Kwenye ulingo wa Siasa; Kiongozi yeyote makini akiona haya na mengineyo lukuki yasiyoandikika pengine kuukifu ukurasa huu yanatokea na kuendelea kuzidi angetafakari upya nafasi yake na uwezo wake wa kuongoza na kufanya maamuzi: Maamuzi hayo pekee ndiyo yangeweza kumtofautisha na hao wengine. Lakini ukimya huo wa kiongozi wake mkuu naye unampotezea Credibillity ya kuitwa kiongozi.