Ukwasi wa mishahara kwa baadhi ya Watumishi.

msnajo

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
3,066
1,136
Wakuu salaam,

Naomba kwa pamoja tujadili hili swala.

Tanzania hii kuna watumishi wanalipwa mpaka 20ml, upande wa pili kuna wanaolipwa laki 3. Hii inatia uchungu sana. Najiuliza tofauti kubwa namna hii tunaenda wapi?? Majuzi nilisoma thread moja humu kuwa wabunge wamefika 10ml(sina uhakika). Hawa wanaolipwa huu mishahara ya ukwasi namna hii wanafanya kazi gani kubwa kiasi hicho ili hali uchumi wetu graph ipo zero. Mathalan wabunge kama kweli watalipwa hicho kiasi, najiuliza wanafanya kazi gani wakati wengine hakuna uwakilishi wowote wanaofanya??

Mfano hawa wabunge wa viti maalam, kazi yao nini?. Ukifika wakati kuchangia mjadala, utasikia wanavyozungumza upuuzi na kuunga mkono hoja za kipuuzi. Kuna haja ya kutazama upya hili swala la wabunge wa viti maalum. Mbaya zaidi hata hawalipi kodi wakati huyu wa laki 3 anakamuliwa haswa!
 
Leo Zitto amedhibitisha kwenye taarifa yake ya leo kwa Tume ya maadili ya viongzi kuwa mshahara wake kama mbunge mwaka 2010 ulikuwa Tsh 99.5 milioni kwa mwaka na posho Tsh 21.8 milioni kwa mwaka hivyo jumla Tsh 120 milion kwa mwaka sawa na Tsh 10 milion kwa mwezi.
 
Inamana Mbunge anapokea mshahara zaidi ya mil 8 hakatwi kodi
Watumishi wengine wa umma baadhi ya kada wanapokea laki 3 wanakatwa kodi

Kitu gani haswa kinachofanya wasikatwe kodi na mwingine akatwe?
 
Sio viti maalumu tu, hakuna kazi anayofanya mbunge ya kustahili kulipwa wanavyolipwa. Laki 4, kazi ngumu, kodi kibao na bodi wapo mlangoni wanataka 15%.
 
Wabunge wa ccm ndiyo hawana faida yoyote kwa sababu kwa wingi wao ni kulala tu wakiamka ni ndiyoo?!?!?! lakini hii mishahara na posho iliwekwa ili iwe ngumu kuwarubuni na kupindisha mambo,lakini mliona wakati wa mswada wa habari jinsi maccm yalivyopewa milioni kumi kila mmoja ili kupitisha huo mswada,tafsiri yake ni kuwa kazi aliyotumwa ameshindwa kuifanya na hivyo kuonekana kama hakuna wanachokifanya,
jambo jingine ni maswala ambayo wanayasimamia na kuyagharamia kwenye majimbo yao
 
Leo Zitto amedhibitisha kwenye taarifa yake ya leo kwa Tume ya maadili ya viongzi kuwa mshahara wake kama mbunge mwaka 2010 ulikuwa Tsh 99.5 milioni kwa mwaka na posho Tsh 21.8 milioni kwa mwaka hivyo jumla Tsh 120 milion kwa mwaka sawa na Tsh 10 milion kwa mwezi.

Huyu ZZK aache kutuzingua.. Badala ya kuweka mishahara ya 2016 anatuwekea ya 2010...
Kama hakumbuki leo ni 30Dec2016, the right time to reveal what transpired over the year.. Mbona kaweka orodha ya vitabu alivyosoma 2016?? Why salary ya 2010????

Shituka
 
Wabunge wa ccm ndiyo hawana faida yoyote kwa sababu kwa wingi wao ni kulala tu wakiamka ni ndiyoo?!?!?! lakini hii mishahara na posho iliwekwa ili iwe ngumu kuwarubuni na kupindisha mambo,lakini mliona wakati wa mswada wa habari jinsi maccm yalivyopewa milioni kumi kila mmoja ili kupitisha huo mswada,tafsiri yake ni kuwa kazi aliyotumwa ameshindwa kuifanya na hivyo kuonekana kama hakuna wanachokifanya,
jambo jingine ni maswala ambayo wanayasimamia na kuyagharamia kwenye majimbo yao
Kwaiyo wabunge wa vyama vngine wakipewa hiyo chapaa ni sawa kabisa mkuu?
 
Ki ukweli hii 15% kwa mshahara wa laki 5,ni unyanyasaji wa hali ya juu.Hivi kweli wamekosekana watu wakuelewa kwamba ndani ya laki 5. Ipo kodi ya nyumba,nauli ya kwenda kazini,bili ya maji na umeme? Mazingira ya kazi hasa kwa walimu wa sekondari si rafiki.Hivyo kwa ushauri wangu,ibaki hiyo 8% maana nijukumu la serikali kuhudumia watumishi wake but imeshindikana.Katika kuivumilia serikali basi kuna haja na wao waone huruma kwa watumishi wake.
 
Kuna kazi nyingine huo mshahara mdogo sana, 20mil ni sawa na $ 8,500 tu kwa mwezi..

Hivi, unafikiri Pilots wanalipwa sh. ngapi. ? Sbb wako wa hadi $ 12,000/month, ila Ulaya au Uarabuni, Pilots wanalipwa hadi $ 20,000 to $ 33,000 per month..!!

So, mshahara, unategemea kazi gani unafanya
...!!
 
Inamana Mbunge anapokea mshahara zaidi ya mil 8 hakatwi kodi
Watumishi wengine wa umma baadhi ya kada wanapokea laki 3 wanakatwa kodi

Kitu gani haswa kinachofanya wasikatwe kodi na mwingine akatwe?
Hii nchi mkuu imelaanika,acha tu twende hivo hivo lkn sio fair kbsa
 
ni roho ya kimaskini ndio inafikiri eti mishahara iwe flat rate across the govt au kampuni.
 
Dai mshahara wako upande na na siyo kuleta umbea wa mishahara ya wengine
 
Inamana Mbunge anapokea mshahara zaidi ya mil 8 hakatwi kodi
Watumishi wengine wa umma baadhi ya kada wanapokea laki 3 wanakatwa kodi

Kitu gani haswa kinachofanya wasikatwe kodi na mwingine akatwe?
Hii nchi ukiwaza sana unaweza ukawa chizi...

Watumishia hao wa laki tatu na bado kiinua mgongo hukwata tena kodi!!!
 
Hvi mbaka leo kuna watumishi wanalipwa mshahara wa laki 3!!?

Naomba niwatambue hao.
 
where were you when UKAWA, ACT and CHAUMA carry 'THE NEW CONSTITUTION' during 2015 campaign?? kwakweli MABADILIKO ni lazima 2020 tuache kulia lia
 
Back
Top Bottom