Ukuta Open space iliyovamiwa Ocean Road Wavunjwa

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Nimepita hapo saa moja na nusu usiku, yaani dakika chache zilizopita. Askari wa Jiji na polisi jumla hawapungui 100. Magari matano yamepark upande wa baharini yameeasha taa kumulika upande wa pili wa barabara kuliko na ukuta ambao unavunjwa na tingatinga.

Eneo hili liko baada ya hospitali ya agha khan karibu na uwanja wa golf. Kulikuwepo amani na utulivu, askari wamejipanga imara na tingatinga likiendelea kubomoa huo ukuta tartiiibu, kwa uhakika. Askari wawili walikuwa bize wakiharakisha magari kupita kasi, hivyo sikuweza kupiga picha
 
safi sana mama!hivi kwanini hawa watanzania wenye asili ya asia ndiyo wengi wamevamia maeneo ya wazi kwa nini?hawakuona master plan kabla ya manunuzi?jee sisi wamatumbi tunaweza kwenda india,uarabuni tukapata maeneo ya wazi kama wao watufanyavyo?
 
Mama mam mama mama mama mamasafi sana ndo tunatka viongozi kama ninyo hii nchi ya kwetu na onyesheni sasa mko kwa waajiri ya wananchi wa tanzania.
 
One down sooooo many to go can she do it like nike says............"just do it"
 
Nimepita hapo saa moja na nusu usiku, yaani dakika chache zilizopita. Askari wa Jiji na polisi jumla hawapungui 100. Magari matano yamepark upande wa baharini yameeasha taa kumulika upande wa pili wa barabara kuliko na ukuta ambao unavunjwa na tingatinga.

Eneo hili liko baada ya hospitali ya agha khan karibu na uwanja wa golf. Kulikuwepo amani na utulivu, askari wamejipanga imara na tingatinga likiendelea kubomoa huo ukuta tartiiibu, kwa uhakika. Askari wawili walikuwa bize wakiharakisha magari kupita kasi, hivyo sikuweza kupiga picha

Huyu mama pia anapashwa kuwa makini tusije sikia kuwa serikaki inatakiwa kumlipa fidia baaadae.tutakula na yeye maana uamuzi wa kukurupuka una madhala yake!Kazi njema mama.
 
Ni aibu kubwa kwa jiji kama Dar kutokuwa na open spaces.
Ukweli ni kwamba kwenye master plan ya jiji hayo maeneo yapo na yalipimwa kabla.
Lakini kutokana kukubuhu kwa ufisadi, maeneo yote yameuzwa na yanamilikiwa kinyemela.
Hao wamiliki batili ndiyo hawa wanajiona wana POWER, na kupeleka mikwala ya ajabu ajabu!
Mama, umekabidhiwa sururu, wang'oe wavamizi wote.
Sote tunakuombea na kukutakia ufanisi. Heshima ya nchi yetu inabidi irudishwe..ni wazalendo tu watafanikisha hilo.
 
Kumbukeni ya masaki! Aliyevunjiwa mahakama iliamuru alipwe fidia! Halafu tunakosea kusema kuwa wanavamia, tujiulize nani anawapa? kwani kabla ya huyu mama hivi viwanja vilikuwa hewani? je sehemu hizi viongozi wakubwa kuliko yeye huwa hawapiti? Je baada ya hapa kitafuatia nini? Bado tunachangishwa kuilipa dowans au mshasahau?
 
anayewapa huwa anahongwa kutokana na njaa kazini! si unajua jeuri ya fedha ila kukomesha tabia inabidi kuvunja kumkomoa aliyeenda kuhonga ili wajue fedha si zaidi ya sheria na anayebomolewa aende kumshtaki aliyemuuzia
 
12_10_mghpa6.jpg
Tingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam likibomoa ukuta uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan ambao umejengwa kinyume cha taratibu. (Picha na Robert Okanda).
 
Nimepita pale Palm Beach muda si mrefu napo papo FLAT ni VIFUSI TU
Du kweli mama Kiboko
 
safi sana mama!hivi kwanini hawa watanzania wenye asili ya asia ndiyo wengi wamevamia maeneo ya wazi kwa nini?hawakuona master plan kabla ya manunuzi?jee sisi wamatumbi tunaweza kwenda india,uarabuni tukapata maeneo ya wazi kama wao watufanyavyo?
hili ni swali zuri-jibu lake ni HAPANA-tatzo la hiii nchi baadhi ya wanasiasa wanawakumbatia sana hawa wa2 wenye asili ya asia,kiasi kwamba wankuwa na power sana,na kujikuta wanfanya mambo yao kwa nguvu ya hela,na kuifanya hii nchi wapendavo wao-
 
Kumbukeni ya masaki! Aliyevunjiwa mahakama iliamuru alipwe fidia! Halafu tunakosea kusema kuwa wanavamia, tujiulize nani anawapa? kwani kabla ya huyu mama hivi viwanja vilikuwa hewani? je sehemu hizi viongozi wakubwa kuliko yeye huwa hawapiti? Je baada ya hapa kitafuatia nini? Bado tunachangishwa kuilipa dowans au mshasahau?
Anayevamia si yule anayejenga tu ni pamoja na aliyempatia hicho kibali wote wavamizi, anayejenga inawezekana kapisha rupia ili apate kibali cha kujifichia tu lakini wote wahalifu, kama yule wa Palm Beach eti ana kibali halali, sheria ikifuatwa haianzii kwenye kibali (hard copy) inaanzia kilipotoka.
 
safi sana mama!hivi kwanini hawa watanzania wenye asili ya asia ndiyo wengi wamevamia maeneo ya wazi kwa nini?hawakuona master plan kabla ya manunuzi?jee sisi wamatumbi tunaweza kwenda india,uarabuni tukapata maeneo ya wazi kama wao watufanyavyo?

ubaguzi huo...!
 
anayewapa huwa anahongwa kutokana na njaa kazini! si unajua jeuri ya fedha ila kukomesha tabia inabidi kuvunja kumkomoa aliyeenda kuhonga ili wajue fedha si zaidi ya sheria na anayebomolewa aende kumshtaki aliyemuuzia

mimi nafikiri muuzaji na mnunuzi wote washtakiwe pamoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom