Ukuta kama wa Berlin wajengwa Tanzania kwa pesa za watanzania

Aibu kwa waliomadarakani Ila nguvu ya Umma ipo siku itauangusha uluta huo!! usitie shaka
 
Hivi mnasahau kuwa Tanzania yetu inaongoza kwa kuwa na Mafukara wengi kuzunguka eneo la rasilimali zetu? Bora hata wavuvi wa Sangara wanaopelekwa EU toka ziwa Victoria kwingineko its much worse than you can imagine. Niliwahi kushiriki mradi fulani around Bulyanghulu, niliishia Machozi tupu, Shinyanga ni Masikini mafukara (yaani masikini+fukara) kuliko watu wowote waliozungukwa na rasilimali.
Another thing sasa Kahama ni Kitovu cha Ukimwi kuliko eneo lolote mkoani Shinyanga.
 
Mwadui hakuna ukuta siku hizi, tena ilikuwa fensi ya waya si ukuta wa matofali, vipi Wabseshi bado wanaingia Mwadui?
 
Hivi Mkuu unasema kweli?
Ukuta wa km 80?...Ni kweli wanahitaji kujilinda kwa namna hiyo?
Labda utuambie ni wa material gani kwanza kama si wa tofali!

Lakini kwa namna yoyote, hiyo tofauti ya kipato kati ya kaburu na wabongo inasikitisha!
Naamini kauli mbiu ya MayMosi kuwa Watanzania wanaonekana WATUMWA katika nchi yao wenyewe!

mimi ningependa kuangalia hii topic kibiashara zaidi,
Kwanza material inatumika pale ni pure cement, mchanga na nondo ambazo zinatengeneza block za i think 4x4m ambazo ndo zinasimama.
hizi nondo na cementi ningependa kujua ni za TZ au ni imported kiasi kwamba zinatukosesha nafasi za kuuza
kampuni zilizopata tenda ni za kigeni tena wanyanyasaji sana, hivi hakuna local companies competent zinaweza kushinda tender za mgodini, kwa kawaida pale kuna vi-kampuni vingi tu na vyote vya nje na tender zao ndio kama hizi qualification ni kuongea kikaburu
nakumbuka wakati nipo geita gold mine misosi mingi ilikuwa imported kwa vigezo kwamba local suppliers hawawezi ku satisfy needs za wale jamaa, hivi kama hao local suppliers wanakidhi mahitaji ya mji mzima kv Dar, Arusha, Mwanza, itashindikana ku satisfy mgodi ambao una watu less than 3000..
 
Back
Top Bottom