Ukumbi wa sherehe ulio katika hoteli ya Landmark Ubungo kwa wizi, nausaluti....

Kiumbe duni

Senior Member
Dec 3, 2011
100
8
Wadau- jmosi iliyopita tulifanya sherehe ya harusi Landmark hotel ubungo ktk ukumbi wa ( Ibungila) kilichotukuta ukilinganisha na muonekano wa hoteli yenyewe ni aibu kwa mmiliki wa hoteli. Mimi nilikuwa ni mmoja wa wanakamati kwa hiyo nilifika mapema ukumbini, cha kushangaza wahudumu walikuwa ni wengi sana kila unayemuuliza anajibu mi nahusika na hiki mara kile tukawaacha tu. Kasheshe ni shughuli ilipoanza badala ya kuhudumia wao walikuwa na kazi ya kuiba, kuficha vinywaji kwenye masufuria makubwa, wakati wa chakula walipunguza sahani tulizohesabiana ili zisitoshe watuuzie chakula upya. Tulilipia viti mia 6 lkn baada ya kuvihakiki walivipunguza bila sisi kujua, wageni walipozidi tukaongeza viti 30 kwa 390,000/: pamoja na chakula. Walidai watapika chakula kingine kwa ajili ya watu walioongezeka kumbe haukuwa ukweli walichofanya ni kupunja watu ili chakula kilekile kitosheleze. Baada ya wageni wote kupata chakula sahani zikaisha wkt kamati ikiwa bado haijala, wakadai kila sahani itakayotoka ni elfu 13 wakati chakula kilikuwa kimebaki kingi tu na kilipikwa kwa ajili yetu, kamati ikawasusia walipoona tumesusa wakaleta sahani ili tule lkn tulikataa. Tulikuwa na ndafu 5 wakachukua 3 kwenda kuzikata ktk mbili zikabaki, ktk zile 3 moja wakaificha kwenye sufuria kubwa tukaishtukia ikabidi zile mbili zilizobakia tukaondoka nazo. Tulikuwa na local bia kreti 120 lkn zilivyoyeyuka huwezi amini, waliiba konyagi ndogo za chupa na ktk kupanga makreti matupu ya bia walificha kreti 3 zenye bia tukazikamata. Katika wizi huu wanashikiana wote mpaka mameneja ila sijui kama mmiliki wa Hotel anajua. Kumbe ukumbi huu unajulikana kwa wizi, mapambo yalikuwa feki chakula kila mtu alikilalamikia hakikuwa na ladha. Nimewajulisha wadau ili msije mkaingia mkenge kama sisi.
 
usiishie kulalamika tu ndugu, chukua hatua.........huu sio muda wa kufumbia wizi peupe namna hiyo.
 
kila mtu nchi hii amekuwa mwizi,
thanks for information ,tutachukua tahadhari
 
du hii ni noma aisee ngoja nimshtue massawe alikua anautaka ule ukumbi....

Ukitaka kuamini muulize mtu yeyote ambaye amehudhuria au kufanya sherehe ktk ukumbi huu. Labda mmiliki wa ukumbi hajui hujuma zinazofanywa na wafanyakzi wake. Namhurumia masawe wako kama amekwishalipia.
 
Lol asa si wanauwa hiyo kitu! Fukuza wote mwenye hotel hawa watakuachia janga wao wataenda gonga mzigo pengine!
 
Landmark ni wezi sana sio kwenye ukumbi tu,hata kwenye mahesabu ya kawaida ukienda kupiga pale msosi watakuchanganyia sana.
Mie december nusura nimtoe mtu roho,nimelipa nasubiria chenji,baada ya dk20 kupita chenji sipati kwenda kufuatilia wananiambia mhudumu kaenda nyumbani.Nikawaambia mziki wa leo hakuna wa kuuzima ,ndo wakanipa chenji,******* sana,mie nimeapa sitaenda hiyo hotel tena.
 
Hata chakula chao wanauza ghali sana halafu si chochote si lolote ni bora ukale kwa mama lishe.
 
Wizi na ukabila ndiyo viti anavyoendekeza mwenye biashara. Ila hajali hata ukienda ku complain
 
Wizi na ukabila ndiyo viti anavyoendekeza mwenye biashara. Ila hajali hata ukienda ku complain
Ktk kulalamika kwetu tukawaambia wale wafanyakazi tutamwambia bosi wao, wakatujibu kwa kejeli " ni afadhali ya majibu tunayowapa sisi kuliko mtakayopewa na bosi wetu"
 
Ktk kulalamika kwetu tukawaambia wale wafanyakazi tutamwambia bosi wao, wakatujibu kwa kejeli " ni afadhali ya majibu tunayowapa sisi kuliko mtakayopewa na bosi wetu"

Wasije wakathubutu kunijibu Mimi hivyo watakiona Kilichomnyoa kanga manyoya
 
Back
Top Bottom