Ukumbi wa Land mark ubungo

Kireka1980

JF-Expert Member
Mar 18, 2008
302
43
mimi nina mpango wa kufunga harusi mwezi wa sita miongoni mwa kumbi ninazozifikiria ni landmark kutokana na unafikika kirahisi, lakini nimepata habari kwamba jamaa wana huduma mbovu sana kama vile kuwa na wahidumu wachache, wizi wa vinywaji na vyakula vya muda mrefu. wadau kuna mwenye experience?
 
Go go go go.... Kila ukumbi hufanya hivyo hivyo!!!!

wee make sure kamati ya vinywaji iko fit ukichukua walevi wakishaanza kulewa na wao watakusaidia kuzificha ili wanakamati wasijewakalewa zaidi na kuharibu sherehe, kamati ya mapokezi nayo ikizobaa ndo hivyo tena
 
Nakubaliana na Baba Enock kuwa mafanikio ya shughuli nzima ni wanakamati wako. Kila ukumbi una misheshe zake. Kwa mfano uzoefu wangu hata kwa upande wa chakula (kama unakipata wa outside catering eg Istana) ni kuwa usipokuwa macho plates zinapunguzwa kinamna ili uombe zingine ili gharama iwe juu. Hivyo Kamati zote zinatakiwa ziwe sawasawa. All the best.
 
mimi nina mpango wa kufunga harusi mwezi wa sita miongoni mwa kumbi ninazozifikiria ni landmark kutokana na unafikika kirahisi, lakini nimepata habari kwamba jamaa wana huduma mbovu sana kama vile kuwa na wahidumu wachache, wizi wa vinywaji na vyakula vya muda mrefu. wadau kuna mwenye experience?

Hey jaribu lunchtime. Uko karibu na external pembeni ya barabara ya mandela upande wa kushoto kama unaelekea tazara. Bei za zao ni nafuu na pako elegant, ingawa bado hapajawa maarufu. Pia sio mbali na land mark, so kama unaona landmark panafikika kirahisi basi hapa pia.
 
Ze Marcopolo ni ukumbi gani hauna jina? Unapotaka kumwelekeza mtu mahali anagalu taja jina lake. Ni vyema ufafanue zaidi. Wadau wanaweza kuwa wengi zaidi.
 
Ze Marcopolo ni ukumbi gani hauna jina? Unapotaka kumwelekeza mtu mahali anagalu taja jina lake. Ni vyema ufafanue zaidi. Wadau wanaweza kuwa wengi zaidi.

Nimeandika jina lake hapo juu. Unaitwa lunchtime. Uko kwenye Hotel inayoitwa lunchtime hotel.
Kuna kumbi mbili mpya kwenye hiyo hotel.
 
Ze Marcopolo ni ukumbi gani hauna jina? Unapotaka kumwelekeza mtu mahali anagalu taja jina lake. Ni vyema ufafanue zaidi. Wadau wanaweza kuwa wengi zaidi.

wewe jamani hauna macho? unaitwa lunchtime, Uko karibu na external pembeni ya barabara ya mandela upande wa kushoto kama unaelekea tazara

wabongo! mnachekesha :)
 
Muhimu ni kuwa na kamati iliyo makini zaidi ili kudhibiti hizo kero ambazo mara nyingi zinaharibu au kuyumbisha sherehe.

Awepo mtu makini kwenye kamati ya vinywaji maana na hao wahudumu wanaangalia 'situation' ya kuiba hivyo vinywaji wakiona wahusika kwenye hiyo kamati ni legelege. siyo kila sherehe wanaiba.

Pia naamini ukumbi kama BANORA uliopo baada ya mlimani city maeneo ya savei, ni mzuri na rahisi kwa mtu kufika.
 
Well,

Nilifungia ndoa yangu pale. Nilitumia ukumbi mkubwa na yafuatayo ndiyo ninayoweza kukushauri.


  1. Ukumbi mkubwa utumie ukiwa na uhakika wa kuwa na wageni wanaozidi 600.
  2. Ukumbu mkubwa unavuta lakini hawajui kuupamba kiasi unakereka sana na kamati yako itajisikia vibaya kuona namna mpambaji alivyo na nyodo kwa mapambo ya Laki 7.
  3. Ukibahatika kuwa na kamati nzuri basi chakula na vinywaji pale utafaidi, lakini kamati zako mbili hizi zikilemaa kidogo wahudumu wao ni wezi haina mfanowe! Wanahamisha vinywaji vikali na wanaviweka kwenye boxes flani wanakuwa nazo. Nilijikuta naamini vinywaji vimeisha kumbe kreti mbili zilikuwa zishabebwa. Mbaya zaidi nikajikuta zinabaki kreti 5 za beer. Kila beer moja inauzwa Tshs 2,000 na mkataba wao ukiusoma hausemi hivyo. Ukibakiza beer unapewa limit ya siku 3 tu uwe umechukua beer zako vinginevyo zinakuwa zao bila hiari yako. Ukiamua kuwauzia kila beer moja wanaiununua kwa Tshs 700! Hapo lazima uwe una kreti zako za haraka mapema tu.
  4. Security ya pale ni ya kuridhisha kwa kiwango flani na parking inaonekana kuwa ya afadhali.
  5. Ukimaliza ndoa yako sikushauri kulala kwenye hoteli yako labda siku ya tukio tu. Honeymoon kufanyia pale pana kero sana. Inategemeana na kipato chako, kama kinaruhusu napendekeza jaribu kwenda Zanzibar (L'ajema Hotel) au nenda White Sands uta-enjoy Honeymoon yako ambayo ni ya mara moja na hutokumbana nayo tena katika maisha ya ndoa.
Vinginevyo, mimi nipo Dar na namba yangu ndo hiyo, niko tayari kukuchangia kama mwanachama wa JF na si lazima unipe kadi ya mwaliko!

Mac
 
Back
Top Bottom