Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukubwa wa serikali sio idadi ya mawaziri bali matumizi!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Aug 22, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 1,905
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Napenda kutoa elimu tu kuhusu ukubwa wa serikali hapa. Tunavyoongea ukubwa wa serikali sio tu idadi ya mawaziri bali ni kiasi gani serikali inatumia mapato ya nchi kuhudumia shughuli na biashara za serikali ukilinganisha na shughuli za maendeleo. Unaweza kuwa na mawaziri wachache lakini kama serikali inatumia pesa kulipa wafanyakazi wengi zaidi na miradi mingi zaidi basi serikali imeongezeka ukubwa hata kama mawaziri wamepungua!!. Serikali sasa inajiingiza kwenye shughuliza biashara za ATC huduma za Tanesco na miradi mingine mingi kama mikataba ya mashamba ni moja kati ya vitu vinavyosababisha serikali kuwa kubwa. Kama mkuu wa Tanesco anaripoti kwa waziri na pesa ya Tanesco inatoka serikalini basi wafanyakazi wa Tanesco tukubali au tusikubali ni wafanyakazi wa serikali!!. Napenda kutoa ufafanuzi kwani watu wengi hapa wanafikiria ukubwa wa serikali ni idadi ya mawaziri pekee.
   
 2. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 868
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lakini hapa kwetu Tanzania, idadi ya mawaziri inaongeza gharama automatically. Yale mashangingi wanayotembelea, gharama za vikao, safari, mishahara.. chai, mialiko ya nje.. nk
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 10,619
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Kamundu,

  ..ukubwa wa serikali ni pamoja na wingi wa mawaziri na hayo mengine uliyoyataja.

  ..hebu tuanze kwanza na kupunguza idadi ya mawaziri, pamoja na "viongozi."

  ..pia tupunguze au tuondokane na shughuli zote ambazo haziongezi mapato ya serikali.

  ..kwenye nchi za wenzetu shirika lenye monopoly kama Tanesco lazima liingize faida kwa serikali.

  ..kama tunaweza kupata mapato toka kwenye breweries kwanini tunashindwa kupata mapato toka Tanesco??

  ..kuhusu ATC au shirika la ndege hilo nadhani tunapaswa kuachana nalo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 1,905
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hata kama tukipunguza mawaziri watano na mashangingi yao labda Billion 3 kwa mwaka haitakuwa pesa nyingi ukilinganisha na pesa mfano wanazopewa Tanesco au ATC ambayo haina hata ndege na wafanyakazi wa haya mashirika. Kama kweli tunataka serikali iwe ndogo ni kupunguza majukumu ya serikali ikiwa ni pamoja na serikali kujitoa kwenye shughuli za biashara. Ni lazima tuelewe vilevile hizo pesa za ATC ambayo haina faida zingeweze kupelekwa kwenye elimu na afya.
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  KAMUNDU mchango wako ni mzuri, lakini huwezi kutenganisha wingi wa mawaziri na ukubwa wa serikali. Hiki ni kiashiria muhimu..... huwezi kukikataa wala kukipuuza kwa namna yoyote ile. .............. SOMA MICHANGO ya wadau wengine ili elimu unayoitoa isiwe na matango mwitu!!!!!!!!!!!!!!!..
   
Loading...