Ukosefu wa ladha ya lugha ya Kiswahili kwenye mapenzi

Kwanini nanyi msirengeneze tamthilia au movies mkatumia hayo Maneno ya mahaba ya Kiswahili ili mkitangaze Kiswahili chenu?

Mwanao hakiiti dadii weye? Just curious! Ofisini kwenu mnaandika report za lugha ya taifa? Are Dr. Riwa? Kama ndio kwanini maprescription msiandike kwa Kiswahili kilichochanganywa na kilatini?

Ananiita hivyo...tena na king'eng'e kingi tu ambacho hata mie hakipandi! But thats 'inevitable', lazima nimlee katika hali ambayo ataweza kuja kushindania na wenzake soko la ajira au biashara huko baadae, ukimnyima na wenzie wakipata...atashindwa ushindani ni itakuwa ni kosa langu!

Lakini kwenye mapenzi tunaongelea 'uhalisia'....na sioni kama bi mdada atakuwa 'halisi' akija niambia sijui I love you sijui fefe fefe...mi naona anakuwa 'fake'!
 
Nimekuwa nikisikia "ninakutamani" na "nimekutamani" ikitumiwa kabla ya kujua kuna neno "I miss you".

Na kama nikumbukie sentensi ya enzi hizo basi itakuwa ni kutoka kwa bibi yangu nikiwa na miaka 5-6 hivi, akisema "Nimekutamani sana, kwa sababu hujaja kuniamkia wiki nzima" na hadi leo hii, baba zangu husema hivyo hivyo nikizungumza nao baada ya kukaa kitambo bila ya kuongea nao.

Kwa hiyo labda hakuna maana ya moja kwa moja kutoka kwenye Kiingereza kwenda kwenye Kiswahili, lakini maneno yanayoshabihiana maana yanayotokana na tofauti za kijamii yapo.

Kiswahili kina maneno mengi yakuweza kumtoa nyoka pangoni lakini wengi wetu hatuyajui. Na mbaya yake ni kuwa hakuna juhudi zozote za watu kutaka kujifunza.

Shaaban bin Robert amesema haya kuhusu Kiswahili

Kiswahili kwa dhahiri, kimo ndani ya msitu,
Hili nimelifikiri, kwa muda wa siku tatu,
Na sasa nalihubiri, afahamu kila mtu,
Hima pakutane watu au tutahasiri

Hapana lugha damiri, ana yake kila mtu,
Mimi hasa nafikiri, tunachekwa na wenzetu,
Tumo katika ghururi, ya kutupa lugha yetu,
Hima pakutane watu au tutahasiri

"titi la mama li tamu..." - shaaban robert
 
Gaijin naomba nikuandalie japo chai ya mkandaa

Eeh na wewe mkandaa ndio nini?

Gaijin sijafikiria kujifunza kiswahili kabisa, labda kidogo kifaransa nikachange mind. Kwa muda nafikiria kujifunza ujasiriamali ili niongeze kipato cha kaya yangu na pia niachane na utumwa wa kuajiriwa unaonifanya niwe mbali na wapendwa wangu (mchuchu, mtoto, mama n.k)
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu enzi za mama zetu walikuwa courted kwa barua za mkono kwa mashairi ya Kiswahili.

Ukiziona hizo barua lazima uende ngoi. Unabaki na wewe kuweka mgomo kuwa hukubali mpaka na wewe upate wa kukuandikia barua .........japo hata barua pepe :confused2:

Hali yangu waijua,
Nimekonda kama uzi,
Sili silali kwa saa,
Wala sishushi pumzi,
Huba yataka niua,
Kwa fikira na majonzi

Kuwa sipati barua,
Imenizidi simanzi,
Wala moyo sijatua,
Silali yapata mwezi,
Huba yataka niua,
Kwa fikira na majonzi

*Usikubali kwa nini hapo? :mwaaah:

aisee umenikumbusha shairi ambalo mpenzi wa hayati seth benjamin mpinga aliliandika baada ya kifo cha shujaa huyo wa azimio la arusha, ngoja nikalitafute fasta fasta, yaani lina mahaba makali yanasuuza na kuuchoma mtima pamwe!
 
Nadhani tunakosea tunapochukulia kujifunza Kiswahili ni sawa na kujifunza lugha ngeni kabisa kwa hiyo itakuchukulia muda wako mwingi na kukunyima nafasi ya kujiongezea kipato. Hapana. Unaweza kujifunza kwa kusoma vitabu vilivyoandikwa kwa Kiswahili. Pia kusikiliza nyimbo hususan za taarab za zamani zitakupiga bonge la msasa katika Kiswahili. Kwa hiyo unakuwa unajifunza kwa kupitia mambo ya staarehe tu.

Pia kwenye jumuiya kama hii, ukiona neno hujui maana unauliza......haba na haba hujaza kibaba.

Kujifunza Kiswahili kwa mtanzania ni rahisi iwapo kaweka ile nia tu na raghba ya kufanya hilo ipo
 
Fanya na mahamri yalokolea hiliki

manta khofu!
mahamri ntayatia tui bubu na mkate wa bafta pembeni vipi?utafaa?
kisha ntakuandalia mkekani juu nimefunika kawa yenye rangi ya samawati
halafu nakukosha mikono kisha nikukaribishe ,ukishamaliza ntakupa maji ya sharbat yenye barafu kidogo na limao kuhanikiza hirmu!
 
Eeh na wewe mkandaa ndio nini?

Gaijin sijafikiria kujifunza kiswahili kabisa, labda kidogo kifaransa nikachange mind. Kwa muda nafikiria kujifunza ujasiriamali ili niongeze kipato cha kaya yangu na pia niachane na utumwa wa kuajiriwa unaonifanya niwe mbali na wapendwa wangu (mchuchu, mtoto, mama n.k)
chai ya mkandaa ni chai ya mkono mmoja!
 
Ziwa la mama tamu japo la mbwa. Jamani uzalendo umenishinda! Mzee wa watu shakespeare analalama kazama kwenye dimbwi la mahaba haramu, kujinasua hawezi.

What potions have i drunk of
siren tears
Distilled from limbecks foul as
hell within
Applying fears to hope and
hopes to fears
Still loosing when i saw myself to
win
What wretched errors hath my
heart commited
While it hath thought itself so
blessed never
How have mine eyes out of their
spheres been fitted
In the distraction of this
madding fever
O benefit of ill now i find true
That better is by evil still made better
And ruined love when built
a new
Grows fairer and far more strong
far greater
So i return rebuked to my
content
And gain by ills thrice more than i have spent.
 
aisee umenikumbusha shairi ambalo mpenzi wa hayati seth benjamin mpinga aliliandika baada ya kifo cha shujaa huyo wa azimio la arusha, ngoja nikalitafute fasta fasta, yaani lina mahaba makali yanasuuza na kuuchoma mtima pamwe!

Fanya uje utubandikie humu, tufurahie mahaba yaliyoelezwa kwa Kiswahili.

Wenzio waliandikiwa haya kwenye barua za "uchuchu" enzi zao.......must have been niceee :)

Karibu wangu mpenzi, njoo ukae moyoni
Pita bila ya simanzi, nakuomba niamini
Naapa takuhifadhi, takulinda na majini

Na mikono ipo wazi, tayari kukupokea
Ukae kwangu hirizi, kunikinga na wabaya
Daima nitakuenzi, ili tupate tulia
 
manta khofu!
mahamri ntayatia tui bubu na mkate wa bafta pembeni vipi?utafaa?
kisha ntakuandalia mkekani juu nimefunika kawa yenye rangi ya samawati
halafu nakukosha mikono kisha nikukaribishe ,ukishamaliza ntakupa maji ya sharbat yenye barafu kidogo na limao kuhanikiza hirmu!

Umetishaaaa.......

ila hata juice ya ukwaju yenye arki kwa mbaliii, fahuwa hapa. Sina makuu :shut-mouth:
 
Fanya uje utubandikie humu, tufurahie mahaba yaliyoelezwa kwa Kiswahili.

Wenzio waliandikiwa haya kwenye barua za "uchuchu" enzi zao.......must have been niceee :)

Karibu wangu mpenzi, njoo ukae moyoni
Pita bila ya simanzi, nakuomba niamini
Naapa takuhifadhi, takulinda na majini

Na mikono ipo wazi, tayari kukupokea
Ukae kwangu hirizi, kunikinga na wabaya
Daima nitakuenzi, ili tupate tulia

nafasi ya moyo wangu, yako wewe peke yako
takufungia na pingu, sitompisha mwenzako
Na upoe humu mwangu, niwe wako mali yako
daima iwe dawamu,kukupenda kwangu tunu
lako halinishi hamu,nakupenda sina laumu
wajijua kwa matamu,wanasema wanipa ndumu
yailat nakupenda ,wajijua u wangu mimi

tulia pate ya kweli,sizuzuke na maguberi
tulia nipe kweli kweli,waniache mafedhuli
lugha yako ya hiyari,huna chao kile kiburi
yailati nakupenda,wajijua u wangu mimi
 
Umetishaaaa.......

ila hata juice ya ukwaju yenye arki kwa mbaliii, fahuwa hapa. Sina makuu :shut-mouth:

juice muachie Kaunga siye yetu maji ya sharbat!
sukari yetu ni tende,kitafunwa ni halua!
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha, usinifanye nikakopi nikajidai nimetunga mwenyewe

Hili shairi liko kimahaba zaidi, sema watu tumekipuuza kiswahili, nacho kimetuacha
Sasa tunarudi kukilaumu

Sasa hivi kizazi cha leo, hata kuzingatia mizani na vina kwenye ushairi ni ndoto, sababu ya uchache wa misamiati tunayoijua.

Kuna watu enzi za mama zetu walikuwa courted kwa barua za mkono kwa mashairi ya Kiswahili.

Ukiziona hizo barua lazima uende ngoi. Unabaki na wewe kuweka mgomo kuwa hukubali mpaka na wewe upate wa kukuandikia barua .........japo hata barua pepe :confused2:

Hali yangu waijua,
Nimekonda kama uzi,
Sili silali kwa saa,
Wala sishushi pumzi,
Huba yataka niua,
Kwa fikira na majonzi

Kuwa sipati barua,
Imenizidi simanzi,
Wala moyo sijatua,
Silali yapata mwezi,
Huba yataka niua,
Kwa fikira na majonzi

*Usikubali kwa nini hapo? :mwaaah:
 
weye tena!mwanafunzi wangu ninayependezwa naye(hapa lazima kutakuwa na kesi muda wa kipindi wenzio Asprin na SnowBall watarusha ngumi najua)
weye nitakuandalia kwa mujibu ya nukuu #88
Shukran snowhite. Mashallah nipatapo siha njema sifa zikuendee mwalimu wangu, mi bawabu tu ila tende naitia mdomoni hamad imekuwa halua! Alhamdulillah! Pema........ukipema si ........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom