Ukomunisti uliwafanya watumwa korea ya kaskazini!

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
2,128
1,225
madhala ya kutawaliwa kikomunisti ni makubwa na mabaya sana , mojawapo ni raia wa nchi kuwa watumwa kisaikolojia. Ona jinsi watu wa korea kaskazini walivyolazimishwa kisaikolojia kutawaliwa na mtoto wa kim Il Sun-Kim iljong un! Ina maana hapo korea hamna mtu mwenye busara zaidi ya mtoto wa marehemu Kim Il sun!

hapo korea kuna pengine 70% ya raia wanachukizwa na kitendo hicho, ila hawana pahala pa kulalamikia. Vyombo vyote vya habari vimeshikwa na serikali ya kidikteta! halafu zitanza kutungwa kwaya na watu kulazimishwa kumuimbia huyo kijana wa miaka 29 kuwa ni mzuri saana na ana hekima na siasa zake ni mfumo wa babake!

Usiombe kutawaliwa na wnasiasa walioiteka nchi na kuifanya ni yao na kutoa maamuzi ya maudhi kila kukicha. Nawaombea wakorea kaskazini mungu awafumbulie macho ya haki na siku moja wawatimue wanasiasa walioiteka nchi yao na kuanzisha siasa za kimwinyi za kulindana.
 
ndio maana ukomunisti umekufa kifo cha haibu!!!!
 
Anzia kwanza nyumbani kwenu wewe! Utumwa wa wa-TZ ni mbaya zaidi kuliko huo unaouona kwa Wakorea.
 
Ofcoz kwa hesabu pevu utawala huu si ni wa kifalme tu, kuna tofauti gani na S. Arabia ?
 
madhala ya kutawaliwa kikomunisti ni makubwa na mabaya sana , mojawapo ni raia wa nchi kuwa watumwa kisaikolojia. Ona jinsi watu wa korea kaskazini walivyolazimishwa kisaikolojia kutawaliwa na mtoto wa kim Il Sun-Kim iljong un! Ina maana hapo korea (1)hamna mtu mwenye busara zaidi ya mtoto wa marehemu Kim Il sun!

(2) hapo korea kuna pengine 70% , ila hawana pahya raia wanachukizwa na kitendo hichoala pa kulalamikia.(3) Vyombo vyote vya habari vimeshikwa na serikali ya kidikteta! halafu zitanza kutungwa kwaya na watu kulazimishwa kumuimbia huyo kijana wa miaka 29 kuwa ni mzuri saana na ana hekima na siasa zake ni mfumo wa babake!

(4)Usiombe kutawaliwa na wnasiasa walioiteka nchi na kuifanya ni yao na kutoa maamuzi ya maudhi kila kukicha. Nawaombea wakorea kaskazini mungu awafumbulie macho ya haki na siku moja wawatimue wanasiasa walioiteka nchi yao na kuanzisha siasa za kimwinyi za kulindana.
1. Hivi wewe ndio unaona una busara kuliko wakorea wote !, hayo maendeleo walipata kwa utumwa wao ni kwa manufaa ya nani ?
2. Unapata wapi hiyo 70% ? kama si akili za kukariri, Watanzania wangapi hawiungi kono CCM!?
3. Umesahau nyimbo na mapambio ya Baba wa Taifa na Chama chao ! Chama chao kinatukuzwa mpaka kumbi za starehe !
4. Tunateseka na maamuzi mabaya ya Richmond, EPA, nk nini mchango wako ?
Anzia kwenu kwanza ndio unabii mzuri !

 
Mimi nimewapenda Wakorea wana umoja na utaifa.Kuhusu Rais awe nani siyo tatizo ila je analeta maendeleo?Kuna faida gani kubadilisha Marais wakati chama ni hicho hicho kisichojal wananchi?
 
madhala ya kutawaliwa kikomunisti ni makubwa na mabaya sana , mojawapo ni raia wa nchi kuwa watumwa kisaikolojia. .

Waulize na wagiriki wanaotawaliwa na ubepari, pia kuna wale occupy wall street wanasema wao ni 99% inafaa uwaulize nini ubepari umewafanya.
Ukipata jibu, unaweza kuuzimua usemi wako.
 
Kim Jong-un ni mtoto. Hata Wakorea wenyewe wanajua. Suala ni kuwa siasa za Pyongyang zimejikita katika mapambano dhidi ya Washington. Dhana imekuwa ni kuendeleza ukoo wa Kim Il Sung (Baba wa Jong-Il) kwa imani kuwa angalau misimamo yake inatabirika na ni ujumbe kwa Marekani na wenzao kuwa misimamo ya Korea ni ile ile japo kimsingi wanaotawala ni (hata kisiasa) kwa sasa ni wanajeshi na Baraza la Kikomunisti. Lakini kwa mawazo rahisi tu ni kuwa kuna wengi ambao wangeweza kuongoza badala ya Jong-un, ila hawaaminiki (wasije wakaja na habari za demokrasia).

Niliona wanajeshi (wanawake) wanavyolia katika msiba wa Jong-Il. Almost wote walikuwa wanalia kilio cha kupagawa. Kwa namna navyowajua binadamu walivyo (pamoja na tofauti zetu zote) nahofu kuna "kaigizo" fulani (angalau kwa baadhi yao) kalikokuwa kanaendelea. Naweza nisiwe sahihi.
 
Aisee asije mtu akakupangia jinsi ya kuishii na mkeo .....atakuchukulia . Mtoa mada think out of box. Nchi yako yahitaji sera za nchi then vyama vya siasa viwe mbwembwe tu. Maanake hata chizi akiwa kiongozi National interest itakuwa palepale na sio interest za watu binafsi. Ndivyo ilivyo Korea. Dogo ni ICON tu ya Ideology yao lakini waongoza nchi wapo behind. USA ni communist wa kwanza duniani. Jiulize hivi kwa nini ilitoa bailout kwa kampuni zake wakati wa economic crisis. Kwa nini huduma za awali za shule na afya ni lazima kwa watu wote. Kwa nini makazi ni haki ya kila mauamerika. Kwa nini marekani yapigana vita pale utakoonyesha unavuruga interest za makampuni yake. Mkulima marekani anapewa ruzuku asizalishe chakula au azalishe wewe umemabiwa no ruzuku?. Marekani kuna watu wachache kura zao zina weight kubwa kuliko raia wa kawaida. Tuanzie hapo.
 
raia wa north korea wanapata tabu sana,kuna defectors wengi wanaojaribu kwenda china,south korea na kwingineko ili japo waishi kwa amani,kama wangekuwa wanajua dunia inakwenda wapi,na nni kinatokea duniani kwa sasa,basi wangetakiwa wafanye revolution zaidi ya waarabu walivyofanya,
 
Back
Top Bottom