Elections 2010 Ukombozi wa Zanzibar ni kitendawili tega.

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,233
8,779
Na. B.OLE,

Baada ya kumaliza kwa sakata la uchaguzi Visiwani kinachoendelea sasa ni mdolongo wa kazi unaowakabili watendaji wa Serikali hasa Rais pamoja na makamo wake ambapo kwa mara ya kwanza Zanzibar itakuwa na makamo wawili na mmoja wao ni kutoka chama cha upinzani.

Licha ya kumaliza kwa uchaguzi ambao kwa muono wangu mimi binafsi ulijaa usanii kama chaguzi nyengine zilizopita, lililokosekana na ambalo mpaka leo hii tunajivunia ni kutokupigwa,kunyanyaswa na kudhalilishwa kwa Wananchi wasio na hatia, kwa muono wangu hili ni jambo la kushukuriwa kabisa na kupongezwa na kila mpenda amani.


Ama kuhusu matokeo halali ya uchaguzi hapa kila Mzanzibar anaelewa na mpaka Rais wetu anaetuongoza anajua ni nini kilipangwa na kutendeka katika uchaguzi uliopita. Hata hivyo hatuna budi kwa Wazalendo wa kizanzibar kujifunza kutokana na uchaguzi uliopita kwani kuna funzo kubwa la kudhingatia katika hilo.

Hata hivyo hapana budi kwa Wazanzibar wote wale wa chama cha C.C.M na C.U.F kumpongeza Maalim Seif kutokana na hekima na busara alizochukua kuiepusha Zanzibar na janga zito ambalo tayari lilikuwa limeshaandaliwa na wenzetu wasiopenda maendeleo ya Wazanzibar.


Maalim Seif aliwathibitishia Wazanzibar kwa mara nyengine tena kwamba yeye yupo kwa ajili ya maendeleo ya wote na kuinusuru Zanzibar na Wazanzibar wote bila kubagua, hilo ndio lengo na madhumuni yake. Cheo ni baadae lakini kwanza ni usalama wa Raia na nchi kwa jumla.


Kukubali kwamba ameshindwa na huku kila moja wetu akijua kwamba yeye ndie mshindi, lakini yote hayo hakuyapa kipaumbele, kwanza alihakikisha kwamba amani na utulivu ndio unaochukua nafasi yake Visiwani.Nafikiria hii ndio falisafa kwa Mwanasiasa wa kweli anaejua ni nini anafanya,umuhimu na wajibu wake kwa jamii iliomzunguka.


Jambo moja ambalo nilipata funzo katika uchaguzi uliopita ni zile kauli mbiu za baadhi ya chama na Wanachama wao kutangaziwa matokeo na kuhakishiwa kwamba kwa vyovyote vile itakavyokuwa Rais lazima atakuwa ni fulani na hata kama yeye mwenyewe hatojipigia kura basi sisi kutokana na nguvu zetu tutamuweka.


Suala langu ni kwamba kuna haja gani ya kufanyika uchaguzi wakati Rais ameshajulikana ? Ni vizuri tu kwamba zile gharama zilizotumika katika uchaguzi kuingizwa katika huduma za jamii kama vile hospitali na mashuleni kuliko kuzipoteza kwa ajili ya uchaguzi ambao tayari Rais ameshachaguliwa na pia Wabunge na Wawakilishi wake wanajulikana.


Lakushangaza zaidi ni kwamba matokeo yote yanapangwa na Watawala na Wakoloni wa Tanganyika na huku Zanzibar yanaletwa kwenye kapu ikiwa Wazanzibar watayakubali au watayakataa hilo sio tatizo kwao. Nasema hapa pana siri kubwa sana,hasa kwa wale Wazanzibar ambao hadi leo hii hawajaamka bado wanakasumba na tope za macho.

Fikra zangu zinalenga moja kwa moja katika suala zima la Muungano kwamba wenzetu wa upande wa pili wanafaidika sana na hii hali iliopo ya Muungano hewa. Kwa nini waing'ang'anie Zanzibar kwa bei yeyote ile hata ikibidi damu imwagike basi hapana budi, hivi Mkapa na gurupu lake inamhusu nini Zanzibar ?

Haya yote ni maendelezo na ubabe wa ukoloni mambo leo ambao hauna nafasi tena katika jamii ya leo.

Ushahidi ni kwamba iweje Serikali ya Tanganyika isimame kidete kuwanyima Wazanzibar uhuru wao wa kujiongoza wenyewe ?

Kwani nini wapuuze uamuzi na matwakwa ya Wazanzibar hadi kufikia kupanga mpango mkubwa wa Mapinduzi pindipo akitangaziwa mtu mwengine zidi wa yule wanaemtaka ? Ni kweli Rais wa kupangiwa na watu fulani kutoka Tanganyika tena kwa mtutu wa bunduki ataleta maendeleo yanayotakiwa na Wazanzibar ?

Jee kama hatukufikia kule tunako taka nani wakulaumiwa ?Tumevumilia vya kutosha lengo letu Wazanzibar ni maendeleo na kujiongoza wenyewe na wakati sasa umefika wa kufanya hivyo.

Wazanzibar natakawa niweke wazi na hili lichukuliwe kama vile ni usia kwetu kwamba "Ukombozi wa Zanzibar ni mgumu kuliko ule wa ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano." Sote tulishuhudia ulinzi mzito wakati wa kukaribia uchaguzi, majeshi yaliletwa kutoka Tanganyika kwa mpango maalum huku tukijuwa kwamba Wazanzibar wenyewe tumeshapatana na wala hatuna ugomvi wakupatiwa ulinzi wa Jeshi kutoka Tanganyika, imani yangu ni kwamba hata Polisi wetu wangeliweza kutoa ulinzi unaohitajika siku ya uchaguzi kwani uchaguzi ni demokrasia na sio vita.

Kwa wale wasio elewa ni kwamba Zanzibar mpaka hivi sasa hatuna Nchi kinachojaribu kufanyikana ni kuzibwa macho Wazanzibar toune bado Visiwa vyetu tunavyo lakini ukweli wa mambo sivyo ulivyo.

Kilichobakia ni kujikongoja lakini ugonjwa tulionao ni mkubwa na kama hatukupata matibabu yenye uhakika ni dhahiri kwamba tutaiaga dunia na kuanza kuishi maisha mengine ya kuzimu. Wazanzibar kwa mara ya mwanzo nimeshuhudia wakiungana na kuitetea Nchi yao kwa njia demokrasia lakini wamepigwa tena pute, tukumbuke kwamba huu sio wakati tena wakulumbana na kulaumiana kwani Wazanzibar walio wengi wameitikia mbiu ya mgambo ambayo siku zote ikilia huwa na jambo.



Nimalizee kwa kusema kwamba kwale wana Ukombozi lazima wafikirie mbinu nyengine mbadala kwani sioni ya kuwa iko siku Mzanzibar atakata pingu za kutawaliwa kirahisi kama wengi wetu tunavyofikiria na kwamba kila mmoja wetu ajihisi kwamba yuko huru na kuishi kwa mwevuli wa demokrasia ambayo wahusika wenyewe hawajui hata tafsiri yake ni nini.


Kinyume chake ni kwamba tukubalini kuwatii wakoloni wetu wakamilishe matakwa yao kwa Zanzibar ambapo kwa asilimia 80% wameshafanikiwa kututeka na kuiteka nchi yetu.
 
Back
Top Bottom