Uko kwenye ndoa zaidi ya miaka 5?naomba ushauri.

yaani wewe nasubiri urudi kutuambia unajuta kwenda kwa huyo mwanamke wa pili rasmi

utamu upo ukiwa unaiba ila ukiamua kuingia mojamoja wengi huwa wanajuta tabia ya mkeo ni wewe ndo umemfanya awe hivyo, lazima alikupenda sana na kukuamini na ki saikolojia uamuazi wako wakuiba nje na kuwa na mwanamke mwingine umemuaffect labda hata kiakili na zaidi.

mimi kama mwanamke nataka nikuambie ukweli, shame on you kwa nini ulimuoa kama ulitaka kwenda kuiba nje na ndoa yako hata hukusubiri miaka iende usingizie labda awezi kazi chumbani etc

tamaa yako itakupeleka kubaya huyo wa pili unaweza kuta atakuwa sumu kwako, anza kuishi nae basi uone itakuwaje utakoma na kujuta na nitafurahi yakikukuta haya wala sikuonei huruma. ungekaa chini na kumfungulia mkeo tu zipu yako basi usingepitia haya.

eehh kwani lazima wanenu wakutane? mwache nae awe na uamuzi wewe mwizi then unataka lazimisha mengine na yeye ndie aliyebeba mtoto miezi 9.

haya nenda kwa hawala wako si ndo maana umekuja kuuliza humu ili tukuambie hivyo? eeehhh nenda na utaona mkeo wa ndoa anaishi kwa raha na hatakuwa na matatizo ya kuumwa kichwa wala kutoangalia wanawe vizuri. wewe ndio kizuio hapo ondoka mwanamke apendeze apendeke. na huko unakoenda uende kuzeeka haraka na kuwaaa buzi au jinga la ndani wakati akienda kulala na wanaume nje, na kukutukana juu.

umeniuzi na swali lako unadhani wanawake ni mipira piga huku na kule na hawaumii rohoni?
 
Mengi yamesemwa na naomba nikiri kwamba JF ni kisiwa cha hekima................
labda tu niseme kwamba tatizo kubwa hapo ni mwanaume, pale ndoa inaposhambuliwa na vrusi vya uzinzi, kamwe haiwezi kuwa salama. Sasa huyu mume kafanya zinaa na ushahidi upo (Mtoto) hakuna mwanamke anayeweza kukubali kuwa mjinga kiasi hicho. Mwanaume azae huko, bado aendelee kufanya ngono na huyo mzazi mwenzie..................Labda kama itakuwa ni ndoa ya Mitala, lakini kama ni ndoa ya mke mmoja (Kanisani?) hilo haliwezi kuwa sahihi.

Hapo inahitajika busara ya mwanamke, kama ana nia ya kuendelea na hiyo ndoa kama ameichoka na haitaki tena, ni vyema wakaivunja na na kila mtu akashika hamsini zake..........Ku-revange haisadii sana sana itawaletea maradhi ya ukimwi na kuwaacha watoto wateseke.
 
Salaam wakuu,
Hii ndoa ina miaka 7,watoto 3.
Tatizo la kibinadamu-kama walivyo baadhi ya binadamu wengine,bwana akapata mpenzi,akazaa nae.
Akawa akijitahidi kutimiza mapenzi sehemu zote 2 na matumizi nyumbani, lakini baada ya kujulikana siri , mke wa ndoa akazua vita kali na akaamua kuingia kanisa la wokovu.
Mapenzi yakaporomoka kwa mke wa ndoa.Mama wa ndoa muda mwingi akaanza kuuweka kwenye hilo kanisa na uhusiano na familia ya mme na yake umepungua zaidi ya asilimia 70.
Mme halali nje ya nyumba yake. Lakini mapenzi anafanya kote.Wake wote wana pesa za kujitosha.
Shida ni moja tu,mama wa ndoa hana muda wa kushughulikia watoto, wala nyumba yake na wala hataki hawa watoto wake wajuane na mtoto wa bi mdogo.
Katika kukosa amani katika nyumba yao,mama wa ndoa akaanza kutembea na ndugu wa karibu na mume na siku walipokuwa na tafrani akamwambia mumewe kuwa ana revenge.
kwa sababu hii nauliza kiukweli tu,kama mume anahitaji kuishi humu duniani afanyeje mkewe wa ndoa akitaka penzi?atembee nae kwa condom au wakapime kila mara akimtaka au amuache-divorce au separation maana yeye anajijua kuwa ana makosa na anakubali, lakini adhabu yake isiwe kuikubali revenge na ategemee kifo cha ukimwi.?
Asante.

Dah! Swali zuri sana hili...Ila sasa huwa linaulizwa too late! Angetakiwa ajiulize hili swali the minute he got his eyes set on the nyumba ndogo (always don't ever forget to ask yourself this..)
Tel him he got this coming and has no one to blame...
 
Always what goes around comes around,raha zaidi unakuta huyo anayemtuliza waifu wako yuko vzr kwny mechi kuliko wewe,yaani hapo waifu wako alipo anasema sijui nilikuwa wapi sikuzote naaumiza roho kumbe kuna watu wazuri na wabunifu kuliko wewe kiruka njia, mbona poleeeeeeee!
 
Kwa kuwa zinaa imeingia,na maelewano hakuna,bora watengane.. Waende kwenye vyombo husika,watengane...

Kwa kufanya hivyo ibilisi atakuwa ameshinda kwani hiyo ndio nia yake, tumepewa utashi na tumeumbiwa msamaha ili tumshinde shetani.
Ushauri wangu:
  • Mume amuombe msamaha mkewe
  • Mke amuombe msamaha mumewe
  • Wote wawili watubu dhambi hiyo kwa Mwenyezi Mungu
  • Mume atambulishe watoto wa nje ya ndoa kwenye familia yake na asitishe mahusiano na huyo mwanamke, mke asitishe mahusiano na huyo ndugu wa mume
  • Wajenge nyumba yao upya.
Ndoa is a scared vow.

Pamoja sana.
 
The wholly book of Quran kinasema "MZINIFU HUZINIWA''. Mzinifu mwanamume au mwanamke huziniwa pia mwenza wake. Sasa jipime wewe unazini? basi jua kuwa nyumbani kwako kwaziniwa.

Wanaume wengi tunadhani kuwa tuna haki ya kufanya uzinifu, haki ambayo wake zetu hawapaswi kuwa nayo. That is very wrong mentality. Mimi nakushangaa sana ndugu yangu, Mungu amekupenda sana, amekupa mke mwema hayawi ya yote akakujalia watoto 3 maridhawa, wataka nini nje ya ndoa. I urge you to be focused, think about your present and future life for your lovely family in general and your childern in particular. Mawazo yako finyu sana unapodhani kuwa mkeo anaweza kukuletea maradhi hivyo unajaribu kutaka kutumia kinga lakini unasahau kuwa wewe unafanya uasherati nje ya ndoa unashindwa kufikiria kuwa huyo wa nje anaweza kuwa anakazwa na mwa/wanaume wengine na akaweza kukuletea wewe maradhi na kumwambukiza masikini mkeo.
Uzoefu na utafiti usio rasmi waonesha kwamba sababu kubwa ya wanandoa wa kike kwenda nje ya ndoa ni kwa waume zao kutokuwa waaminifu ingawa hawapaswi kufanya kisasa lakini wao ni binadamu pia wana extent of tolerance. Na ukiona mkeo anajua kuwa wewe unamahusiano ya nje na hakubughuzi basi kuwa mwangalifu sana kwakuwa na yeye atakuwa anavinjari pahala pengine.

Ushauri kwako wewe mzinifu mwanaume pasi na sababu ya msingi ni kuwa rudi kwa Mola wako, tubu kikwelikweli na Mungu anamjua anayetubu kikwelikweli. Mjengee matumaini mkeo kuwa ilikuwa ni bahati mbaya Ibilisi tu alipitia na sasa umerudi kwenye mstari namuombe mkeo muishi kama zamani. Wake zetu ni watu wazuri sana, wanatupenda sana na dhidi ya yote ni wepesi kutusamehe. mweleze hayo maneno matamu kama unauwezo nje ya pahala unapoishi somewhere kama uko Dar basi iwe in one of the nice hotel possibly along the beach kama unauwezo na unapomueleza hayo huku ukimpiga magoli ya uhakika na ukilia juu ya kifua chake, atakusamehe tu. Ondoa mentality kuwa yeye ndo mwenye makosa. Wake zetu hawa wako very delicate let us handle them with great care and respect. They real love once they are loved. Achana naye huyo mshamba wa nje na wakulaumiwa ni ndugu zako waliokubali kutembea na mkeo hali wakijua ni mkeo. Remember that you are the driving-force behind your wife's unlawful-actions. Take your responsibility and acknowledge your wrong-doing as a responsible husband and a father and make the right difficulty decisions for the future betterment and on favour of your lovely family. KOSA NI KURUDIA KOSA, PLEASE MAKE YOUR WIFE PROUD OF YOU AS SHE DESERVES BEST OUT OF YOU.

Salaam wakuu,
Hii ndoa ina miaka 7,watoto 3.
Tatizo la kibinadamu-kama walivyo baadhi ya binadamu wengine,bwana akapata mpenzi,akazaa nae.
Akawa akijitahidi kutimiza mapenzi sehemu zote 2 na matumizi nyumbani, lakini baada ya kujulikana siri , mke wa ndoa akazua vita kali na akaamua kuingia kanisa la wokovu.
Mapenzi yakaporomoka kwa mke wa ndoa.Mama wa ndoa muda mwingi akaanza kuuweka kwenye hilo kanisa na uhusiano na familia ya mme na yake umepungua zaidi ya asilimia 70.
Mme halali nje ya nyumba yake. Lakini mapenzi anafanya kote.Wake wote wana pesa za kujitosha.
Shida ni moja tu,mama wa ndoa hana muda wa kushughulikia watoto, wala nyumba yake na wala hataki hawa watoto wake wajuane na mtoto wa bi mdogo.
Katika kukosa amani katika nyumba yao,mama wa ndoa akaanza kutembea na ndugu wa karibu na mume na siku walipokuwa na tafrani akamwambia mumewe kuwa ana revenge.
kwa sababu hii nauliza kiukweli tu,kama mume anahitaji kuishi humu duniani afanyeje mkewe wa ndoa akitaka penzi?atembee nae kwa condom au wakapime kila mara akimtaka au amuache-divorce au separation maana yeye anajijua kuwa ana makosa na anakubali, lakini adhabu yake isiwe kuikubali revenge na ategemee kifo cha ukimwi.?
Asante.
 
Eti ategemee kifo cha ukimwi..... kwani alipokuwa anatembea na yule mdada wa nje mpaka mke akajua alitegemea nini, amemfrastrate mama wa watu mpaka akachanganyikiwa, na hayo yote anafanya sababu ya stress zimesongamana ndani ya akili yake,na wanawake wengi waaminifu sana hawana access ya kukutana na wanaume wengine yaani bar kwa mfano, maofisini au mahala pengine, wenyewe ni mulemule ndani,either houseboy, mlinzi ama hata ndugu coz tangu mwanzo hakupenda hiyo tabia, na sasa anaona akienda na watu wengine watamwona muhuni kwa hiyo anajibana humohumo karibu

wanaume mjue revenge ya mwanamke huwa ni mbaya sanasana hasa akiwa na hasira zilizojirundika siku na siku, akae na mkewe wote waachane na watu walee familia na kama mnaona mapenzi yameisha kabisa kabisa basi hamna budi kuachana,ambayo mie sioni kama ni suluhisho,Mungu hapendi kuachana, rekebisheni tu makosa yenu
 
Wanaume bana, mkewe angekua hazai angesema natafuta mtoto..........mkewe anazaa sasa nje unatafuta nini kama sio tamaa. Wacha niwakumbushe tu kua.........tamaa mbele, mauti nyuma. Aah mnanichosha kweli.
 
Wanawake ni watu wa msamaha... sijuhi mwanamke mjinga uvunja ndoa yake mwenyewe na bla bla bla kibao za kumnyanyasa mwanamke kijinsia.

Twende kwenye mada; wewe una makosa mengi tu na wala mkeo hakuwa na sababu yeyote ya kukusamehe. Kwanza umetembea nje ya ndoa na kithibitisho ni mtoto ulozaa. Sawa ningekuwa mkeo labda nasema tena labda ningekusamehe baada ya miaka kadhaa ya kuishi na hasira kichwani mwangu kila nikikumbuka kuwa umezini na una mtoto nje ya ndoa.

Ila kwa nini basi hustahili msamaha; kwa kuwa uhitaji kusamehewa kwani wewe si kuwa unajuatia kosa lako bali huoni kama umekosea. Kwa nini nasema hivyo; kwa sababu mwenyewe umekiri hapa kuwa unaendelea kuzini na huyo hawara yako. Masamaha wanapewa wale wanaotubu na kukusudia kuacha wewe huna kusudi la kuacha.
Na soon utaongeza mtoto mwingine nje ya ndoa yako. Wewe unadhani huyo kimada hana akili, nia yake ni kukuteka jumla na maugomvi ya ndoa yako kwake ni sherehe.

Naona umekuja kutafuta jibu la kuku suport na uzinzi unaoendelea kuutenda. Kumbuka msahara wa dhambi ni mauti.

Najaribu kufikiri; hivi wababa wanaozaa nje ya ndoa wana nafasi gani katika malezi ya watoto wao?... Kwa maneno mengine unaweza kuwakanya watoto wako waache kuwa mcharuko wakati wewe una watoto nje ya ndoa?
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
hizi ndoa hizi, aaaarrrrrrrrrrrrrrrrrrr

makosa ni ya mwanaume ameharibu yeye na atafute njia ya kutengeneza.

ni vema amrudie muumba, kutubu na kuacha zinaa

akae na mkeo amwombee msamaha
 
Wanawake ni watu wa msamaha... sijuhi mwanamke mjinga uvunja ndoa yake mwenyewe na bla bla bla kibao za kumnyanyasa mwanamke kijinsia.

Twende kwenye mada; wewe una makosa mengi tu na wala mkeo hakuwa na sababu yeyote ya kukusamehe. Kwanza umetembea nje ya ndoa na kithibitisho ni mtoto ulozaa. Sawa ningekuwa mkeo labda nasema tena labda ningekusamehe baada ya miaka kadhaa ya kuishi na hasira kichwani mwangu kila nikikumbuka kuwa umezini na una mtoto nje ya ndoa.

Ila kwa nini basi hustahili msamaha; kwa kuwa uhitaji kusamehewa kwani wewe si kuwa unajuatia kosa lako bali huoni kama umekosea. Kwa nini nasema hivyo; kwa sababu mwenyewe umekiri hapa kuwa unaendelea kuzini na huyo hawara yako. Masamaha wanapewa wale wanaotubu na kukusudia kuacha wewe huna kusudi la kuacha. Na soon utaongeza mtoto mwingine nje ya ndoa yako. Wewe unadhani huyo kimada hana akili, nia yake ni kukuteka jumla na maugomvi ya ndoa yako kwake ni sherehe.

Naona umekuja kutafuta jibu la kuku suport na uzinzi unaoendelea kuutenda. Kumbuka msahara wa dhambi ni mauti.

Najaribu kufikiri; hivi wababa wanaozaa nje ya ndoa wana nafasi gani katika malezi ya watoto wao?... Kwa maneno mengine unaweza kuwakanya watoto wako waache kuwa mcharuko wakati wewe una watoto nje ya ndoa?

Tena asivyokua na haya............eti mkewe ndie atakaye mletea magonjwa.............Ahhh some pipo wanachefua kweli:smash::smash::smash::smash::smash:
 
Afu anasema mkewe hataki watoto wao wamjue mtoto wa nje. Si ajiulize ni kwa nini mkewe hataki. Anaona aibu ataanzia wapi kuwaambia watoto kuwa baba yenu ni mzinzi na hili ndo tunda la uzinzi wake. Au wewe mleta mada huoni aibu kuwambia watoto huyu mwanangu wa "nje"? Well unless hao watoto wako ni wadogo sana; kama ni wakubwa wataungana na mama yao kukuchukia.

Tena asivyokua na haya............eti mkewe ndie atakaye mletea magonjwa.............Ahhh some pipo wanachefua kweli:smash::smash::smash::smash::smash:
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Mwanaume kachefua ndoa yake mwenyewe. kuteleza kupo haswa kwetu sisi men lakini si kuchonga mzinga la sivyo hakuna mwanamke aliyeko ndani ya ndoa atakayekubali huo ufidhuli. tujue wanawake nao wana hisia jamani na wanafikiri kwanini tunataka kuwafanya kama wanyama? wanahitaji respect
 
Afu anasema mkewe hataki watoto wao wamjue mtoto wa nje. Si ajiulize ni kwa nini mkewe hataki. Anaona aibu ataanzia wapi kuwaambia watoto kuwa baba yenu ni mzinzi na hili ndo tunda la uzinzi wake. Au wewe mleta mada huoni aibu kuwambia watoto huyu mwanangu wa "nje"? Well unless hao watoto wako ni wadogo sana; kama ni wakubwa wataungana na mama yao kukuchukia.

Saa ingine mtu hata unashindwa kunashangaa kwani anatumia nini kuwaza???
 
Kwa wenye ndoa ni kumuomba MUngu anusuru hizi ndoa zetu kwani kwa sasa kuna ibilisi kila kona. Kuna hawa wanaojiita independent women na wanaosema hawana shida ya kuolewa; basi wao wako busy kutafuta waume za watu wa kuwapandikiza mbegu ili wawe single parents bila kujali kuwa wanabomoa ndoa za watu. Tena ukiwa na mume mwenye mvuto ndo kabisa u'r in trouble. Huyu kaka amekaa kuumiza kichwa wakati alo zaa nae kama anavyosema ana pesa (wale wale), yeye keshapata alichotaka na wala haikuwa bahati mbaya.

Saa ingine mtu hata unashindwa kunashangaa kwani anatumia nini kuwaza???
 
Anasali kanisa la wokovu halafu tena kaamua kurevenge kwa kutembea na ndugu wa mumewe! Hii kali wokovu utatoka wapi hapo.

Ila mumu ana makosa kama kweli anataka amani ndani ya ndoa yake arudi amuombee mkewe msamaha wa kweli then wakapime afya zao maisha yaendelee na aachane na nyumba ndogo.

Kama vipi, wanaona mambo ni magumu basi watengane
 
Mkewe kwa ufupi yuko frustrated. Na hawezi jua what will be next maana ameanza kwa kuokoka, kaona bado hajapata faraja, kaamua kutafuta na yeye wa kuzini nae, hatujuhi kama amepata faraja; hii ndoa kwa kifupi iko kwenye real trouble. Kwa kuwa jamaa ni chanzo atafute suluhu, ikiwemo kuachana na kimada wake na kumwangukia mkewe.

Kumuacha mke na kuoa kimada inaweza kuwa si maamuzi sahihi (sijipendelei) kwani mdada anayekubali kuzini na mume wa mtu anaweza kuwa na sifa za mke zaidi ya good sex partner??? Navyojua mimi ndoa ni zaidi ya sex.

Anasali kanisa la wokovu halafu tena kaamua kurevenge kwa kutembea na ndugu wa mumewe! Hii kali wokovu utatoka wapi hapo.

Ila mumu ana makosa kama kweli anataka amani ndani ya ndoa yake arudi amuombee mkewe msamaha wa kweli then wakapime afya zao maisha yaendelee na aachane na nyumba ndogo.

Kama vipi, wanaona mambo ni magumu basi watengane
 
nimekuchukia sana japo sikujui, yani huna adabu wala aibu, roho yako mbaya sana wewe, we unajua mkeo ameumia kiasi gani mpaka akaamua kutembea na shemeji yake?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom