Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Ndugu yangu Mzee ES, nimeshaandika barua kwa wabunge wa chama chetu nikiwaomba angalau wa come up strongly on this issue.

Kwa kweli mimi bado nipo kwenye puzzle, viongozi wetu wanatoa wapi nguvu za kuwakemea wananchi kujichukulia sheria mkononi kama wao wenyewe na watoto wao wanafanya hichohicho? Inakuwaje viongozi hawana aibu kiasi hiki; ni vigumu kuamini kwamba hadi sasa Ditotupile hajajiuzulu anasubiri afukuzwe!? Kibaya zaidi, haonekani kujutia kitendo alichokifanya na baadhi ya vyombo vya habari vinataka watu wamhurumie Ditotupile na sio Mbonde! Nimesoma gazeti la Daily News linaongelea habari za watu kutoa machozi na kusisimka kwa kumhurumia Ditotupile! We are becoming not only unscrupulous but also unethical and inhumane.

Honestly, japokuwa kila mtu ana haki ya kutetewa, wanasheria walio ethical wangeogopa kusimama upande wa huyu bwana! Yes, they will get money, but at the peril of their moral conscience and public disreputation!

Bado ninaamini JK atakuwa firm kwenye hili japokuwa may be too late!

Mliopo nyumbani endeleeni kutupa habari as quick as possible ili tuwe pamoja katika kuona mwisho wa hili jambo.
 
Mimi nina wasiwasi hata na huyo Tibaigana!, kwani hata kauli zake zinatofautiana ,na inawezekana pia nao wanahusika ktk kuficha silaha iliyotumika kwenye mauaji.Kwanini Ditopile akimbilie kwa Tibaigana?Nyumbani kwake kumekuwa kituo cha Polisi? Ktk maelezo yote ya Tibaigana hakumtaja abiria wa kike aliyekuwepo kwenye gari!,kuna sababu gani ya kumficha huyo Mama?Na kwa maelezo ya huyo huyo Tibaigana eti inaelekea risasi ilipigwa kwa bahati mbaya.Kuna kizungumkuti hapa!kulikuwa na mkutano mkubwa kabla ya kumkabidhi Ditopile kwenye vyombo vya Dola!
 
Maskini Braza Dito!
Hawa jamaa (JK na Dito) walikuwa bado washikaji au walishatofautiana pale Dito aliponyimwa U-Makamba (Katibu Mkuu wa CCM)? Kama alikuwa anakwenda Mlingotini (alikuwa akielekea Bagamoyo...) kurekebisha mambo halafu ikawa kinyume, basi ni noma kwelikweli!

Tusubiri baadaye kidogo...

JK kumzungumzia Ditopile leo

2006-11-07 15:28:03
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambayo ipo katika mtego mkali wa kiongozi wake wa Mkoa Kapteni Mstaafu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri kumtwanga risasi raia aliye dereva wa daladala, inatarajiwa kutoa tamko lake rasmi juu ya kadhia hiyo leo.

Taarifa za kuaminika zilizopatikana mapema saa 4:00 asubuhi kabla hatujaenda mitamboni, zinasema kwamba huenda serikali ikatoa uamuzi mzito kwa Kapteni Ditopile anayetajwa na baadhi ya marafiki zake kama Brother Dito au Kaka Dito, ambaye inasemekana kuwa kuwepo kwake Dar es salaam pia kuna walakini.

Taarifa zaidi zinasema kwamba tamko hilo huenda akalitoa Rais mwenyewe ambaye kwa sasa yupo ziarani nchini Korea Kusini au Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, ambaye hivi sasa yuko kwenye bunge linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

Kapteni Ditopile ambaye jana alisomewa mashtaka ya mauaji na kutakiwa kutokujibu chochote pale kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inadaiwa na chanzo cha kuaminika kuwa aliondoka kwenye kituo chake cha kazi bila ruhusa ya Mkuu wake wa kazi.

SOURCE: Alasiri
 
Huyu jamaa atafungwa tu,he has been charged with murder na adhabu yake ni kifo.Raisi hawezi kufanya kitu chochote hata kama angetaka,hii kesi ni kubwa sana,na hata IGP,Mwanasheria Mkuu na washauri wake wote watamwambia akae nayo mbali,na yeye mwenyewe anajua.Ingekuwa aliua nyumbani kwake au hata kwenye bar,ingeweza kurekebishwa lakini hii hairekebishiki,huyu kaua raia mlalahoi,aliyekua kazini kwake mbele ya umati wa watu,hio tu ni jeuri ambayo itamkera hata mtu anayetaka kumsaidia.
JK anajali sana kupendwa na wananchi,hawezi kuwa-let down kwa sababu ya best man wake.Brother Dito kishajitoa kafara mwenyewe.
Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba hata-nyongwa,but he will be found guilty without a shadow of a doubt.Sasa labda wabongo tulete 'ubongo' wetu na wale mashahidi wote wakatiwe mkwanja na waseme kuwa dereva wa daladala alitoa spana na kutaka kumvamia Dito,nae kwa kujihami akatoa bastola....hii ni bongo bwana,anything can happen.Lakini as far as higher authority goes,he is doomed! Sasa hivi kwanza wote watamkimbia,maana kishakuwa muuaji,nani anataka kuonekana na muuaji? Watamtembelea gerezani mara moja au mbili kuondoa lawama,then kwisha,anabaki yeye na familia yake na marafiki zake wa karibu sana.
Ndugu zangu,ukitoa roho ya binadamu kama alivyofanya huyu bwana hustahili hata kusema eti innocent until proven guilty.

Wale wakina Nguza na watoto wake wamefungwa maisha kwa sababu ni walalahoi na sio raia kwa kesi ambayo hata hao victims wenyewe walikuwa hawaielewi,pamoja Nguza kusema hana 'nguvu za kiume' lakini bado wakafungwa maisha,mtoto wake wa miaka 17 nae kafungwa maisha...tuone sasa na hii.Hakuna cha u-best man,wala nini sasa hivi,ni yeye na msaafu wake tu.
Huu ndio mfano wa viongozi tulionao kweli? Huyu ni mtu ambye kakabidhiwa mkoa autawale,issue ndogo kama hio anaimaliza kwa mtutu?
Huyo ni dereva wa daladala tu kamchomekea,je angekuwa kazikwa pesa,au mtu katembea na mkewe ingekuwaje?
 
Halafu watu wasisahau kuwa Dito hakuwa dereva!!! Dereva wake alienda kuzungumza na dereva mwenzie na nusura wayamalize hadi pale mtu mkubwa (bila ya shaka kujipatia ujiko kwa huyo mmama) akaamua na yeye kwenda kutilia mkazo.
 
kwani ni nani anatia saini yake ya mwisho mtu auawe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo kama ni JK na tayari mmeishasema kuwa alikuwa best man wake

sasa hapo mnasemaje!!

JK anajua kuwa kura atapta hana shida lakini akimuua rafiki yake atampata wapi?
 
Wanabodi,

Naona magazeti yameanza kumlabel Dito kama victim katika hii kesi , jamani tusisahau victim ni dereva wa dala dala . Pili hili suala la JK kusubiri masaa 72 bila ya kumfukuza huyu bwana kazi ni jambo la kusikitisha sana . Hii inaonyesha kabisa serikali ya JK imezoea KUDESA haiwezi kutoa maamuzi bila ya kupata mlungula nitaelezea ...

Serikali ya JK imesubiri siku tatu ili kujua Reaction ya wananchi , then sasa ndio wanasema JK atalizungumzia hili suala ,Hii inaonyesha dhahiri ya kuwa hawana princible or value that they are standing for instead they are waiting for public opinions . Hii ni hatari sana kwa taifa ni lazima tuwe na viongozi ambao wana principle ambazo zinawaongoza katika maamuzi yao na sio kusubiri watu wanalionaje hili jambo .

Mimi nataka kwanza tuijadili hii serikali ya JK na kigugumizi chake katika kutoa maamuzi . Jee ni sheria gani za nchi yetu zimekiukwa ? na kama kuna sheria zimekiukwa then who is to blame ? Suala la kusema JK hayupo nyumbani sio excuse na wala halina nafasi katika bodi kama hii iliyojaa watu wenye kuona mbali.
 
Siamini JK anaweza kwenda kinyume na sheria. Na ujue kuwa hata yeye (JK) akichemka sheria itambana.

Sipendi na wala sitarajii kuamini kuwa anaweza kuweka ushikaji mbele na kusahau maslahi ya taifa.

Kauli za Tibaigana japo zinatia wasiwasi lakini mwelekeo wa issue hii unaonesha bayana hakuna tundu dogo la huyu ngamia kupenya.

Bagamoyo alikokuwa akienda huenda pakawa hapakumfaa alilazimisha. Bahati mbaya Babu alishafariki, angemwondolea nuksi hata huko mahabusi.

Nitafurahi saaaaana akihukumiwa kukaa pamoja na mshkaji wake Zombe ili walonge kujua ni upuuzi gani uliwapelekea kufanya yale walofanya.

Nshasema, sisi tumezoea kuchokozwa tunavumilia kwakuwa tunajua kuna sheria. Huyu kashindwa kujua kuwa masikini nae mtu japokuwa hana kitu, wacha avune matunda ya jasho lake.

Ila ni bonge la anguko... kama asemavyo kichuguu! Yani kutoka Mkuu wa mkoa hadi mfungwa? Hii imekaa vibaya! Kilimanjaro imekuwa kichuguu within a minute!

Wengine watapata fundisho kwa ya Zombe na Dito (maybe).
 
JK amekubali kujiuzulu kwa Ditopile.

amesema vizuri sana. Na si kama Mkapa aliyewahi kusema anasikitika kujiuzulu kwa mmoja wa mawaziri wake!

sasa sheria ifuate mkondo wake. Je huyo kijana wa Mungai naye kakamatwa?
 
Haha, kumbe mkuyuga umefatilia?

Haikuwa na jinsi, kwa kosa hili ilikuwa bayana Dito asingekuwa mkuu wa mkoa tena. Hilo halikwepeki. Lakini anguko lake ni kubwa hadi sielewi...
 
Hatimaye kile ambacho tumekuwa tukikipigia kelele kimefanyika. Ditopile amejiuzulu ukuu wa mkoa na rais amekubali barua yake ya kujiuzulu (hakuna jinsi nyingine).

Toka "Uhuru"

RAIS Jakaya Kikwete amekubali kujiuzulu kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya raia mjini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana usiku, Rais Kikwete amekubali ombi hilo kufuatia barua aliyoandikiwa na Ditopile Jumapili iliyopita, siku moja kabla ya kufikishwa mahakamani, akimuomba Rais akubali kujiuzulu kwake.

Anayetaka kutoa maoni piga simu: 206-337-0563 na maoni yako yatarushwa moja kwa moja kwenye KLH News na kusikika dunia nzima!! Zungumza kwa kifupi na kwa sauti ili usikike!!

M. M. Mwanakijiji
Host KLH News
email: mwanakijiji@journalist.com, mwanakjj@hotmail.com
 
Bravo Mwanakijiji!

Baada ya kujaribu ku-reach out kwa Mzee JK, kwa njia za nyuma Braza Dito akaambiwa kuwa not on this one, na akaambiwa andika barua ya kujiuzulu haraka!

Great sasa tunataka kuona the next step, nothing but sheria kufuata mkondo wake, na huyu mzee apande ngarandinga!
 
Kwa hiyo atashtakiwa pia kwa kuzembea na kupoteza silaha??

Ditopile's gun goes missing
FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Wednesday,November 08, 2006 @00:08

JK accepts his resignation

THE pistol allegedly used by the Tabora Regional Commissioner, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, to kill a commuter bus driver in Dar es Salaam last Saturday, was lost after the shooting, the 'Daily News' has learnt.

Ditopile, who is former Dar es Salaam, Lindi and Coast regional commissioner, appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court on Monday, charged with the murder of a daladala driver, Hassan Mbonde (33).

Commander of the Dar es Salaam Special Police Zone Alfred Tibaigana told the 'Daily News' in the city yesterday that according to the accused, the firearm, loaded with five rounds of ammunition, got lost when a mob attacked him (Ditopile) immediately after the incident.

Mr Tibaigana said the accused told the police that a group of people attacked him after the shooting, wrestling the weapon from his hands. The RC also allegedly sustained injuries on his left arm. He said police were still searching for the gun.

Meanwhile, President Jakaya Kikwete has accepted the immediate resignation of Mr Ukiwaona Ditopile Mzuzuri as Tabora Regional Commissioner, who is currently facing murder charges.

A brief statement issued by State House yesterday evening said the president had accepted Ditopile's resignation offer filed yesterday.

The president said in the communique that Ditopile's resignation was the best option in the circumstances, and that, it had manifested his steadfast patriotism even in dark moments.

He added: "Your resignation brings honour to our nation, which adheres to the rule of law". CCM Secretary-General Yusuf Makamba told the 'Daily News' later that Ditopile did not hold any post on the ruling party.

At the Kisutu Resident Magistrate's Court on Monday; Ditopile was not allowed to enter any plea to the charge because his case would be tried by the High Court. Principal Resident Magistrate Michael Luguru, who is conducting a preliminary inquiry on the case, remanded him until November 20, this year.

It was alleged before the killing that the driver of the commuter bus, plying between Ubungo and Tegeta, slammed into Ditopile's vehicle from the back. At the time of the accident, the RC's vehicle was being driven by Mr Nassor Mohammed (42), and was heading to Bagamoyo.
 
Ndugu zangu na jamaa wote mnaoishi nchi za nje....
Kuna hoja hapa imetolewa na mshikaji wangu wa karibu kuwa tuchange nguvu zetu kwa familia ya marehemu kuonyesha kuwa tupo nao bega kwa bega dhidi ya hao watawala.
Moja ni kumsaidia mke na watoto wawili aliowaacha marehemu kwa kutoa michango yetu ya fedha kupitia jumuiya zetu popote pale tulipo kisha tuwasiliane na mtu kama Michuziline ambaye atafuatilia mpango wa Mama mjane kuwa na account huko Bongo ambayo tutaweza ku wire michango yetu.
Binafsi nimeafiki jambo hili nadhani lina maana kubwa zaidi kwa hao waliobaki ambao hawana njia ya kujiendeleza na maisha!

Mwasemaje?
 
niambieni detail.. I was thinking of helping in the legal costs.. lakini twaweza kuwasaidia wana familia pia... kama kuna mtu anaweza kuniunganisha na baba wa Marehemu nizungumze naye wakishakamilisha mipango nina uhakika tutaweza kuwasaidia... ni PM basi
 
mwanakijiji,
sasa kama ni michango ni vizuri iende kwa mke wa marehemu na si baba wa marehemu,
maana mke ndio analea watoto au inakuwaje hapo?
 
One thing for sure sasa hivi ni kwamba Mzee Dito, atakwenda jela hiyo haina ubishi kabisaaa, maana hata JK amenawa mikono, sasa kinachopiganiwa na wapambe wake ni muda atakaokaa gerezani ambalo tayari limeshaamuliwa litakuwa pale Morogoro, njiani kwenda Dodoma, ambalo katika awamu ya kwanza walikaa sana kina Seif Bakari,

Nasikia sasa unachezwa mchezo wa muda atakaokaa, na pia kutakuwa na msamaha wa rais, somehow somewhere, hiyo ninaamini kabisaaa, lakini angalau sheria itafanyika sio haba!
 
Back
Top Bottom