Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Someni gazeti la mwananchi, limeandika vizuri zaidi hii saga kuliko hiyo habari iliyopo kwa kiingereza kwenye Tzuk.net. Na-paste hapa for clarity purposes

Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji

Na Muhibu Said

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia bastola yake jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zinaeleza kuwa Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam kwa kumpiga risasi kichwani.Ditopile, anatuhumiwa kumuua dereva huyo juzi saa 2.30 usiku, katika njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.Gari hilo lililigonga gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Nassoro Mohamed (42), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo, mkoani Pwani.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.

Walisema wakati dereva huyo akiendelea kulikagua gari hilo, Ditopile naye alishuka na kuungana na dereva wake katika ukaguzi huo.Walisema baada ya kuona uharibifu huo, Ditopile, alimfuata marehemu na kumtaka ashuke katika gari alilokuwa akiliendesha ili aende kushuhudia uharibifu uliotokea na kisha waende polisi.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu, alimweleza Ditopile kuwa ajali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na kumwomba msamaha kwa tukio lililotokea.Walisema mkuu huyo wa mkoa, hakukubaliana na utetezi huo na badala yake aliendelea kumwamuru marehemu ashuke kwenye gari na kumtaka akaeleze maneno hayo polisi.

Mashuhuda hao, walisema marehemu alipoona Ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali, aliamua kufunga kioo cha gari kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo.Walisema kitendo hicho kilimuudhi Ditopile ambaye alichomoa bastola aliyokuwa nayo na kuanza kuitumia kugonga kwenye kioo cha gari la marehemu huku akimsisitiza kushuka katika gari.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu aligoma kutii amri hiyo ya Ditopile na ndipo alipomfyatulia risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha marehemu.Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya tukio hilo, alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeegemea kwenye kiti cha dereva huku damu na ubongo vikiwa vimetapakaa ndani ya gari alilokuwa akiliendesha.Tukio hilo lililozua hofu, lilisababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa watu, wakiwamo madereva na abiria waliokuwa wakisafiri katika njia hiyo, kutokana na mlio wa risasi.

Watu waliokuwa kwenye magari, walishuka na kuanza kukimbia ovyo katika sehemu mbalimbali wakidhani kuwa eneo hilo limevamiwa na majambazi.Watu pekee waliobaki katika eneo hilo, ni dereva anayedaiwa kuwa wa Ditopile na mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye anadaiwa kuwa alikuwa katika gari lililokuwa limembeba Ditopile.Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana.

Dakika chache baadaye, polisi waliobeba silaha wakiwa ndani ya magari matatu aina ya Lond Rover Defender, walifika katika eneo hilo.Akielezea tukio hilo, Kamishna Tibaigana, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika eneo hilo na gari lililombeba Ditopile, lilikuwa na abiria wawili; akiwamo Ditopile mwenyewe na mtu mwingine ambaye hajafahamika. Alisema wote walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo."Mara baada ya ajali hiyo kutokea, magari hayo yalisimama. Dereva Nassoro Mohamed alishuka na kwenda kuangalia gari lake ili kubaini lilivyoharibika/kugongwa, aliliona limepata madhara kidogo upande wa nyuma," alisema Kamishna Tibaigana na kuongeza:

"Wakati Nassoro Mohamed akiendelea kuangalia, alishuka mheshimiwa Kapteni Ukiwaona Ramadhani Ditopile Mzuzuri ili naye aende kuona uharibifu uliotokea. Baada ya kuona uharibifu uliotokea alimtaka dereva wa Isuzu Journey, Hassan Mbonde, ashuke ili naye aone uharibifu uliotokea kisha waende polisi kutoa taarifa."Dereva wa Isuzu Journey alikataa kushuka kwenye gari lake na badala yake alifunga kioo cha dirisha la mlango wake kisha alifunga mlango na ku-lock kwa ndani. Mheshimiwa Ditopile Mzuzuri baada ya kuona dereva amefunga mlango, alisogelea dirishani na kutoa bastola yake na kuanza kugonga dirisha kwa kutumia bastola yake, huku akimwamuru ashuke ndipo ghafla alifyatua risasi moja ambayo ilivunja kioo cha dirisha na kumjeruhi Hassan Mbonde kichwani na alifariki dunia papo hapo," alisema Tibaigana katika maelezo yake kwa waandishi wa habari.

Tibaigana, alisema baada ya tukio hilo, dereva Mohamed, aliendesha gari lake na kuondoka sehemu ya tukio akiwa na abiria wake wawili."Mtuhumiwa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri amekamatwa na anaendelea kuhojiwa. Pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Kamanda Tibaigana.Asubuhi jana, watu walimiminika katika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao juu ya jinsi walivyoshuhudia tukio hilo.Baadhi walisimulia kuwa katika tukio hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipiga risasi mbili ambapo moja ilimkosa marehemu na nyingine ndiyo ilimuua papo hapo.Daladala aliyokuwa akiendesha marehemu Mbonde ilikuwa imeegeshwa katika kituo hicho cha polisi na baada ya baadhi ya watu kutoa maelezo, walitakiwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Nyumbani kwa marehemu kulikuwa na watu wachache huku mvua ikiendelea kunyesha na wengi wao walikuwa wakijadili tukio hilo. Marehemu Mbonde ameacha watoto wadogo watatu."Hii inatakiwa Rais aunde Tume kama ilivyokuwa kwa Zombe, hivi hivi hakutakuwa na haki," alisema muombolezaji mmoja.Watu hao walishikwa na hasira na kutaka kuwavamia waandishi waliokuwa msibani hapo baada ya redio moja kutangaza kuwa marehemu alikufa katika ajali.

Habari zilizopatikana msibani hapo zilieleza kuwa marehemu Mbonde atazikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Kawe.
Enzi hizo JF ya moto kwelikweli
 
Rip jaman

h
 
Back
Top Bottom