Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Hii tabia ya "UMUNGU MTU" ndio kitu kinachoniudhi kwa viongozi wetu,ni lazima sasa Utawala wa sheria uchukue nafasi yake,haiwezekani kutoa maisha ya mtu kwa sababu ya kuharibu taa ya gari (prado) ambayo hata haizidi Tshs 30,000.Nimekwishasikia habari za watu kuua na baadaye unawaona kwenye mabaa na mabarabarani wakiwa huru,ati kwa sababu tu wana influence na watu waliopo madarakani!!Sasa hapa sheria ikipindwa tutapigana mawe,kama silaha wanapewa wenye uwezo tu!!Hainiingii akilini kuona mtu anatumia silaha kwenye mgogoro ambao unaweza kutatuliwa kwa mjadala.Hiyo ni kashfa na inabidi "AJIUZULU" Nyadhifa zote hata kama nae ni Mwanamtandao.Ni lazima sasa tujali Utawala wa Sheria,na sio kujiamulia mambo kama Gang Groups!!.
 
sidhani kama Ditopile alikuwa na nia ya kuua. Nadhani nia yake ilikuwa kuchimba mkwara, lakini bahati mbaya ajali ikatokea.

Sheria ikifuata mkondo wake, Ditopile anaweza kwenda jela kwa muda mrefu sana. Hta hivyo, Raisi Kikwete, kama rafiki mkubwa wa Ditopile, anaweza kumtoa jela kwa kutumia nguvu ya Msamaha wa Raisi.

Mnakumbuka yule Rubani aliyekamatwa na dhahabu Airport Darisalama? Raisi Mwinyi alikuja kumtoa gerezani.
 
This info is correct and has been on the radio/TV.Sasa tuangalie "cover up" iemisha anza.Kesho tutaambiwa nii BAHATI MBAYA
 
Ok! Habari iliyoandikwa na hilo gazeti haina uongo kama nilivyosikia kwa waliokuwepo, tena wanasema kuwa alitumia muda mrefu kumtishia dereva huyo na hiyo bastola, na wanasema kuwa hata baada ya kumuua aliokota kwanza ganda la risasi aliyoipiga na kuondoka taratibu,

basi lilikuwa na abiria kibao waliojionea kwa macho the whole sagga, damn Ditopile what were you thinking?! Yaani kwa sababu mtoto wa Rupia aliachiwa, Kinje aliachiwa, Aziz aliachiwa, Rajpa aliachiwa sasa na wewe unataka kufuata mkondo huo wa kufikiri utaachiwa?

Maan you are doooomed!, Siku zote nilikuwa ninampa ka-heshima fulani huyu mzee maana alimtoa jasho Mwalimu kule Kizota, lakini kumbe ni bomu! Wewe RC mzima unatoa bastola mbele ya wananchi nini maana yake kwamba sasa tuanze kuwa Texas, yaani kutoa tu bunduki kama vile wachunga ng'ombe, huyu afungwe maisha, maana hakuna excuse, tena Mzee JK hapa ndio the test ya urais wako, yaani hapa ni njia panda ndugu yangu wewe ni kuosha mikono tu, tena huyo Ditopile aende kule Keko msiamfanyie kama mtoto wa Rupia kumuweka kwa wahaini kwenye raha, aende kule atumie ndooo kama watu wote huko!
 
first things first!

The President should immediately relieve Mr. Mzuzuri of all his presidental titles effective immediately. Regardless of the outcome of the case, if it is established that Mr. Mzuzuri fired the deadly shot, from now on, he should not be appointed to any government post!!! infinitum!!

Mr. Mzuzuri should resign or forced to out from all other private capacities until his trial is over
 
Mimi ushauri wangu kwanza serikali iunde tume huru kuchunguza ili jambo na ikiwezekana familia ya marehemu ifanye mpango ipate Dokta binafsi atakefanya Autospy mwili wa marehemu ili tuweze kujua ni risasi ngapi zilipigwa ?

I think there is more to this story than what we have been told !
 
jamani... Mwananchi inasema hivi:

"Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana."

a. hakuna aliyemuona aliyepiga risasi?
b. Watu kugombea bunduki (kupoteza fingerprints)
c. Bunduki kutoweka

basically, watataka iwe kesi ya mazingira bila ushahidi wa silaha, alama za vidoel n.k!!! angalieni dereva wa Dito atabebeshwa msalaba!!!
 
Mwanakijiji,

What happened to you?, unataka kutueleza nini uhusiano wa hadithi yako na tukio la Ditopile kuua?
 
Ogah, sorry... sikutaka kupost hiyo... unajua mambo ya kucopy na kupaste... nilichotaka kuonesha ni kile kilichoandikwa kwenye "Mwananchi" Hiki ndicho nilichotaka kubandika

jamani... Mwananchi inasema hivi:

"Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana."

anatengenezewa mlango wa kutokea?

a. hakuna aliyemuona aliyepiga risasi?
b. Watu kugombea bunduki (kupoteza fingerprints)
c. Bunduki kutoweka

basically, watataka iwe kesi ya mazingira bila ushahidi wa silaha, alama za vidoel n.k!!! angalieni dereva wa Dito atabebeshwa msalaba!!!
 
Wazee hakuna aliyegombea bunduki, Ditopile alikwenda kwenye basi klilikuwa limejaa abiria na kuanza kumtisha dereva ashuke, huku abiria wakimshangilia dereva kuwa asitoke, the next thing Ditopile akapiga risasi moja iliyomfumua kichwa marehemu na kutoa ubongo pamoja na damu kibao kwenye basi hilo,

hakukuwa na mtu yoyote aliyegombea bunduki, wala kupotea fingerprints, tusianze kuigeuza hiii crime ambayo ni simple and clear kwa kila mtu aliyekuwepo!
 
Dito hapo kaharibu, after all yeye ni mjeshi kwa hiyo lazima anajua vyema kutumia silaha. For my opinion suala sio bahati mbaya ila ni uzembe. Hivyo sheria inatakiwa kuchukua mkondo wake ili iwe deterent kwa wengine wote, no one is above the law. May be inaweza kufufua na kesi za kina Kinje na wengineo.
 
Kuna wanasiasa wengi wamekuwa wanatembea na bastola na kuzitumia kutishia raia lakini serikali haijwahi kuwafungulia kesi zozote za attempted murder. Inawezekana kuwa Ditopile hakuwa na nia ya kuua, bali alitaka kumtishia tu lakini kwa bahati mbaya bunduki ikafyatuka. Ndiyo maana katika nchi nyingi duniani, ni kosda la attempted burder kumlenga mtu kwa bunduki ambayo iko loaded. Viongozi wetu pale wamekuwa wanafanya bastola kama toy la kutishia watu bila kuchukuliwa hatua yoyote.

(1) Miaka michache ilyopita mtoto wa Kingunge alitumia bastola ya baba yake kumtisha mtu kule Kinondoni lakini kesi hiyo ikaisha kienyeji tu.

(2) Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu pale Dar se salaam Didas Masuburi (sasa mbunge wet katika afrika ya mashariki) alitishia watu kwa bastola wakati wa kampeini za uchaguzi. Wakati huo akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Dar es Salaam aliingilia mkutano wa kampeini wa Dr Lamwai wakati huo akiwa NCCR-Mageuzi. Bwana huyu hakufunguliwa kesi yoyote na aliendelea na uongozi wake kama vile hakufanya lolote.


Kwa jumla rekodi ya Ditopile kama kiongozi nayo haikuwa nzuri na nashangaa kwa nini amekuwa madarakani muda mrefu hivyo. Amewahi kudai watu wa bara hawafai kugombea uongozi katika vitonmgoji vya Dar es Saalam kwa vile wao "ni wa kuja tu - Dar ina weneyewe". Miaka ya mwazoni mwa tisisni alishikwa ugoni pale Kinondoni, halafu akatoa maneno ya kashfa sana kwa mme halisi wa mwanamke aliyekuwa amekamatwa naye. Kuna upuuzi mweingi uliokwisha fanywa na bwana Ditopile bila kuchukuliwa hatua zozote. Ngoja tusbiri hatima yake katika skendo hili.

Kwa tukio kama hili hakutakiwa kuanza kubishana na dereva wa daladala. Yeye kama kiongozi angepiga simu polisi waje kupima uharibifu na kuachia vyombo vinavyohusika vifanye kazi yake. Lakini bwana huyu alitaka kuonyesha umbwamba.
 
Hii stori kwamba ni accident naishuku. Huwa unagonga dirisha na mtutu umelenga kichwa cha mtu?

Alichotakiwa kufanya (kama ilibidi) ni kupiga risasi matairi ili gari lisiondoke. Na angeweza kupiga simu (mobile) Polisi wakaja wakamkuta bado analinda dereva asiondoke.

Kila mtu, hata dereva wa daladala, ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Uhai wake ni dhamana kuu kutoka kwa Mungu. Haikubaliki RC kuua mtu kama kuku.

Augustine Moshi
 
Sheria za nchi yetu ziko very clear kuwa ajali za traffic hushughulikiwa na polisi wa traffic, sio RC kutoa bunduki na kumtishia a helpless dereva wa dala dala, na baadye kumuuua FULL STOP,

Ditopile na watakaomtetea wanataka kutuambia nini kuwa wenye uwezo wakipata ajali barabarani watoe bunduki na kuwaua wanyonge?

Mzee JK, ndugu yangu hapa sasa ndio njia panda ya urais wako, one mistake umekwisha tena huyu Ditopile ana kiburi sana huyu toka siku nyingi sasa lazima kiburi kiishe tena apelekwe Keko, kwa wazee kule aonje joto ya elimu dunia, maana asiyefunzwa na mama, hufunzwa na dunia yaani kule Keko!
 
ditopille chizi kwani hamjui,,,mpenda mademu nk alipofumaniwa maeneo ya upanga alijigamba kuwa ugoni si kosa kwa mwanaume lijali ,,,sasa atasemaje,,sasa fikiria aina ya mtu ambaye jk alitaka kumpa ukatibu mkuu wa ccm,,sasa tutawaamini vipi watu anaowateua,,,angalieni namna makamba anavyotumia ruzuku nono kununua wapinnzani...huu ni ubakaji kama ubakaji wowote...yetu macho ,,hapa hana namna zaidi ya kumtosa
 
Wewe mzee vipi? wewe umetumwa kuvuruga issue ya Ditopile wewe mzee huyo jaamaa ambaye uko obssesed naye sio news, the news ni Ditopile tena usianza mchezo wako wa kuharibu issue hiii hatutakuacha, yaani huyu rafiki yako Ditopile mliyekuwa mnakaaa naye kwenye vikao sasa atakiona cha moto,

au JK ataadhirika mtu mzima, tema ndugu yangu usituchokoze kwenye hili, tunataka kuona sheria inafuata mkondo wake ki-kweli kweli, usituletee ya tajiri hatuyataki hapa the news ni Ditopile, bro sio tajiri, hapa tunalia na RC aliyevunja sheria sio tajiiri, usilete za kuleta hapa wewe tafiti, hivi unaishi dunia gani wewe?

Jamani msituchanganye, the news ni Ditopile na ndivyo hii mada inavyosema!
 
Alichofanya Bwana Ditopile ni kosa la jinai na anastaili kufungwa. Yeye ni mwanajeshi mstahafu anajua nini maana ya silaha. Anastahili kifungo kwa kosa hilo. Lakini kadri ninavyoijua nchi yetu Ditopile hatafungwa na ataendelea na kazi kama kawaida ukichukilia aliyeuawa ni mlala hoi.Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi amina.
 
Back
Top Bottom