Ukiwa Rais kila siku unapaswa kuzungumza na nani?

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Hvii mtu akiwa Rais kila siku anapaswa kuwasiliana na nani? Je, siku inaweza kupita kwa usalama kabisa bila kuwasiliana walau kwa simu na hawa:

1. Waziri Mkuu
2. Mkuu wa Majeshi
3. Mkuu wa Polisi
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa
5. Katibu Mkuu wa Chama Tawala

?
 
4 --- 1. Waziri Mkuu
2 --- 2. Mkuu wa Majeshi
3 --- 3. Mkuu wa Polisi
1 --- 4. Mkuu wa Usalama wa Taifa
5 --- 5. Katibu Mkuu wa Chama Tawala

...and the rest kama simu yako bado ina salio!
 
Labda niliweke swali katika muktadha wa nchi ya Afrika: Hivi kiwa Rai wa nchi ambayo watu wanachinjana kwa mapanga, viongozi wanapigana vikumbo vikaoni na kufumbia macho ufisadi, fedha zinaibwa na kubwiwa kama chibuku, ni nani hasa unapaswa kuwasiliana naye kila siku ili kuhakikisha nchi haiendi mrama hasa unapokuwa na shughuli nyingi za kimataifa na kibiashara?
 
Swali lako lilieleweka tangu mwanzo na huu muktadha ulieweka pia... nimekujibu according to hali iliyopo na list yako uliyoweka; kuanzia wizi wa mabillioni ya pesa za 'kilimo kwanza' mikoani, mauaji ya Musoma, n.k. n.k. Ni nani wa kumlaumu?? The buck stops with the President! Finito.
 
Labda niliweke swali katika muktadha wa nchi ya Afrika: Hivi kiwa Rai wa nchi ambayo watu wanachinjana kwa mapanga, viongozi wanapigana vikumbo vikaoni na kufumbia macho ufisadi, fedha zinaibwa na kubwiwa kama chibuku, ni nani hasa unapaswa kuwasiliana naye kila siku ili kuhakikisha nchi haiendi mrama hasa unapokuwa na shughuli nyingi za kimataifa na kibiashara?

Kama Rais wa Marekani watu wake walipouwawa na Magaidi au watoto wa shule wanavyoenda na Bunduki na kuua wenzake. Anapaswa kuwasiliana na nani kila siku?
 
Surely that does not mean he is party to that, does it?

Yep, true that, but he has the authority to command and speak to them all at his slightest whim, just to regurgitate your question. Else what would be the significance of leadership or being in charge for that matter?
 
Inategemeana pia ni haiba ya Rais husika, kuna marais wengine hawapendi mambo magumu, wanataka kila siku asikie watu wakimsifia na kumtukuza, huku akiburudishwa na 'viburudisho' tofauti tofauti na wengine akiwaoa kabisa!! Rais kama huyu, atapenda kuzungukwa na watu aina hiyo tu bila kujali amempa nafasi gani ya uongozi.

Kama Rais ni mjasiliamali...basi ikulu patakuwa ni mahali pa walanguzi na wabaka uchumi kukutuna na kujadili interest zao!!

Kama Rais ni kama Obama, kutokana na hali yenyewe ya kidaidi basi kila siku lazima awasiliane na watu wa usalama wa taifa and other key figures!!
 
4 --- 1. Waziri Mkuu
2 --- 2. Mkuu wa Majeshi
3 --- 3. Mkuu wa Polisi
1 --- 4. Mkuu wa Usalama wa Taifa
5 --- 5. Katibu Mkuu wa Chama Tawala

...and the rest kama simu yako bado ina salio!
Hiyo namba 5 ndipo mambo yanapoharibikia kama mtu mwenyewe ni Makamba. Atakuharibia siku bure!
 
Labda niliweke swali katika muktadha wa nchi ya Afrika: Hivi kiwa Rai wa nchi ambayo watu wanachinjana kwa mapanga, viongozi wanapigana vikumbo vikaoni na kufumbia macho ufisadi, fedha zinaibwa na kubwiwa kama chibuku, ni nani hasa unapaswa kuwasiliana naye kila siku ili kuhakikisha nchi haiendi mrama hasa unapokuwa na shughuli nyingi za kimataifa na kibiashara?

Add, nchi ambayo watu wakipata mkono wa albino wamekuwa matajiri!!!!
 
Wazungu, Waarabu, Wahindi, au yeyote ambaye si ngozi nyeusi, labda kama atawezesha kupata *SIFA* , kualikwa au kutangazwa *NJE* ya nchi.
 
Mkeo ndio unatakiwa kuwasiliana naye kila siku, wengine wote uliowataja ni only sporadically
duh ina maana mshauri wa kwanza kabisa ni mkewe? sababu mkewe ndiyo anakaa na rais muda mrefu kuliko hao wote aliowataja mtoa hoja, sasa je mke wa rais akiwa bogasi ninakuwaje?
 
Kuhusu hili la mke mnakumbuka Mwalimu alisema nini enzi za Loliondogate I?
 
Back
Top Bottom