ukiwa home aka nyumbani!!!

stevoh

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
2,921
1,104
hivi niambie ukiwa home panaboa au panaudhi au panavutia au panachosha au pakoje. Kwetu sisi vyote vinatokea kwa mida tofauti tofauti.
 
panavutia sana kwangu
napenda sana kuwa nyumbani
nakuwa na amani kuliko sehemu nyingine yeyote.
 
Napenda kuwa nyumbani. . na kuboreka ni ngumu maana nikiona vipi napigq zangu usingizi. Nikiwa nje ya nyumbani ndio naweza nikaboreka kirahisi kwa kukosa uhuru.
 
Napenda kuwa nyumbani. . na kuboreka ni ngumu maana nikiona vipi napigq zangu usingizi. Nikiwa nje ya nyumbani ndio naweza nikaboreka kirahisi kwa kukosa uhuru.

mmh! Sasa kwa mfano weekend yote ukohome unalala tu?
 
......Inategemea, week days nipo busy na mihangaiko ya maisha. Weekend nakuwa off, Jmos napenda kushinda home wala hapaniboi.
Ila jumapili naweza shinda home hadi mchana, baada ya hapo naboreka jioni lazima niende out.
 
Unapoongelea home unamaanisha 'kwako' ama 'kwenu'? Ni wajibu wako kupatengeneza nyumbani kwako kuwe comfortable ili upapende na usiboreke. No wonder watu wanaweka mini golf course nyumbani..
 
Week days nakua Job, jumamosi naamka saa 2 asubuhi napata kahawa yangu baada ya hapo ni Movie mpaka saa 9 alasiri, Nikitoka hapo Naingia Bafuni nikitoka hapo naenda kupata Menu baada ya hapo ni Lager mpaka saa 6 usiku nikiwa hapo nakua nacheki Ligi ya Uingereza na Spain... Ikifika saa 7 usiku siku moja moja huwa naenda Club, Jumapili hua nafanya usafi.. Mpaka time fulani naanza kucheki Movies au Mpira ka upo.. Ikifika saa 4 usiku nalala kwa ajili ya Jumatatu. Huwa siboreki nikiwa home au mtaani
 
Inategemea nyumba yako ina muonekano gani,
Kama ni safi ,inavutia ,mapambo yamekaa kimpangilio
Miundo mbinu ya home kama TV ,Radio, Laptop or Simu iliyo connected na mtandao
inayokufanya usikosekane JF na kwingineno
hewa ya kutosha ,pasafi ...Utatamani usiondoke ndani tusker or serengeti serengeti kwenye fridge
Ukiingia Room kama ndo kusafi kitandani kinavutia kujilaza ..
Hutaboreka hata kidogo,
 
panaboa sana kama tanesco wamechukua umeme ili zaidi ya hapo pako poa sana..
 
Inategemea nyumba yako ina muonekano gani,
Kama ni safi ,inavutia ,mapambo yamekaa kimpangilio
Miundo mbinu ya home kama TV ,Radio, Laptop or Simu iliyo connected na mtandao
inayokufanya usikosekane JF na kwingineno
hewa ya kutosha ,pasafi ...Utatamani usiondoke ndani tusker or serengeti serengeti kwenye fridge
Ukiingia Room kama ndo kusafi kitandani kinavutia kujilaza ..
Hutaboreka hata kidogo,

Ee bana , kama arrangement nzuri na sehemu ipo spacious inanoga sana kukaa home.

Iwe living room au chumba kulala sipendi kuwe na makorokoro mengi , kama kitanda chumbani na TV baas. Sebuleni nako TV na viti vya kukaa na ka meza ka TV kadogo ambacho kata accomodate home theatre inatosha :lol:
 
Back
Top Bottom