Ukitaka uwe mwalimu mwenye hela soma Civics

ayubuchacha12

Member
May 8, 2012
19
7
Makaratasi huwa ni mengi ya kusahihisha somo la uraia/civics kwenye mitihani ya kitaifa ya sekondari, General study (GS) kwa sekondary ya juu (High School) na development studies kwa ngazi ya vyuo. Kwa hiyo waalimu wanaosahihisha URAIA wanapata hela nyingi kushinda waalimu wa PHYSICS, CHEMISTRY, BIOLOGY na MATHEMATICS. Ukweli unaendelea kuwa huo huo kwa maprofesor wa masomo magumu magumu ukilinganisha na maprofesor wa masomo ya usanii (arts), kweli sio kila mwenye mbio ashindaye... watu wanaofanya kazi ngumu na kwa masaa mengi sio wanaolipwa vizuri hasa hapa Africa. NO FAIRNESS... Kama mtu anajua kwa nchi za wenzetu walioendelea tofauti ya mshahara na marupurupu nchi kama Uholanzi kwa mtu wa kima cha chini na kima cha juu ni mara nne tu,,, mfano profesor anamzidi mhudumu wa ofisi mara nne tu...eg profesor kama analipwa milioni 4, mhudumu analipwa milioni moja....lakini kwa hapa kwetu profesor analipwa milioni 3,,,,mhudumu analipwa laki moja....what a difference!!!!

Jamani keki ya Taifa haigawanywi kwa usawa,,,,hata sijui hao watu wanaopanga mishahara kama wamesoma au wanabuni tu kiwango cha mishahara????????

Tafadhari ofisi ya utumishi wa umma na wizara ya kazi na ajira mwende ziara ulaya na nchi zilizoendelea mkajifunze jinsi gani ya KUGAWA KEKI YA TAIFA KWA USAWA,.
 
Kwa mfano hapo unachotaka kuzungumzia ni nini?

kama nimemwelewa ana maanisha wanafunzi wakimbilie kuchagua combination za usanii.
Anasahau kuwa malaria haija expire, mainjinia hawatokani na usanii nk.
 
kama nimemwelewa ana maanisha wanafunzi wakimbilie kuchagua combination za usanii.
Anasahau kuwa malaria haija expire, mainjinia hawatokani na usanii nk.
namaanisha kuwe na haki katika malipo, mwenye kufanya kazi ngumu / kusoma masomo magumu alipwe mshahara mnono.
 
Kwa mfano hapo unachotaka kuzungumzia ni nini?
Kuna watu fyatu kwelikweli, sasa kama mdomo wako unanuka unaogopa kuongea si bora huo mkono ungeukata ili ushindwe kubonyeza keyboard kuweka huu *****? Mwenzio ana lipoint, wewe unaleta za kuleta, ebo!
 
ninyi waalimu hovyo kabisa. natamani ningekuchapa viboko kama yule DC
 
Kuna watu fyatu kwelikweli, sasa kama mdomo wako unanuka unaogopa kuongea si bora huo mkono ungeukata ili ushindwe kubonyeza keyboard kuweka huu *****? Mwenzio ana lipoint, wewe unaleta za kuleta, ebo!

:A S thumbs_down:
 
Na usipopata Nafasi ya kusahihisha? Na ni Mara Ngapi kwa Mwaka.

MAWAZO MGANDO HAYO

Wenzako wanaingiza hela kwa TOPIC MOJA 15000/= MPAKA 25000/= Kwa Mwanafunzi Mmoja wa Sayansi. TUITION INALIPA. Unakuta Anawanafunzi 150-200 wanaosoma topic zaidi ya Tano. Zidisha kwa Hela hiyo uone anapata sh. Ngapi kwa Mwezi.

WE UNAFIKIRIA KUSAHIHISHA MITIHANI. Wenzako wanaondoka na Mil 3 kwa Mwezi za TUITION.

MFANO:
¤Sir Unga
¤T.O
 
hii ndio bogo bwana usishangae sana..BAJETI YA OFISI YA RAISI YA CHAI TU IS BILLIONS OF MONEY onategemea nini??
 
Umesoma usanii aka arts? Jamaa ameeleweka sana tu.
Mzee na wewe chukua hii.:A S thumbs_down: kwa sababu nyie wote wawili ni wanafunzi wa secondary... hivyo mnafikiri kisekondari sekondari tu. Je maprofessor na malectures wa universities na vyuo vya kati nao wasomee civics ili wavute mkwanja mwingi? Mbona hiyo pesa ya kusahihisha civics ni mbuzi na ya msimu tu? Think big!
 
Back
Top Bottom