Ukitaka kushangaa nenda Buza Tandika

Buza na Tandika ni sehemu mbili tofauti. Kwakuwa maelezo yako yanaonyesha hiyo Toyo ipo Buza hebu toa ufafanuzi ni buza ipi? kwa Lulenge, Kanisani au wapi?
 
Hao ng'ombe kama wapo zenji nishitue nipate mtaji watu hatuna ajira
wala mitaji halafu mitaji inazunguka inaachwa nakuja huko kuwachukua
tuache masikhara bwana
 
DISTAZO, Buza sehemu gani? hebu nieleze ili na mimi nikashuhudie kwa macho yangu kwani muda si mrefu nitatinga huko.

Ukiwa unakaribia Tandika relini, ukiuliza kila mtu anaijua hii story.
 
Mimi nilidhani ina
uhusiano na uislamu kwa kuwa husomwa na mashehe. Nielimishe katika hili
ndugu. Lugha inayotumika ni ile ya qur-an au ni arabic?

Lugha ni Arabic. Qur-an ni mafunzo,yanaweza kuwa translated kwenye lugha yoyote ile.
 
kumbe,,ucpoamini hakuna lolote,na haihicani na mafundisho ya kiislam

Unajua dni ilikuja vizuri sana na ikaachwa vizuri tu, ila kuna watu wamekuja kuitumia kipuuzi kabisa kwa maslahi yao,na hii yote imechangiwa na maisha kuwa magumu tu,
Ntakuambia kitu hii dini mfano ya kiislam katika mafundisho yake tumesoma kuwa imeteremshiwa sana katika nchi za kiarabu hasa saudia arabia'na baadhi ya mitume wakiwa misri, Iraq, Sham au syria,Palestina na israel, ajabu kitu kimoja nlikuja kushangaa,nimewahi kuishi katika baadhi ya nchi hizo ambazo dini ilishukia,watu wa kule baada ya kunifaham kuwa mimi natokea east africa hasa znz basi wengi sana wakawa wananiulizia kuhus wataalum yaani waganga wenye kusomea watu wenye kujua mambo ya kimazingira,
Mwisho nikawa nawauliza mtaalum wa nini mnataka wananiambia maustadh au masheikh wanaojua kusomea vitu vikawa kweli,wengi wao nlikuwa nawapa jibu moja tu,nawaambi ikiwa dini imeshukia nchi hizi zenu na hao wataalum wamekuja kuisoma dini huku kwenu na hapa kwenu hakuna hao wataalum je hao wa kwetu hiyo elimu ya uganga wameitoa wapi? Mwisho nikawa nawaambi hakuna tiba zaidi ya kuifata Qur-an na kile alifundisha mtume muhammad vingine vinavyobaki ni utapeli tu wakibinadamu,wengi kati yao walikuwa wananielewa sana nini nasema,
 
Buza kuna pikipiki Toyo ya matairi matatu imepaki pembeni ya barabara yapata mwaka sasa baada ya kuuliza kulikoni nikaambiwa hiyo Toyo imeshauwa watu sita. Wezi waliiba na waliohusika na hiyo Toyo walianza kufa mmoja baada ya mwingine walipofika sita ndugu zao waamua kuileta hapo barabarani wakaitelekeza.
Wakati barabara inajengwa aliletwa shehe aruhusu iwekwe pembeni baada ya kujenga ikarudishwa palepale mpaka hivi leo, tuliendelea kushangaa.
Tuliendelea kumuuliza jamaa mmoja akadai mwenye hiyo Toyo yake hawezi kwenda kuichukua kwa sababu ilishasomewa kitabu yaani Al badir na kama akienda kuichukua na yeye anakufa, hii imekaaje?
Nikifanikiwa kupita tena huko nitawawekea picha hapa.

Angalia usije kuunguza kasimu kako kamchina au ukwa kipofu, wee penda kupiga picha kisichopenda kupigwa picha. :smiling:
 
Natamani ningeona kwenye kuran iwe inataja msamaha kwa watenda dhambi, hapo ningeupenda sana uislamu

Tafuta qur-an yenye tafsiri soma, msamaha umetajwa mara nyingi sana katika qur an,msamaha una stop tu pale roho itapokuwa imetolewa lakini kinyume chake upo,
 
Angalia usije kuunguza kasimu kako kamchina au ukwa kipofu, wee penda kupiga picha kisichopenda kupigwa picha. :smiling:

Hata kuangalia itakuwa hairuhusiwi?, nikiweka picha humu utakuwa huangalii? basi una nia mbaya na hiyo Toyo.
 
Mimi nilidhani ina uhusiano na uislamu kwa kuwa husomwa na mashehe. Nielimishe katika hili ndugu. Lugha inayotumika ni ile ya qur-an au ni arabic?

Ndugu yangu ukiona mtu anasoma al-badr halafu anajiita sheikh basi jua huyo anafata dini yake na sio uislam, katika uislam albadir ni shirki,yaani anaesoma albadr ni mshirikina,na katika uislam tunaambiwa hakuna dhambi kubwa kama ushirikina, yaani tumefundishwa kuwa mtu anaefanya shirki dhambi yake ni kubwa sana hata kuliko mtu aliuwa,
 
Angalua umetujuza kitu fulani kuhusu hiyo kitu. Hii inanipa picha kuwa kuna waislamu ambao hawajui mafundisho ya kwenye vitabu vyao.
Nakumbuka miaka ya karibu na 2000 kuna msikiti mmoja upo mwamboni Tanga walikuwa wanatangaza kwenye loud speaker (count down) siku watakayosoma Al Badri kwa kuhimiza mtu aliyeiba kitu fulani(kulingana na aliyeripoti kuibiwa) arudishe hicho kitu kwa mwenyewe vinginevyo atadhurika. Na matangazo kama haya yalikuwa yakitolewa mara kadhaa.
Kwa maana hii hata yule (muumini au shehe) aliyekuwa anatangaza akiwa ndani ya msikiti alikuwa hajui.

Ndugu yangu hao ndio tunawaita masheikh ubwabwa tu, wamekuwa wanamchafua sana mtume kwa njaa zao,dini hii haikuwa hivi mtume aliiacha ikiwa safi kabisa na baada ya mtume miaka 400 yaani karne 4 dini bado ilikuwa safi tu,ila baada ya hapo watu wakaanza kutafuta nafuu katika baadhi ya sheria maana wengine hata zakka walikuwa wanapinga basi wakaanza kuitengeneza kila mmoja na lake,lakini msingi wa dini ukabaki katika qur an na hadithi za mtume ambazo ni sahihi japo kuna baadhi ya hadithi nyingi tu feki ziliingizwa tu ili kukidhi mahitaji ya baadhi ya wafalme au watu flani ambazo kiukweli hakuzisema mtume,ndio moja yao hayo mambo ya albadir hata mtume hayajui wala wafuasi wake alowaacha pia hawajui kitu hicho
 
Viongozi wetu wa dini wamekuwa sawa na wana siasa tu sioni tofauti yao,maana ukitazama msingi wa siasa ni mzuri sana lakini wanaosimamia huo msingi mambo wanayofanya ni kinyume kabisa,
Ni sawa na viongozi wetu wa dini tena hapa ni wa dini zote wamekuwa wao ndio vyanzo vya kila upuuzi,wamekosa maadili wamekosa hekma wamekuwa wapo wapo tu,wengi wao mafundisho ya dini zao wameyasahau zaidi wanafata matamanio yao tu,

Ntawapa mfano wa kiongozi muadilifu ambae aliwahi kutokea baada ya mtume muhammad huyu bwana alikuwa anaitwa omar bin khatab,huyu bwana historia inasema alikuwa katika ujinga na hakuwa muislam na alikuwa adui mkubwa wa uislam na aliuwa sana waislam,lakini baada ya miaka mingi huyu bwana akaamini yaani akasilimu akamfuata mtume,

Basi huyu bwana alimsoma mtume sana akasoma sana dini mpaka ikamwingia akawa ni mtu wa karibu sana na mtume,na huyu bwana alikuwa ni mtu tajiri sana pale makkah na alikuwa ni maaruf pia,
Historia inasema huyu ndio katika viongozi waadilifu duniani ambao walipata kutokea basi omar alikuwemo,
Omar ni khalifa wa mtume wa 3 yaani baada ya kufariki mtume aliefuata kuwa mtawala wa makkah alikuwa ni Abubakar siddiq, wa pili Othman bin affan,na wa 3 alikuwa ni Omar bin khattab,
Kuna siku jamaa mmoja alitembelea ofisini kwake omar ilikuwa muda wa usiku alikuwa ana maongezi nae wakati huo akiwa omar ndio kiongozi mkuu wa saudi arabia,basi huyu bwana alikuwa akimuuliza omar maswali mengi tu ya dini na family yake anachanganya maswali, basi omar alikuwa na mishumaa miwili pale ofisini kwake basi alikuwa anawasha mshumaa mmoja mara anazima mwingine,yule mgeni wake ikabidi amuulize mbona mara anazima huu anawasha huu?
Omar akamjibu wewe unaniuliza maswali mchanganyiko kuna maswali unaniuliza yanahusu family yangu ndio maana nazima mshumaa huu nawasha mwingine'kwa sababu mshumaa mmoja nimenunua kwa pesa ya kwangu na mwingine kwa pesa ya waislam ndio maana hapa naogopa kupata dhambi kila ukiniuliza swali la family yangu nazima mshumaa wa waislam nawasha wangu nakujibu,na ukiniuliza swali la waislam nazima wangu nawasha wa waislam pia sitaki kuwafanyia dhulma family yangu,
Hebu jaribu kufikiria uadilifu gani huyu jamaa aliokuwa nao?

Na historia inatuambia huyu omar alikufa kwa maradhi ya tumbo kwa sababu alikuwa hataki kula vizuri licha ya yeye kuwa tajiri alikuwa akisema hawezi kula chochote kizuri wakati mitaani kuna watoto yatima wamejaa na wajane wasio na misaada ndio akaona badala ya kula yeye vizuri bora wengine wale,
Je viongozi wetu wa leo hata robo ya uadilifu wanayo?
 
Buza na Tandika ni sehemu mbili tofauti. Kwakuwa maelezo yako yanaonyesha hiyo Toyo ipo Buza hebu toa ufafanuzi ni buza ipi? kwa Lulenge, Kanisani au wapi?

Samahani hata mimi ni mgeni mitaa ile isipokuwa leo nimemuuliza vizuri dereva wangu amesema panaitwa Yombo Dovya, vile vile nimefanikiwa kupata picha as objective evidence.

Jiulize kama ina muda karibu mwaka hapo basi itakuwa ilitelekezwa ikiwa mpya kabisa.Kweli ukishangaa ya Musa utaona ya firauni.


DSC01262.JPG DSC01260.JPG DSC01261.JPG
 
Mngalikuwa waadilifu kiasi hiki mngalienda kuvunja, kubomoa na kuchoma makanisa kweli? Hivi mnajua nini maana ya nyumba ya Mungu nyie? Mmebakia kutishiana huku mkitawaliwa na ujinga wa kupindukia. Ukiona mtu wa miaka arobaini anaridhia kuoa mjukuu wake yaani mtoto wa miaka kumi na nne ujue dini yake ni ya shetani. Acheni kuabudu mashetani na ujinga wenu zingatieni maadili. Kwa kweli uislam ni umasikini tena ule wa kutupwa!
 
Mngalikuwa waadilifu kiasi hiki mngalienda kuvunja, kubomoa na kuchoma makanisa kweli? Hivi mnajua nini maana ya nyumba ya Mungu nyie? Mmebakia kutishiana huku mkitawaliwa na ujinga wa kupindukia. Ukiona mtu wa miaka arobaini anaridhia kuoa mjukuu wake yaani mtoto wa miaka kumi na nne ujue dini yake ni ya shetani. Acheni kuabudu mashetani na ujinga wenu zingatieni maadili. Kwa kweli uislam ni umasikini tena ule wa kutupwa!

Maskini ni wewe mwenye mawazo mgando,mara ngapi viongozi wa kanisa katoliki wamehusishwa na ulawiti wa watoto wadogo?je ujinga wa baadhi ya wawaumini wa ukristo mzigo huo tuupe ukristo au wahusika? Na je kanisa anglikana mpaka sasa linawachungaji mashoga na lina sapoti ushoga duniani je hapo ukristo unahusika? Na hapo ipi dini ya shetani? Acha kukashifu imani ya wengine jifunze kuheshimu watu na imani zao
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Hao ng'ombe kama wapo zenji nishitue nipate mtaji watu hatuna ajira
wala mitaji halafu mitaji inazunguka inaachwa nakuja huko kuwachukua
tuache masikhara bwana

Kwanini uhangaike hadi Zenji bana, wapo ng'ombe wengine waliosomewa hiyo kitu na sasa wanajichunga wenyewe tu, kunduchi tena barabarani kabisa, karibu na kambi ya jeshi RTS au ukitaka kuwapata kirahisi wanalala barabarani pale usawa wa bar ya MALANJA INN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom