Ukitaka kushangaa nenda Buza Tandika

Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,002
648
Buza kuna pikipiki Toyo ya matairi matatu imepaki pembeni ya barabara yapata mwaka sasa baada ya kuuliza kulikoni nikaambiwa hiyo Toyo imeshauwa watu sita. Wezi waliiba na waliohusika na hiyo Toyo walianza kufa mmoja baada ya mwingine walipofika sita ndugu zao waamua kuileta hapo barabarani wakaitelekeza.
Wakati barabara inajengwa aliletwa shehe aruhusu iwekwe pembeni baada ya kujenga ikarudishwa palepale mpaka hivi leo, tuliendelea kushangaa.
Tuliendelea kumuuliza jamaa mmoja akadai mwenye hiyo Toyo yake hawezi kwenda kuichukua kwa sababu ilishasomewa kitabu yaani Al badir na kama akienda kuichukua na yeye anakufa, hii imekaaje?
Nikifanikiwa kupita tena huko nitawawekea picha hapa.
 
Tuliendelea kumuuliza jamaa mmoja akadai mwenye hiyo Toyo yake hawezi kwenda kuichukua kwa sababu ilishasomewa kitabu yaani Arbadili na kama akienda kuichukua na yeye anakufa, hii imekaaje?
Nikifanikiwa kupita tena huko nitawawekea picha hapa.

Duh! hiyo kali kwani aliesoma hilo arbadili ni nani? kama ni mwenye toyo si alitakiwa akachukue mali yake!!!
 
unakua umeshavuka pale kwa mama kibonge? mimi nashinda zangu pale gaddaf lakini bado sijaona hiyo kitu. mia
 
Yanatokea hayo.Njooni Zanzibar maeneo ya mchina mwanzo, kuna ngombe zaidi ya 20. hawana mwenyewe wanazurura tu mpaka manispaa imewashindwa.kila mwaka wanaongezeka. inasemekana kuna ngombe kama watatu waliibiwa miaka mingi kidogo nyuma. mwenyewe akawasomea Albadiri.walioiba wakapukutika, tokea miaka hiyo ngombe hawana mwenyewe wanazurura na kuzaliana tu mitaani.kila mtu anawaogopa.mbaya zaidi mwenye mali alishatangulia mbele ya haki.kwa wale wasiomini Quraan Tukufu waje wachukue mali za bure.au wakachukue hiyo Toyo.
 
Naomba uelewe kwanza Qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
Kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya Badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe
 
Natamani ningeona kwenye kuran iwe inataja msamaha kwa watenda dhambi, hapo ningeupenda sana uislamu
 
Natamani ningeona kwenye kuran iwe inataja msamaha kwa watenda dhambi, hapo ningeupenda sana uislamu[/QUOT
kwani uliisha tafuta ukakosa kuona......? msamaha upo bali una vipengere vyake ili upate kusamehewa. na anayesamehe ni mmoja baada ya kutimiza mashari ya toba.
 
Naomba uelewe kwanza Qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
Kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya Badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe

Asante kwa ufafanuzi huo, sasa mimi nikiipiga picha hiyo Toyo kuna tatizo lolote? nia yangu ni kuonyesha ushahidi bayana kuhusu nilichoelezea.
 
Naomba uelewe kwanza Qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
Kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya Badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe
Ngongoseke, umefunguka na umetupa fundisho binafsi nilikuwa sijui nini maana ya Albadir, usipoamini haiwezi kufanya kazi.
 
Last edited by a moderator:
Maana ya Al - Badri ni hii, jina hilo linatokana na majina ya waislam waliopigana vita ya Badri na makafiri kisha wakashinda wakati waislam walikuwa 333 na makafiri walikuwa 1000. Baada ya hapo Allah aliwabashiria pepo watu hao waliokufa na waliohai kutokana na vita hiyo.

Sasa binadamu kwa ubabaishaji wao wanaingiza shirki au ulozi na dua hiyo wakaiita Al - Badri. Kifupi Al - Badri ni bidaa.
 
Naomba uelewe kwanza Qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
Kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya Badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe

Mimi nilidhani ina uhusiano na uislamu kwa kuwa husomwa na mashehe. Nielimishe katika hili ndugu. Lugha inayotumika ni ile ya qur-an au ni arabic?
 
Naomba uelewe kwanza Qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
Kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya Badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe

Angalua umetujuza kitu fulani kuhusu hiyo kitu. Hii inanipa picha kuwa kuna waislamu ambao hawajui mafundisho ya kwenye vitabu vyao.
Nakumbuka miaka ya karibu na 2000 kuna msikiti mmoja upo mwamboni Tanga walikuwa wanatangaza kwenye loud speaker (count down) siku watakayosoma Al Badri kwa kuhimiza mtu aliyeiba kitu fulani(kulingana na aliyeripoti kuibiwa) arudishe hicho kitu kwa mwenyewe vinginevyo atadhurika. Na matangazo kama haya yalikuwa yakitolewa mara kadhaa.
Kwa maana hii hata yule (muumini au shehe) aliyekuwa anatangaza akiwa ndani ya msikiti alikuwa hajui.
 
Yanatokea hayo.Njooni Zanzibar maeneo ya mchina mwanzo, kuna ngombe zaidi ya 20. hawana mwenyewe wanazurura tu mpaka manispaa imewashindwa.kila mwaka wanaongezeka. inasemekana kuna ngombe kama watatu waliibiwa miaka mingi kidogo nyuma. mwenyewe akawasomea Albadiri.walioiba wakapukutika, tokea miaka hiyo ngombe hawana mwenyewe wanazurura na kuzaliana tu mitaani.kila mtu anawaogopa.mbaya zaidi mwenye mali alishatangulia mbele ya haki.kwa wale wasiomini Quraan Tukufu waje wachukue mali za bure.au wakachukue hiyo Toyo.

Tanga walikuwepo mbuzi wa al Badri, watu walikuwa wanawaogopa kuwala enzi hizo. Siku hizi wameliwa wote, hakuna aliyebaki.
Usisikie, dhiki ni mwalimu mkuu, itakufanya utafute ufumbuzi na utaupata tu.
 
Yanatokea hayo.Njooni Zanzibar maeneo ya mchina mwanzo, kuna ngombe zaidi ya 20. hawana mwenyewe wanazurura tu mpaka manispaa imewashindwa.kila mwaka wanaongezeka. inasemekana kuna ngombe kama watatu waliibiwa miaka mingi kidogo nyuma. mwenyewe akawasomea Albadiri.walioiba wakapukutika, tokea miaka hiyo ngombe hawana mwenyewe wanazurura na kuzaliana tu mitaani.kila mtu anawaogopa.mbaya zaidi mwenye mali alishatangulia mbele ya haki.kwa wale wasiomini Quraan Tukufu waje wachukue mali za bure.au wakachukue hiyo Toyo.

Tatizo lenu mnaiaminia quraan ikifail mnaanza kuchinja askari waislamu nyie vipi bwana.
 
Buza kuna pikipiki Toyo ya matairi matatu imepaki pembeni ya barabara yapata mwaka sasa baada ya kuuliza kulikoni nikaambiwa hiyo Toyo imeshauwa watu sita. Wezi waliiba na waliohusika na hiyo Toyo walianza kufa mmoja baada ya mwingine walipofika sita ndugu zao waamua kuileta hapo barabarani wakaitelekeza.
Wakati barabara inajengwa aliletwa shehe aruhusu iwekwe pembeni baada ya kujenga ikarudishwa palepale mpaka hivi leo, tuliendelea kushangaa.
Tuliendelea kumuuliza jamaa mmoja akadai mwenye hiyo Toyo yake hawezi kwenda kuichukua kwa sababu ilishasomewa kitabu yaani Al badir na kama akienda kuichukua na yeye anakufa, hii imekaaje?
Nikifanikiwa kupita tena huko nitawawekea picha hapa.

DISTAZO, Buza sehemu gani? hebu nieleze ili na mimi nikashuhudie kwa macho yangu kwani muda si mrefu nitatinga huko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom