Ukitaka kumtongoza mwanamke tumia sikio la kushoto…………utampata………….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Wataalamu wamebaini kwamba, sikio la kushoto ndilo likilishwa kauli ya upendo hushika sana kauli hiyo na aliyeambiwa kauli hiyo huwa hawezi kuisahau kirahisi. Uwezekano wa jambo hili siyo suala la kudhani, kwani linaweza kuelezewa kutokana na mfumo wa akili. Kauli hii inaweza kuwashangaza wengi, lakini ndivyo wataalamu wanavyoeleza.

Kwa nini wanasema hivyo?

Wanasema hivyo kutokana na ukweli kwamba sikio la upande wa kushoto linathibitiwa na upande wa kulia wa ubongo. Upande huu wa kulia wa ubongo ndiyo ambao unashughulika na hisia za binadamu kama furaha, huzuni na mengine. Kwa kuwa upande wa kulia wa ubongo ndiyo unaodhibiti hisia za binadamu na sikio la kushoto linadhibitiwa na upande huu wa ubongo, kauli zote za kihisia zikipitia kwenye sikio la kushoto zinakuwa na ugumu katika kufutika. Ugumu huu unatokana na ukweli kuwa zimeingilia mahali pake.

Kwa hiyo kama tunataka kuhakikisha kwamba wapenzi wetu hawasahau kirahisi au maneno tunayowaambia kuhusiana na jinsi tunavyowapenda yanawaingia kwa kina, inabidi tuzungumze nao kwa kupitishia maneno hayo kwenye sikio la kushoto……………
 
Gud mrng dingi.. . . .Ngoja nijitahidi kila nikimyatia Smile nimuende upande wa kushoto.Eti anadai ana bikra!Kama ni kweli si nitakua luck guy?
 
Last edited by a moderator:
Naomba niweke angalizo: Hapa sizungumzii yale mapenzi ya mwanamke kuvutiwa na mwanaume kutokana na rasilimali anazomiliki...Gari, nyumba, biashara kubwa au ukwasi alio nao mwanaume, kwani hapo mwanaume hahitaji kutumia gia kubwa sana kumpata mwanamke........Mimi nazungumzia mapenzi ya dhati lakini sio ya kuhemkwa. Nazungumzia mapenzi ambayo yanatoka moyoni kabisa.

Maana najua kuna watu watakuja hapa na kusema shida yote hiyo ya nini wakati siku hizi chapaa inaongea...........!
 
Gud mrng dingi.. . . .Ngoja nijitahidi kila nikimyatia Smile nimuende upande wa kushoto.Eti anadai ana bikra!Kama ni kweli si nitakua luck guy?
Sio kusudio langu kuwafundisha uasherati...............Kama umempenda Smile peleka posa si ameshasema ni BIKRA...............!
 
Last edited by a moderator:
Naomba niweke angalizo: Hapa sizungumzii yale mapenzi ya mwanamke kuvutiwa na mwanaume kutokana na rasilimali anazomiliki...Gari, nyumba, biashara kubwa au ukwasi alio nao mwanaume, kwani hapo mwanaume hahitaji kutumia gia kubwa sana kumpata mwanamke........Mimi nazungumzia mapenzi ya dhati lakini sio ya kuhemkwa. Nazungumzia mapenzi ambayo yanatoka moyoni kabisa.

Maana najua kuna watu watakuja hapa na kusema shida yote hiyo ya nini wakati siku hizi chapaa inaongea...........!
Afadhali umeweka angalizo mapema
 
Duuh sasa ndio nimejua kwanini I am not successful in love life, I am somehow kiziwi upande wa kushoto. Sitaki kuamini!
 
Duuh sasa ndio nimejua kwanini I am not successful in love life, I am somehow kiziwi upande wa kushoto. Sitaki kuamini!

Yaani Hiyo Avatar Yako nimeizimiaje,,,, Nimependa Lipstick hiyo ukiangalia Half of your Lips On the left ndo ziko red. Are you trying to tell us something like we should move toward U r left ear??
 
Back
Top Bottom