Ukitaka kujua tafakari - Usiogope!

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Kwa wanaopenda kutafakari napenda kuwakaribisha katika tafakari yangu hii. Waweza kuipanua, naamini itakusogeza hatua kadhaa mbele katika uchambuzi wa mambo.

1. Uhai wa mtanzania ni nini?

2. Nani wanawajibika kuulinda uhai wa mtanzania?

3. Je, wajibu huu unaweza kukasimiwa?

4. Je, ikitokea uhai wa mtanzania ukitoweka kwa sababu yoyote, nini haki yake, wawakilishi wake, jamii ya watanzania?

5. Nini uhusiano wa uhai wa mtanzania mmoja mmoja na:

o Daktari?

o Polisi?

o Mwanajeshi (JW)?

Karibu Great thinker.:A S crown-2:
 
1. Uhai wa mtanzania ni nini?
Ni haki yake ya msingi ya Mtanzania kuishi kwa afya njema na kupumua kwa jinsi Mungu alivyomuumba ndani ya Ardhi ya Taifa lake kwa kuishi na kupata riziki na maitaji yake yote ya msingi kwa kushirikiana na jamii husika kwa njia halali na pia kupewa ulinzi kiusalama na afya wa yeye,familia yake, jamaa zake,na jumuhiya yake wa ndani na nje ya Taifa lake popote pale dunia kwa kufuata sheria na taratibu za Nchi yake na Taifa husika.

2. Nani wanawajibika kuulinda uhai wa mtanzania?
Serikali yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikishirikiana na jamii yake husika ndio wenye mamlaka na wajibu wa kumlinda Mtanzania

3. Je, wajibu huu unaweza kukasimiwa?
Hakuna na kamwe hauwezi kukasimiwa kwa kuwa maisha hawekewi rehani au maisha hayafanyiwi majaribio

4. Je, ikitokea uhai wa mtanzania ukitoweka kwa sababu yoyote, nini haki yake, wawakilishi wake, jamii ya watanzania?
Ni wajibu wa wanandungu na jamii,kujua sababu za kifo cha mwanajamii ambae nimtanzania na ndio maana uwa kunatolewa cheti cha kifo na pale kunapokuwa na utata serikali inajukumu la kutoa maelezo kwa kufanya uchunguzi wa kimahabara [Post-Mo] na kutoa reporti kwa wahusika chanzo cha kifo a sababu za kifo za mtanzania huyo,hivyo mwenye dhamana kubwa ya Afya ya Mtanzania na uhai wake ni Serikali yake.Ndio maana vyeti vya vifo vonatolewa na Serikali kupitia Taasisi husika.

5. Nini uhusiano wa uhai wa mtanzania mmoja mmoja na:
Kwa mfumo wetu tulivyofika hivi sasa ili ni tatizo kubwa sana na ndio maana bima ya afya mpaka sasa ni kitendawili kwa swala la mtanzania mmoja mmoja.Hivyo dhamana ya uhai wa mtanzania kiharisia ni swala la mtanzania mmoja mmoja yeye na familia yake au watu wake wa karibu wanaomzunguka na kiserikali imebakia ni turufu ya hisani na sio wajibu.
o Daktari?
Ni kumtibu mtanzania na kupatia taarifa za ugonjwa na kutoa taarifa za mgonjwa kwa wanandugu pindi hali ya mgonjwa Mtanzania inapokuwa mbaya na hana uwezo wa kuipokea taarifa na kuamua hivyo inabidi wanafamilia au jamaa kuamua kwa niaba.lakini kwa sasa Tanzania inaupungufu mkubwa wa madaktari kwa kuwa kwa wenzetu kama CUBA daktari mmoja anahudumia familia mbili mpaka tatu.Lakini kwa Taifa letu daktari mmoja anahudumia maelefu ya familia.

o Polisi?
Kumlinda Mtanzania yeye na familia yake,ndugu zake,jamaa zake na jumuhiya yake kwa ujumla wao na mali zao dhidi ya wanajamii waovu au wageni waliondani ya Taifa na kimataifa pale inapobidi kwa kutumia sheria na kanuni jamii iliyojitungia kama mwongozo wa kuisho kama watu wastaarabu.

o Mwanajeshi (JW)?
Kulinda Taifa kwa maana ya watanzania wote kwa ujumla wao,mali zao za ndani na nje ya Taifa dhidi ya adui yoyote wa Nje na ikibidi wa ndani ya Taifa kwa dhamana ya hali ya juu na kwa gharama yoyote ile kama Taifa.Kwa kuwa msingi mkuu wa jeshi ni kulinda mipaka ya Taifa dhidi ya Maadui wa Taifa.
 
DSN: Asante kwa tafakari yako nzuri, nimependa naitafakari na mimi kwa kina ila kwa haraka niongeze hii kwa tafakari yako:
- Hivi wajibu wa Mtanzania uko juu ya serikali kwa ujumla wake kwel(pana sana)i - hivi serikali huapa hivyo "kuwa italinda UHAI wa kila mtanzania?"

- Napenda hii ya wajibu kutokukasimika - kumbuka kuna kuapa

- Juu ya haki UHAI unapotoka sidhani kama kwa anayewajibika kulinda UHAI ni suala la post mortem hapa kwani hata yeye siyo mtaalamu - kwake ni kueleza imekuaje akaruhusu UHAI utoke na akiwa anayewajibika kulinda UHAI wa mtanzania huyu alikuwa wapi mpaka akaruhusu UHAI huo utoweke na anachukua hatua gani kuhusu aliyehusika kwa kosa lake na yeye kwa kuruhusu utoweke ..au siyo ....naendelea kutafakari zaidi nataraji na democratic atakamilisha tafakari yake karibuni

Come on Great thinkers --think, this is your week endd food fod for thought..
 
DSN:
- Hivi wajibu wa Mtanzania uko juu ya serikali kwa ujumla wake kwel(pana sana)i - hivi serikali huapa hivyo "kuwa italinda UHAI wa kila mtanzania?"

- Napenda hii ya wajibu kutokukasimika .

Wajibu wa mtanzania kama mtanzania unanafasi yake katika serikali yake [John Kennedy alipata kusema utaifanyia nini Serikali yako] kwa maana ya kuwa kila Mtanzania anawajibu wa kuijenga na kuilinda Nchi yake kupitia usimamizi wa Serikali inayomuuongoza chini ya uchaguzi wa chama anachokipenda aliofanya kupitia sanduku la uchaguzi kila baada ya miaka mitano.Kura yake ya uchaguzi ni DHAMANA [Wajibu] aliogharimia [Vesting] kwenda kwenye kikundi cha chama ambacho yeye anaimani nacho [Ingawa sio lazima sana kutumia vyama kunawezekana kutumia aina yoyote ya mfumo kupata serikali] ambacho kinateua mtu ambae anasimama kama Rais ambae anaunda Serikali kupitia chama chake kuunda mfumo utakao tawala vyombo mbalimbali vya umma na kusimamia ujenzi na ulinzi wa Taifa kama dhamana [vested] kwa niaba ya umma.

Hivyo wajibu wa umma ambae ni mtanzania kama nguvu ya mtu mmoja mmoja kuamua maamuzi ya jumla ukabidhiwa kwa kikundi cha chama teuliwa nakuwapa mamlaka ya kuamua na kutenda kwa niaba ya umma.

Hivyo tukilejea kwenye uhalisia wa upande wa pili ule wajibu wa mwananchi aliokabidhi kwa Serikali aliyochagua na kuweka kwenye kikundi cha chama kilichounda Serikali hakika wajibu huo sasa kwa tulipofika kama Taifa uko mashakani na una hatihati sana kuwa hautelekelezeki KIUKWELI na kuwa yanayojili mbele ya macho yetu kwa sasa na kuzua maswali magumu yenye majibu mepesi ni uthibitisho kuwa kuna tatizo.

Je tatizo tulilonalo ni sisi wananchi watanzania au ni la chama kilichopewa mamlaka ya kuunda Serikali yetu ndicho chenye tatizo.Kwa kuwa Baba wa Taifa alishasema kuwa CHAMA LEGELEGE UZAA SERIKALI LEGEGE.Kwa picha hiyo ya Baba wa Taifa kumbe hata dhamana ya UHAI wa Mtanzania nao UTAKUWA LEGELEGE.

TAFAKARI PIA.
 
DSN na Wana JF,
Umechambua vizuri na ni matumaini yangu wengi wetu tumesoma mada hii, tatizo letu kubwa ni kuwa wengi wetu hatujui wajibu na haki zetu kama Mtanzania na Tanzania yetu. Pili tu waoga sana na propaganda za uongo,uchonganishi, n.k.
Mungu ibariki Dunia, Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Nawakilisha

Back
Top Bottom