Ukitaka kufaidi pesa za wagombea urais, fanya hivi

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Sasa hivi wanaokusudia kugombea urais hasa kupitia CCM wanajitahidi kuzunguka kila upande kutafuta majukwa ya kuwatambulisha au kuwafanya wajulikane na hivyo kuonekana wanafaa.

Wengine wameshaanza kuzunguka na chopa, wengine makanisani, wengine wameandika vitabu, wengine wanajitahidi kuwa karibu na rais wakijidai wanamsaidia, wengine wanajifanya watakatifu eti wao wanachukiwa na mafisadi kwakuwa wanachukia ufisadi, wengine wameamua kuokoka, wengine wanajiunga na makanisa tofauti tofati, wengine wamekimbilia kwa wanafunzi, wengine kwa wamama nk.

Huko kote wanakozunguka wanatumia pesa na wameshaunda mitandao ya kuwapigia debe. Ndio maana tunaona Tshirt zimeandikwa "Friends of L, Team L nk.Sasa mbinu rahisi ya kufaidi pesa zao ni kwa wewe kama una ka NGO, Kanisa, SACCOS, msikiti, kituo cha yatima, kituo cha mateja waliostaafu, kuchangia ununuzi wa vyombo vya kwaya, uzinduzi wa albam,umoja wa wajane/wagane, boda boda group nk ni kuandaa shughuli ya kuchangisha pesa au harambee, au uzinduzi wa kajengo fulani ka kikundi chenu, kuweka jiwe la msingi hata kama hamtajenga na kisha kuwaalika wenye uchu na urais uone jinsi mambo yako yatakavyokwenda vizuri.

Katika shughuli hiyo usisahau kuwaita waandishi wa habari wa redio, magazeti, wapiga picha na watu wa televisheni kwani hawa uzuri wake watalipwa na ''mgeni rasmi'' mwenyewe. Ujue wengine wakiona hakuna waandishi wa habari wa kutosha huwa wanatoa udhuru.

Ukianza mmoja mpaka uwamalize wote, utakuwa kwa namna fulani umeuaga umasikini au kataasisi kako katakuwa kana sound.

Ukweli wagombea sasa hivi wanatafuta sana majukwaa ya kijamii msipo watumia sasa mtakuwa hamjawatendea haki. Hawa baada ya uteuzi hawatapatikana tena kwani watakuwa hawana wanachokitafuta kwani wengi watakuwa "best losers"
 
Mkuu umenifurahisha sana. Deal ya kula hela ya wasaka urais. Ukiwatazama wagombea unapata mashaka kama kweli wanania ya kusaidia taifa letu au madalali tu. Wengi wametumwa kuvuruga mchakato wa kupata mtu makini wa kutuondolea naadui wetu alowasema mwl JK.
Maadam hao ni madalali basi nasema hela yao iliwe kwa hiari na kwa nguvu.
Hatua ya kwanza ni kujipendekeza hadi kuwa karibu nao na kuchukua hiyo mihela ili ifanye kazi. Ijenge uchumi wetu na kulipa kodi.
Wanagawa mihela lkn hawawekezi ili kutia ajira wala kukuza uchumi wetu.
Ushauri wako uzingatiwe na hiyo heka iliwe haraka.
 
Back
Top Bottom