Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Pia kumbuka kukata bima kubwa si unajua tena ndio unaingia kwenye game na ajali haina kinga mdau hivyo once lolote likitokea unakuwa compensated na si kuanguka kwa pressure, sio mtaalamu sana kwenye hii business ila mwanzo unatakiwa uifuatilie kwa karibu sana ikiwezekana hata siku moja moja unajifanya na wewe kuendesha kama leseni yako inakuruhusu ila kwa style ya nia njema sio ya kumfanya mpaka dereva akushitukie kwamba unamfuatilia (hawa staff wa daladala pamoja na kwamba wengi wanaonekana ni wahuni wakati mwingine inatakiwa style flani ya kuwa-handle)

Jodoki K, asante sana. Nina jamaa yangu ambaye anafanya hii biashara Shinyanga. Miezi miwili iliyopita moja ya Hiace zake ilipinduka na kuuwa abiria wawili (askari) na kujeruhi wengine kadhaa. Bahati nzuri alikuwa amekata "CTP Insurance" na "Comprehensive Insurance" hivyo "liability" haikuwa kubwa sana. Huu ni ushauri mzuri sana.
 
Juzi juzi hapa nilikuwa kwenye daladala ya Aiport - Buhongwa, nikawa namtega dereva (maana nilikaa pale mbele karibu yake) kuhusu hii biashara ya Daladala (Express kwa MZA). Jamaa alifunguka vizuri sana akasema hii biashara inalipa sana kwa pande zote yaani kwa tajiri na wafanyakazi (dereva na konda). Akasema ukipata wafanyakazi waaminifu ndani ya miaka miwili unaagiza basi kubwa (hapo sikumwuliza kama ni MarcoPolo au Yutong), shida akasema inakuja unapokuwa na wafanyakazi wajanja hapo lazima itakula kwako. Kwa MZA alisema siku 1 wanaingiza mpaka 150,000/= na tajiri kati ya hizo anachukua 50,000 wao wanachukua 20,000/=, mafuta na matengenezo madogo madogo 80,000/=.

Pia jamaa alisema wangeweza kupata fedha zaidi ya hiyo kama wangekuwa wanaruhusiwa kupiga mzigo hadi saa 6 usiku. Kwa sasa hivi wanapiga kazi mpaka saa 3. Pia changamoto nyingine alisema kama unataka Hiace ni bora ukaagiza mpya kutoka Japan moja kwa moja (hapa alimaanisha kwamba kwetu ikitoka Japan ni kama mpya pamoja na kwamba kule imetumika). Hapa alisisitiza kwamba ukichukua zilizopo kwenye yards zetu hapa TZ nyingi huwa zimechakachuliwa gear box, huwa wanaweka za Mchina ile original wanaiuza kama spare part (shenzi zetu kabisa, wala hatufai - wizi mtupu). Ukipata original utapiga kazi kama kitu miaka miwili hivi bila shida yoyote wewe kazi yako inakuwa kufanya service tu zile za kawaida ambazo hazili pesa kubwa.

Mkuu kama umeamua piga kazi na jitahidi kusimamia kwa uakaribu zaidi inalipa!!!!!
 
Manjagata, asante sana kwa mchango wako. Naona, pamoja na uimara wa gari na uaminifu wa dereva na konda, umetukumbusha suala la makubaliano ya muda wa ufanyaji kazi. Vilevile tumepata habari "from the horse's mouth" kuwa biashara inalipa, kitu ambacho kinatia moyo. Hapo kwenye kijani, kama mlikuwa kwenye Hiace, nadhani alikuwa akiongelea gari kama Rosa, Civilian n.k. kwani kwa faida ya 50,000/= kwa siku, baada ya miaka miwili unakuwa na kama 36,000,000/= Yote kwa yote hii ni habari nzuri.
 
King Kong III, asante sana kwa mchango wako. Naona kwamba suala la dereva (na konda) bado linaendelea kuwa changamoto nambari moja. Nimefurahi kusoma ya kwamba kuna wadau wengine ambao wanataka kujikita kwenye biashara hii, ishara ya kwamba inalipa. Swali moja tu King Kong III: Unaposema ya kwamba una mpango wa kuisimamia mwenyewe una maana ya kwamba utakuwa dereva/konda mwenyewe au una usimamizi mwengine ambao ni "fail-safe" ?

Hapana sitakuwa konda wala dereve bali nitakuwa kama TT kwenye Train,Mda wote nipo kwenye siti ya mbele naangalia ujazo na mapato ya gari,pia naangalia uendeshaji wa dereva kama yupo rough(swerving swerving),Umakini wake bara barani etc nikifanya kihivyo ainauhakika sikosi 90k kwa siku baada ya makato ya malipo ya dereva na konda....
 
Hapana sitakuwa konda wala dereve bali nitakuwa kama TT kwenye Train,Mda wote nipo kwenye siti ya mbele naangalia ujazo na mapato ya gari,pia naangalia uendeshaji wa dereva kama yupo rough(swerving swerving),Umakini wake
bara barani etc nikifanya kihivyo ainauhakika sikosi 90k kwa siku baada ya makato ya malipo ya dereva na konda....[/QUOTE

Hii style yako sijui kama utapata dereva si bora uendeshe mwenyewe
 
Mimi nakushauri kama hujanunua hizo Nissan Mbili,nakushauri nenda kwenye tipper la Mchanga,Uki bargain vizuri unapata kwa 20,000$ CiF...unalaza 120,000 tsh kila siku ni sawa tu na hizo dala dala 2!...Dala Dala zinalipa ila kwa sasa na hizo kampuni,sijui itakuwaje!
 
Nimeipenda hii thread! Anonimuz hata mie nataka nifanye biashara ya daladala hapo mwakani ila nitafanyia hapa Arusha, ninaomba wadau mliomchangia huyu bwana mnichangie pia na mimi hasa kwenye aina ya hiace ya kununua: nisaidieni kwa hili
 
Wadau ninategemea kuanza kufanya biashara ya daladala, ombi langu kwenu ni aina ipi ya hiace inafaa zaidi hasa katika mazingira ya kwetu hapa Tanzania? Maana naona kuna Toyota, Nissan. Mazda mara 2L mara 5L. Nisaidieni wenye uzoefu wa magari haya
 
Hii biashara bana ina changamoto zake, ofcourse ni part ya biashara zangu kwa sasa.

Mimi naindesha hivi,
Ninazo 2, Nissan Civilian na Toyota Coaster, ambazo roughly nimezinunua kama kwa 50,000,000/= total

Kwa siku za wiki kila moja inaleta 80,000 x2 x5 = 400,000
Jumamosi ni 70,000 x 2 = 140,000
na Jumapili 60,000 x 2 = 120,000

Jumla 1,060,000 kwa wiki.

Matumizi yapo hivi.
Kila baada ya wiki 2 ni services ambayo gharama zake ni kama ifuatavyo.

Engine Oil Lita 20 = 96,500 (kila gari inakula 10Lita)
Oil Filter inaweza kua hata 36,000
Fundi 20,000

Matumizi ya kila mwezi
Msimamizi wa magari yote mawili 200,000

Hapa kuna matumizi mengine hayapo, yaani assumption ni kua kila kitu kiko poa. Hivyo sijaweka matairi, motor vehicle, TLB, bearing labda, Betrii, repair ya pasi ndogondogo n.k.

Msimamizi huyu ni mjomba wangu, na madereva + makonda katafuta yeye.

Hua napigaga tripu za kustukizia pale yanapolala kuangalia kama ni kweli yanalala saa 3-4 usiku. Maana yanaweza kua yanakesha wakakuulia gari.

Kifupi inanilipa kiasi,
Tafuta msimamizi, mlipe vizuri na jaribu kua nae karibu!!
 
Mimi sitoingia kwenye biashara yenyewe ila kwenye aina ya Gari.Kwakweli Nissan ni gari nzuri sana especially zeneye engine kubwa.Kikubwa ni kupata vipuri halisi,ambapo kwa hili Nissan naona wamefanikiwa sana kudhibiti kuliko Toyota.Kwani Nissan ukibadili spare,since it is genuine unasahau.
 
Wadau ninategemea kuanza kufanya biashara ya daladala, ombi langu kwenu ni aina ipi ya hiace inafaa zaidi hasa katika mazingira ya kwetu hapa Tanzania? Maana naona kuna Toyota, Nissan. Mazda mara 2L mara 5L. Nisaidieni wenye uzoefu wa magari haya

Kama unaweza basi epuka kununua gari lililotumika hapa Tanzania, linakuwa limeshapigika sana.

Kingine, kati ya hayo magari uliyotaja, yote ni ya Kijapan na yana sifa za ubora, na spea zake zinapatikana. Ila kuna mengine yana reputation za "roho ya paka" kuliko nyingine (2L vs Hiace "mayai.") Lakini sasa roho za paka hizo unakuta ni matoleo ya zamani sana (2L engine, kwa mfano), unakuta ni bora Hiace "Mayai" ya mwaka 2005 kuliko "Roho ya Paka" ya mwaka 1988, itakusumbua.

Lakini Mkubwa, bila kuku discourage, is this the only business you could get in?

Biashara ya daladala imekaa kienyeji enyeji mno. Huna tight control na biashara yako, utunzaji na matumizi ya assets zako uko mikononi mwa ma strangers, when I say strangers I mean hata huyo dereva wako half of the times sio yeye anaeendesha! Na ndio industry standards, ukisema hutaki "day waka" aguse gari zako unakwenda against the grain of the business kwa saab gari inaamsha saa kumi na moja inazima saa mbili, tatu usiku, dereva mmoja kila siku hawezi! Una deal na mafundi wa miembeni unprofessional, untrustworthy, mpaka unajikuta umeshinda kwenye ma gereji unasimamia ufundi. Una deal na ma security wa kwenye ma gas station zinakolala gari kuwahonga honga all the time wasiibe site mirrors au wasifanye kufuru kubwa zaidi "change quarter" (kubadilisha hata engine zima na usijue)!

Lakini kikubwa kibaya kuliko vyote katika biashara ya magari kwangu mimi, siku kibasi kikipata ajali polisi wanakung'ang'ania wewe mmiliki eti ukawaonyeshe dereva alipo! Wait a minute now, dereva kaingia mitini, na mimi pia nilikutanishwa nae barabarani (hakuna dala dala yenye ofisi Tanzania!) tumekutana Mtanzania mwenzangu ana vibali, ana reference ya ajira za nyuma, nimempa ajira, mapicha na makaratasi yake haya hapa, si ndugu yangu, simjui Mama yake, sijui dini yake, kama ambavyo professional employees wa maofisini wanavyoajiriwa wakiwa ma strangers waliojibu matangazo magazetini, kwa vitambulisho vyao na certificate zao na references of the last jobs wanakabidhiwa mali za ofisi, sasa konda au suka ameharibu ameingia mitini nang'ang'aniwa mimi nikamlete, nimpate wapi kama nyinyi polisi mliobobea kutafuta fugitives hamumuwezi? You know? Such a shambolic, perilous, unprofessional business.
 
Mimi sitoingia kwenye biashara yenyewe ila kwenye aina ya Gari.Kwakweli Nissan ni gari nzuri sana especially zeneye engine kubwa.Kikubwa ni kupata vipuri halisi,ambapo kwa hili Nissan naona wamefanikiwa sana kudhibiti kuliko Toyota.Kwani Nissan ukibadili spare,since it is genuine unasahau.
Ni kweli, although bei ya spares inazidi Coaster by far
 
Kama unaweza basi epuka kununua gari lililotumika hapa Tanzania, linakuwa limeshapigika sana.

Kingine, kati ya hayo magari uliyotaja, yote ni ya Kijapan na yana sifa za ubora, na spea zake zinapatikana. Ila kuna mengine yana reputation za "roho ya paka" kuliko nyingine (2L vs Hiace "mayai.") Lakini sasa roho za paka hizo unakuta ni matoleo ya zamani sana (2L engine, kwa mfano), unakuta ni bora Hiace "Mayai" ya mwaka 2005 kuliko "Roho ya Paka" ya mwaka 1988, itakusumbua.

Lakini Mkubwa, bila kuku discourage, is this the only business you could get in?

Biashara ya daladala imekaa kienyeji enyeji mno. Huna tight control na biashara yako, utunzaji na matumizi ya assets zako uko mikononi mwa ma strangers, when I say strangers I mean hata huyo dereva wako half of the times sio yeye anaeendesha! Na ndio industry standards, ukisema hutaki "day waka" aguse gari zako unakwenda against the grain of the business kwa saab gari inaamsha saa kumi na moja inazima saa mbili, tatu usiku, dereva mmoja kila siku hawezi! Una deal na mafundi wa miembeni unprofessional, untrustworthy, mpaka unajikuta umeshinda kwenye ma gereji unasimamia ufundi. Una deal na ma security wa kwenye ma gas station zinakolala gari kuwahonga honga all the time wasiibe site mirrors au wasifanye kufuru kubwa zaidi "change quarter" (kubadilisha hata engine zima na usijue)!

Lakini kikubwa kibaya kuliko vyote katika biashara ya magari kwangu mimi, siku kibasi kikipata ajali polisi wanakung'ang'ania wewe mmiliki eti ukawaonyeshe dereva alipo! Wait a minute now, dereva kaingia mitini, na mimi pia nilikutanishwa nae barabarani (hakuna dala dala yenye ofisi Tanzania!) tumekutana Mtanzania mwenzangu ana vibali, ana reference ya ajira za nyuma, nimempa ajira, mapicha na makaratasi yake haya hapa, si ndugu yangu, simjui Mama yake, sijui dini yake, kama ambavyo professional employees wa maofisini wanavyoajiriwa wakiwa ma strangers waliojibu matangazo magazetini, kwa vitambulisho vyao na certificate zao na references of the last jobs wanakabidhiwa mali za ofisi, sasa konda au suka ameharibu ameingia mitini nang'ang'aniwa mimi nikamlete, nimpate wapi kama nyinyi polisi mliobobea kutafuta fugitives hamumuwezi? You know? Such a shambolic, perilous, unprofessional business.

Asante sana kwa ushauri mkuu hasa changamoto zake ni ukweli kabisa nimefarijika na huu ushauri, nitaufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom