Ukistaajabu ya missenyi utaona ya.... Kasulu mjini

Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,559
1,272
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida wilayan kasulu sinto faham imeibuka miongoni mwa makaran wa sensa kasulu mjini kuhusiana na malipo yao pamoja na makato wanayo katwa makarani tshs=2500 ya chakula bila ridhaa yao huku wakilishwa wali maharagwe kwa kiasi hicho cha fedha. walipo muuliza MSIMAMIZI wa sensa kutoka ofisi ya takwimu Taifa alipo takiwa kutoa ufafanuzi juu ya makato ya chakula na idad ya siku za semina pamoja na mikataba alisema hafaham lolote kuhusiana na mikataba na siku za semina huku akibonyezwa na waratibu wa semina ambao inasemekana wameandaa mkataba wao ambao haupo sehemu yoyote Chakula wanacho toa kwa makaran kina thaman ya tsh=1500 hivyo wao kuwaibia wasimamiz na makaran wapatao 700 tshs=1000 kwa kila mwana semina hivyo kutengeneza faida ya laki 7 kila siku kutokana na makato hayo.
Baada ya kutokea sintofaham hiyo ilibid hali ya taharuki izuke kituoni hapo na kumfanya msimamiz huyo wa kitaifa kwa mkoa wa kigoma akimbie kituo hicho cha bögwe kwa kupitia mlango wa nyuma na kukimbia ikisemekana kahofia usalama wake
ilipo fika jana trh 18 maafisa usalama na watu wa takukuru kuja jion yake makaran wote waliambiwa semina imesitishwa kupisha idd halaf itaendelea baada ya idd na mpaka leo makaran hawajasain mikataba ya kazi

*my take msimamizi wa sensa tena kutoka ofisi ya taifa takwimu kusema hajui chochote kuhusiana na mikataba na posho je anaficha nini*
NCHI YANGU SERIKALI YANGU !
SOURCE: mimi mwenyewe eneo la tukio
 
unashangaa kukatwa 2500 kwa wali ndondo,njoo tmk hapa dar wanakatwa tshs 3000 na hawapati hawapati hata karanga ya tshs 100,kama unaona unaibiwa sepa aaarghhh...
 
Utasikia wamepewa onyo kali zidisha kwa siku laki 7 mara 11 idad ya ya siku za semina kweli tanzania ni zaid ya uijuavyo
 
Hii nchi kila, mtu akipata gap anataka aibe tu!!!!! Udhaifu tu ndo unaosababisha haya yote!
 
Hao usalama na TAKUKURU ni walewale, wao wamepewa fungu lao wakaja kutuliza upepo. Yani nawachukia sana hawa watu. Ipo siku nitahama tz. Mzururaji msikubali kuonewa
 
Sawa mjomba mwandiga wakiona unajitambua watalekebisha kitu kitasoma
 
Hasira ya uchafu huu wanaowafanyia,muipeleke kwenye uchaguzi 2015. Naskia hii semina wanaunganisha na masuara ya vitambulisho.baadh ya vituo ili suara la nida wamelikataa. Leo walikuwa walipwe pesa ila longolongo kibao. Jion híi tutapata habari kamili juu ya kilichojili apa kasulu
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida wilayan kasulu sinto faham imeibuka miongoni mwa makaran wa sensa kasulu mjini kuhusiana na malipo yao pamoja na makato wanayo katwa makarani tshs=2500 ya chakula bila ridhaa yao huku wakilishwa wali maharagwe kwa kiasi hicho cha fedha. walipo muuliza MSIMAMIZI wa sensa kutoka ofisi ya takwimu Taifa alipo takiwa kutoa ufafanuzi juu ya makato ya chakula na idad ya siku za semina pamoja na mikataba alisema hafaham lolote kuhusiana na mikataba na siku za semina huku akibonyezwa na waratibu wa semina ambao inasemekana wameandaa mkataba wao ambao haupo sehemu yoyote Chakula wanacho toa kwa makaran kina thaman ya tsh=1500 hivyo wao kuwaibia wasimamiz na makaran wapatao 700 tshs=1000 kwa kila mwana semina hivyo kutengeneza faida ya laki 7 kila siku kutokana na makato hayo.
Baada ya kutokea sintofaham hiyo ilibid hali ya taharuki izuke kituoni hapo na kumfanya msimamiz huyo wa kitaifa kwa mkoa wa kigoma akimbie kituo hicho cha bögwe kwa kupitia mlango wa nyuma na kukimbia ikisemekana kahofia usalama wake
ilipo fika jana trh 18 maafisa usalama na watu wa takukuru kuja jion yake makaran wote waliambiwa semina imesitishwa kupisha idd halaf itaendelea baada ya idd na mpaka leo makaran hawajasain mikataba ya kazi

*my take msimamizi wa sensa tena kutoka ofisi ya taifa takwimu kusema hajui chochote kuhusiana na mikataba na posho je anaficha nini*
NCHI YANGU SERIKALI YANGU !
SOURCE: mimi mwenyewe eneo la tukio
Wewe wayasema ya Kasulu wakati huko Mza hali ni hiyohiyo.Nchi haina sheria kila mtu anaamua atakavyo kama sheria zingekuwepo suala nyeti kama hili la sensa lisingefanyiwa mzaa.
 
Huku mufindi nako mambo yapo hovyohovyo makarani wamelazimishwa kupewa rejesta za nida bila hata kuambiwa watalipwa nini wameambiwa wakilipwa washukuru wasipolipwa hewala. Nako mambo yalikuwa ya kuvutana kukatwa hiyo 2500. Swali hiyo gharama ya chakula iweje iwe sawa nchi nzima?

Hii sensa ni kizungumkuti vifaa tumeambiwa havjafika sasa sijui itakuwaje Tanzania sijui tunakwenda wapi Serikali yetu inajambo gani la kujivunia kama kila kitu mizengwe?
 
Baada ya kusimamisha shiling kwa muda mref 2meshinda wame2lipa stahiki zetu zote buhahahaaaaaaa
 
Back
Top Bottom