Ukisikia Pinda ni mnafiki ona sasa haya

nataka niwe objective kidogo hapa. Tundu Lissu alimtaja Kafumu kuchukua posho zile. Ni wazi alijua kuwa naye Makinda na Pinda walilamba. Mbona hakuwalipua pale? Hii tuiweke vipi?
.
Haya mabomu hayalipuki yenyewe yanapangwa namna ya kulipuka. Hilo la Pinda na Bi kiroboto hapo lilipolipukia ndo mahala pake.
 
Haya mambo ya kulindana ni matumizi mabaya ya uongozi bora kwa nchi.lazima viongozi mfike mahali muone huruma na mjinasue katika limbi hili la ulevi wa madaraka na kujilimbikizia hela za watanzania.kumbuka hata ukijenga majumba na kusheheni magari vyote mtaviacha hapa hapa duniani kama baba wa taifa.heshima ya kiongozi ni uongozi bora na uongozi bora ni matokeo bora kwa maendeleo ya wananchi
 
Nimesoma ripoti ya kamati teule kuhusiana na sakata la kitundu Jairo. "Waziri Mkuu" imeandikwa kama mara 67(Sitini na Saba) hivi. Hakuna mahali inaposemwa kuwa na yeye ni mnufaika au hata kusema alipokea je bila kuhoji. Je, kamati teule nayo imechakachua ukweli kuhusu hili?
 
Tusimlaumu Pinda bali tujilaumu sisi wenyewe tunaopenda kuaminishwa mambo bila kujibu. Yeye alipojiita mtoto wa mkulima basi na sisi tukaamini hivyo bila kuhoji na tukiendelea hivi kuna mtu ataibuka na kujiita mtakatifu tutaamnini. Msafi hajawahi kuwa ndani ya CCM ya Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete kama wenyeviti. CCM safi aliondoka nayo Mwalimu 1985 na akafa nayo mwaka 1999 ndipo kina Kingunge kwa ulghai walichukua mradi wa kituo cha mabasi na kuegesha magari, Mkapa wakafanya biashara ikulu na jk akaasisi EPA, Buzwagi, Richmond na miradi ya mafuta na usafirishaji kwa mgongo wa mwanae.

Pinda kuwa safi ni kichekesho cha mchana. Yeye ndiye secretary of procurement unit wa wizara yake. Mashangingi kabla ya kununuliwa yanaidhinishwa na yeye. Sasa mpaka shangingi linafika yeye ndio anakuja kulikataa kisa Mbowe alikataa shangingi. Yeye anao uwezo kisheria na kiplotocal kukataa ununuzi wa mashangingi kwa serikali kama atadhamilia kama alivyofanya mahufuri kuhakikisha magari yote ya serikali na mashirika ya umma yanapata namba kabla hajawa mtu wa ajabu na kuuza nyumba za serikali kwa wakubwa na kimada wake. Hivyo tusishangae pinda kuchukua mtama huo maana hata utetezi wake kwa posho za wabunge ulidhihirisha tamaa zake kwa kisingizio cha kuwapa wapiga kura wake sijui wanasafiri saa ngapi toka sumbwanga kudai posho.

Ukishaamua kuwa CCM basi credibility na integrity yako inakuwa questionable. waadilifu mlioko huko njoo vyama vingine hata TLP inaweza kuokolewa isiwe CCM C kama CUF ilivyoamua kuacha kuwa chama cha wananchi nan kuwa CCM B
 
Nimesoma mwanahalisi la leo kumbe Pinda na Makinda nao walisaini pesa za jairo ili hali wenyewe serikali inawalipia kila kitu.

Hao wawili walisaini kila mmoja 280,000 kwa kikao kisichozidi dakika 40. Sasa huyu ndo yule aliyekataa shangingi na ndio maana alikuwa mstari wa mbele sana kutetea bajeti huu ni uhuni sana!
Sasa ninathibitisha kuwa CC Magamba yote mijizi!! na wanaowashabikia ni mataahira kabisa. Faiza fox, Mbopo, comment please
 
Tukitaka kuwa wakweli January Makamba anaweza kuwa miongoni mwa wana CCM wachache sana makini waliobaki.
 
Nimesoma mwanahalisi la leo kumbe Pinda na Makinda nao walisaini pesa za jairo ili hali wenyewe serikali inawalipia kila kitu.

Hao wawili walisaini kila mmoja 280,000 kwa kikao kisichozidi dakika 40. Sasa huyu ndo yule aliyekataa shangingi na ndio maana alikuwa mstari wa mbele sana kutetea bajeti huu ni uhuni sana!

Wamevunja sheria gani? Msipayuke tu kaa walevi.
 
Tukitaka kuwa wakweli January Makamba anaweza kuwa miongoni mwa wana CCM wachache sana makini waliobaki.
Hana lolote.
Kama sheria ina-demand alipwe basi anayo kesi ya kujibu au angechukua akapeleka kwa charity groups, kuna watoto hawana madaftari /vitabu/ada etc..
 
Lowasa ana afadhali mara million kuliko wanafiki walioko CCM wakiongozwa na Pinda, Makinda & co.
 
Leo ndio mnaelewa? hivi watu tunapodai posho ziondolewe bado hamfahamu athari zake?
Mchezo huu upo bungeni miaka yote toka vyama vingi kuanza na zaidi ya hapo mbunge baada ya kumaliza muda wake hulipwa kiinua mgongo cha millioni 100. Piga hesabu kwa Wabunge karibu 400 na utaweza vipi kushinda na mbunge mwenye millioni 100 mkononi kwa ajili ya awamu nyingine.... Kwa kazi gani ikiwa miswada inapitishwa mpende msipende kwa faida yao wenyewe..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom