Ukisikia Pinda ni mnafiki ona sasa haya

Johnsecond

JF-Expert Member
May 4, 2010
1,076
211
Nimesoma mwanahalisi la leo kumbe Pinda na Makinda nao walisaini pesa za jairo ili hali wenyewe serikali inawalipia kila kitu.

Hao wawili walisaini kila mmoja 280,000 kwa kikao kisichozidi dakika 40. Sasa huyu ndo yule aliyekataa shangingi na ndio maana alikuwa mstari wa mbele sana kutetea bajeti huu ni uhuni sana!
 
If this is true then we have a huge mountain to climb. I guess Jairo & CO will be free in this issue though not ASAP.
 
Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa mungu, CCM hakuna msafi hata mmoja
 
hii ndo tanzania bwana! Pesa mbele vingine baadae, ni nani atafungwa? Labda ccm nzima.
 
Unashangaa nini mkuu?

Ulishaambiwa hakuna mtu msafi katika serikali na CCM kwa ujuma wote wachafu.

Ukianza kupekenyua unaweza kufa kwa presha wote wale wachafu wanazidiana tu huyu kasaini 280,000/= wkt Ngeleja kasaini milioni 4.
 
Mwanahalisi katoa screen shot ya karatasi waliyo saini hizo pesa harafu jina la January Makamba linaonekana limefutwa yaani limekatwa na mstari. Dogo anaonekana aliona mbali sana. Mwanahalisi la leo limenifurahisha sana. labda niwape heading msiokuwa dar
1. Kubenea - Ikulu aibu tupu - ndo ile ya akina pinda sasa
2. Gamba lamponza kikwete
3. Dr Slaa uso kwa uso na JK
4. CCM wamekosea kumshika matiti binti yao
5.Rekodi ya aibu ikulu - hii kali sana nayo
6. Kikwete , Luhanjo, jairo ni zimwi likujualo halikuli likakwisha
 
Wote wang'oke, hakuna msafi pale CCM wala serikalini! Hata mtoto wa mkulima naye yupo? Kweli watanzania tunapaswa kuimwaga serikali ya CCM, no way tutapata maendeleo chini ya majambazi hawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la raia mwema la novemba 23 yenye kichwa cha habari "Pinda, Makinda, wavuta za Jairo" imechapishwa fomu ya malipo ya jumla ya sh 1,120,000/= kwa viongozi wanne huku jina la Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini January Makamba likiwa limekatwa. Kwa mujibu wa jedwali January alipaswa kupokea 280,000/= lakini hakuzipokea. Mimi naanza kuamini kwamba kauli za January ni kielelezo halisi juu ya imani na msimamo wake kwenye maswala yenye maslahi kwa taifa na je tuna vijana wangapi ndani ya CCM wanaoweza kufanya anayoyafanya January?

GZ
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom