Ukishangaa ya uvccm utaona ya lipumba na hamadi rashid

Hamad Rashid: Kweli wewe leo umekuwa wa kuponda chama cha upinzani?? Umesahau kuwa ulishawahi sema kuwa "hamuwezi kuwwachia nguruwe wale peke yao shamba lazima mle wote!!!!.

Au unataka nafasi kwenye serikali ya mapinduzi, maana kama nakumbuka vizuri huna nafasi yoyote. Tutamwambia Maalim Seif akukumbuke eh baba. Tushajua tatizo lako.
 
Jamani mie nauliza: Hivi hizi habari za Prof na Hamadi Rashidi kuisemea CCM dhidi ya Chadema mbona huwa sizisikii katika vyombo vya habari? Huwa zinaandikwa kwenye magazeti yepi, na katika kurasa zipi?

Kama yapo magazeti huziandika basi labda huzificha katika kurasa za ndani!!! Na kurasa za ndani ndimo wahariri wa magazeti wanaona panawafa
Ni aibu kubwa wanayofanya viongozi hawa wakuu wa CUF na mtu kama Hamadi Rashidi anasahau usaliti aliofanya kwa Wapemba wenzake miezi michache tu baada ya mauaji ya wafuasi wa CUF kwa risasi za polisi wa CCM pale alipokubali uteuzi kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Mkapa.

Hiyo ilikuwa ni hongo kutoka kwa Mkapa kwamba Hamadi afunge domo lake -- asilalamike sana kuhusu mauaji yale! Kweli kumtumikia Bwana ndiko huku?

soma habari leo na blog ya mjengwa hizo ndiyo zimejaa hayo maneno , nafikiri huwa wanatumiwa hizo taarifa wao tu, hata gazeti la uhuru haliwezi andika upuuzi huu, shame to CUF and shame to professor
 
Yuko bwana mmoja ni kati ya wanachama waanzilishi wa CUF kanieleza kuwa sasa hivi anaona aibu kujitambulisha kwa watu wengine kuwa yeye ni mwanachama wa CUF kwa jinsi chama chao kilivyopoteza mwelekeo na kukubali kutumika kijinga na CCM. Sasa hakuna ungangari wamebaki na ulainilaini tuu
 
Jamani hawa CUF mbona wanaelekea kufa kifo cha aibu,yaani wameolewa na CCM kwa ndoa ya mkeka lakini hawatulii au wanataka kuolewa,habari yao kwisha kabisa.
 
cuf sasa wamesilimu rasmi na kuwa ccm "b" siamini maneno ya hamad rashid na prof. Lipumba kama kweli wao waliopeleka watu katika maandamano ya jan 21 leo wanasema wenzao ni wahaini? Hapa watz tujifunze kwa hili, wanasiasa wa bongo sio wa kuwaamini kabisa. Sitoshangaa kuwaona lipumba na hamad wakicheza muziki wa tot kama mrema pale dodoma ktk mkutano mkuu wa ccm.

poleni sana cuf, ndio jeneza lenu hilo.... Hatudanganyiki tena!!!!:tongue:


no thank you sir!
 
Mimi nadhani CUF wako sahihi sana,
Naona chadema ndio wamelianzisha,wamewatukana cuf kanda ya ziwa,wamesema cuf ni mke wa ccm n.k.
Hali halisi katika siasa mwenzio akikutukana nawe mtukane au kaa kimya ufe kifo cha mende,mimi nimewasikiliza cuf juzi-wana hoja za msingi sana kuwaeleza wananchi,nadhani ni muhimu chadema iachane na hizi siasa za kuiparamia cuf kila kona,na kama cdm wataendelea kuwatukana cuf ni muhimu cuf wakajibu mapigo na hivyo ndivyo siasa inakuwa .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom