Ukipiga Simu Huku Unaendesha Gari Unatozwa 200,000 Hapo Kwa Hapo.

KKN wewe unapendekeza faini iwe kiasi gani? Mimi nadhani labda iwe 40,000.

Nakubaliana na wewe kabisa kwa kiwango hicho kuwa hapa UK ambako uchumi wake uko juu sana kulinganisha na nyumbani, faini ya kosa kama hilo haizidi pound 60!

Lakini bado najiuliza polisi wametumia vigezo gani ku arrive kwenye hiyo figure? As far as I know, ajali nyingi bongo zinasababishwa na 'drink drive' na wengi mtakubaliana na mimi kuwa very little is being done to stop this. Nenda Rose Garden, Brake Point au Makumbusho Ngwasuma ikipiga uone jinsi car parks zilivyojaa- and almost 90% ya wenye magari wanakanyaga mtungi kwa kwenda mbele bila kujali and no one cares,inaonekana ni kitu cha kawaida tu!

Bado kuna tatizo la watu kuendesha magari barabarani wakati hawajui sheria hata kidogo, na hili kwa kiasi kikubwa nitawalaumu polisi kwa kuwa ukiwa na hela yako hata kama hujui kuendesha- utapata leseni! Ukivunja sheria ukitoa rushwa- unaendelea na safari yako! Bado kunamadereva kibao wanaondesha daladala na mabasi ya kwenda mikoani kwa kutumia leseni feki na polisi wanajua hili!

And mbaya zaidi Rais mwenye kila ikitokea ajali mbaya ya barabarani, badala ya kuja na mikakati ya kupunguza ajali hizi -anaishia tu kusema 'ajali haina kinga', 'kazi ya mungu haina makosa'!
 
Nakubaliana na wewe kabisa kwa kiwango hicho kuwa hapa UK ambako uchumi wake uko juu sana kulinganisha na nyumbani, faini ya kosa kama hilo haizidi pound 60!

Lakini bado najiuliza polisi wametumia vigezo gani ku arrive kwenye hiyo figure? As far as I know, ajali nyingi bongo zinasababishwa na 'drink drive' na wengi mtakubaliana na mimi kuwa very little is being done to stop this. Nenda Rose Garden, Brake Point au Makumbusho Ngwasuma ikipiga uone jinsi car parks zilivyojaa- and almost 90% ya wenye magari wanakanyaga mtungi kwa kwenda mbele bila kujali and no one cares,inaonekana ni kitu cha kawaida tu!

Bado kuna tatizo la watu kuendesha magari barabarani wakati hawajui sheria hata kidogo, na hili kwa kiasi kikubwa nitawalaumu polisi kwa kuwa ukiwa na hela yako hata kama hujui kuendesha- utapata leseni! Ukivunja sheria ukitoa rushwa- unaendelea na safari yako! Bado kunamadereva kibao wanaondesha daladala na mabasi ya kwenda mikoani kwa kutumia leseni feki na polisi wanajua hili!

And mbaya zaidi Rais mwenye kila ikitokea ajali mbaya ya barabarani, badala ya kuja na mikakati ya kupunguza ajali hili -anaishia tu kusema 'ajali haina kinga', 'kazi ya mungu haina makosa'!

Naam polisi wanachangia sana katika ajali za barabarani. Huwa nashangaa sana ninapofahamu jamaa wengi ambao wana magari yao lakini wanaona hakuna umuhimu wa kuwa na leseni!! Ukiwauliza sasa ukikamatwa bila leseni huoni kama ni tatizo kubwa hilo!? Hapa nitacheza na polisi labda zitanitoka elfu kidogo halafu mchezo umekwisha!!!! Kweli ndiyo mambo ya Bongo hayo!! inasikitisha lakini ndiyo hali halisi.
 
polisi wetu ndio wenyewe kwa kukurupuka,sasa wanatunga sheria wao badala ya bunge?yaelekea polisi wetu hawaelewi tofauti ya sheri na kanuni,mambo magumu yanawasumbua wizi wa magari umerudi kama zamani uporaji pia wamekaa kimyaaa wameamua kutokea hapo wapuuzi kweli
 
Achilia mbali hayo ya upumbavu wa polisi, fikiria tu je utajisikia vipi kama utaua mtu kwasababu ulikuwa unaongea kwenye simu huku unaendesha gari?

Mambo mengine cha kuangalia si adhabu unayoweza kupewa bali majuto ambayo unaweza kuyapata na kusababisha kwa familia zingine kwa kushindwa kufuata sheria. Unaweza kupata hizo pesa na kulipa faini, lakini ukiua mtu, familia watakuwa wamepoteza ndugu maisha yao yote.

...wewe mtz naona unaleta fear technic kuhalalisha upuuzi huu,na wala hakuna mtu anabisha controlling cellphone user while driving maana ni hatari wote tunajua,ila kitendo cha mtu mmoja kuja kukurupuka na kutuwekea sheria bila kufuata utaratibu na kutuwekea laki mbili kama fine bila vyombo husika naona ndio hatari kuliko hao madereva wanaotumia cellphone
 
Polisi hawajajua tatizo la ajali linatokana na nini? Hizi ni janja za kujitengenezea rushwa. Jee serikali itacontrol vipi pesa zinazolipwa? Kwanza kabla ya kuunda sheria kuna fact gani zinazo support maamuzi? Jee ajali ngapi zimesababishwa na madereva wanaongea na simu?

Tangu lini Jeshi la polisi likatunga sheria? Jee wapi check and balance ndani ya nchi? jee katiba inalipa jeshi la Tanzania nguvu ya kuunda sheria? Jee kama ni hivyo sheria ilijadiliwa na kina nani? na nani waliipitisha?

I think aliyetoa hilo shauri ni mwehu.Nafahamu kabisa kuendesha na kuongea na simu ni hatari, lakini sidhani kama kisheria jeshi linaweza kutunga sheria.We need to be the nation of law, but not like this
 
Bw. James Kombe na SUMATRA, watu ambao tulitegemea waijue na kuifuatilia pamoja na kuishauri serikali katika masuala ya Marine and Land Transport wametulet down vibaya.

Tabia ya watu kukurupuka na kujitungia sheria kila wanapojisikia ni mbaya na inafaa ipingwe kwa nguvu zote. Tumeona haya kila yanapotokea majanga.

We need to be proactive rather than reactive. Ukurupukaji haufai. Nimejaribu kuipitia Transport Licencing Act ya 1973 na hakuna hata sehemu moja inayozungumzia Licencing Authority kushughulikia TRAFFIC OFFENCES, fun enough on SUMATRA's website napata haya:-

Functions of SUMATRA include:

(e) Liasing with Police, Ministry of Public Safety and Security and Ministry of Infrastructure Development on issues affecting road transport.

(f) Developing rules and regulations in Road Transport.

(g) Regulating tariff and charges. (zipi? Za traffic offence au ?)

Hapa naona kuna tatizo, katika act iliyoiunda hii SUMATRA ambapo function haiko very specific hivyo kuwapa mwanya wa kuprobe kujua ukomo wa nguvu zao. Ile statement ya Kombe inaonyesha bado hawa SUMATRA hawajui ukomo wao au Kombe alikurupuka. Nahisi huyu Kombe alikurupuka kwani SUMATRA wangetangaza wenyewe, kitu ambacho hawawezi kwani sheria haiwapi nguvu hiyo.

Wanasheria wetu humu hebu tusaidieni kabla Wakurupukaji hawajatufilisi na faini zao wanazojitungia...
 
Back
Top Bottom