Ukipangiwa kazi kigoma tarajia kukutanan na haya

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Wana Kigoma wanadai kua Mtu akipangiwa kazi Kigoma ana goma kuja kufanya kazi, akifanikiwa akaja kuanza kazi basi atagoma pia kuhama.
Wanadai kua ukishakula kichwa cha samaki maarufu Kigoma anaitwa MGEBUKA pamoja na dagaa wa Kigoma basi hutoki Kigoma.
Baadae wanamalizia kwa kukupa mke kutoka eneo maarufu linaitwa UJIJI hapo ndo hutoki kabisa yaani ndugu zako wataletewa tu taarifa baada ya kufa.
 
si kweli mbona nimefanya kazi pale miaka mitatu na nimetoka pale, huo ni uzushi tu...
 
umenifurahisha sana na umenikumbusha mbali! mwaka jana nilikuwa Kigoma kikazi pia, mwenyeji wangu akawa anaongelea sana hao migebuka, nikawa najiuliuza , huyu ndiyo mnyama gani, ilipofika Lunch time ndio akanipeleka kwenda kula hao migebuka, ni watamu kweli!!

Ila hilo la kupewa mwanamke itabidi nilifanyie uchunguzi wa kiundani zaidi!
 
Wana Kigoma wanadai kua Mtu akipangiwa kazi Kigoma ana goma kuja kufanya kazi, akifanikiwa akaja kuanza kazi basi atagoma pia kuhama.
Wanadai kua ukishakula kichwa cha samaki maarufu Kigoma anaitwa MGEBUKA pamoja na dagaa wa Kigoma basi hutoki Kigoma.
Baadae wanamalizia kwa kukupa mke kutoka eneo maarufu linaitwa UJIJI hapo ndo hutoki kabisa yaani ndugu zako wataletewa tu taarifa baada ya kufa.

Kaka wacha fix!!!!!!! Ukifika KGM utakachoku tananacho ni usumbufu wa usafili kurudi mikoa ya mashariki tu, manake bei ya nauli ya mabasi Balaaa! na barabara ni vumbi. Tren inasua sua.
 
Back
Top Bottom