Ukiondosha kuunganishwa kwa kiswahili na muungano; kuna jambo gani jengine ambalo watz tutajvunia?

Makame

JF-Expert Member
Jan 3, 2008
512
60
Taifa linajiandaa kusheherekea miaka 50 ya uhuru, kilele chake ni tarehe 09/12/2011. Mimi binafsi kwa haraka naona mafanikio mawili tu

1. Kiswahili kuwa lugha ya kutuunganisha.
2. Muungano [Ambao wenyewe; kuna wasioutakia kheri].

Mengine kusema ukweli imekuwa ni mtihani. Mfano

1. TAZARA - Ni mafanikio, lakini imefisidiwa. Wachina wakituona tunavyohangaika na wametuwekea reli ya kiwango cha juu, wamepasua milima; wanasikitika mno. Ndio maana wanajenga Angola kwa kasi kubwa.

2. Reli ya Kati na Kaskazini, tumeua.

3. Elimu - Mtihani, mtu anamaliza chuo hawezi andika sentensi, wachilia mbali barua. Tumeshindwa kusomesha proportion ya watu wetu ukilinganisha na Nchi zilizokuwa katika mfululizo wa misukosuko.

4. Azimio la Arusha - Failed. (Including nationalization)

5. Denationalization - faile - ATC, TRL you name it!

6. Kila kitu kina fail, mpaka multi party ina fail -----wana CDM kila wakizidiwa; wanatoka Ukumbini.

Huyo mchawi aliyeiroga nchi hii atakuwa marehemu, amekufa bila ya kuondoa aliyotujaribia.

Wana Forum; hayo ni mawazo yangu; sijui ya kwenu.

Pengine mafanikio makubwa yapo; lakini sijayajua. Munielimishe.
 
Kiswahili mbona hata Warundi na Wakongomani wanaongea?
Mimi sioni kinachoendelea kwenye muungano huu zaidi ya
watu fulani kuwanyonya wengine.

Shameless country!
 
Tumefanikiwa kuwa na Demokrasia ya Vyama vingi na Utawala wa Sheria
Tumefanikiwa kugomboa nchi za Afrika kutoka kwa wakolono
Tumefanikiwa kutatua migogoro yetu ya ndani pasi na kuingiliwa.
tumefanikiwa kutatua migogoro ya majirani zetu
Tumefanikiwa kumtoa nduli amin
Tumefanikiwa kuwa na taasisi zenye heshima
 
Tumefanikiwa kuwa na Demokrasia ya Vyama vingi na Utawala wa Sheria
Tumefanikiwa kugomboa nchi za Afrika kutoka kwa wakolono
Tumefanikiwa kutatua migogoro yetu ya ndani pasi na kuingiliwa.
tumefanikiwa kutatua migogoro ya majirani zetu
Tumefanikiwa kumtoa nduli amin
Tumefanikiwa kuwa na taasisi zenye heshima


Taasisi gani wewe, naomba uitaje.
 
Taasisi gani wewe, naomba uitaje.

National Institute For Medical Research.
Tanzania Persticides Research Institute.
National Electoral Commission.
Ile ya HOSEA siitaji; kwa sababu ina madudu yake. Inapaswa ifanyiwe ukarabati.
MOI.
Nk kwa upande wa Serikali

Lakini pia kuna taasisi za sekta binafsi.

Tumefanikiwa kuwa na Uhuru wa vyombo vya habari na wa kuabudu. Mzee Mwinyi alisema 'Hata kama mtu ataamua kula chura -RUKSA' ili watu wafanye watakacho kwa kuzingatia sheria ya Nchi.

Tanzania ni NCHI huru
 
Back
Top Bottom