Ukimya wangu!

Mtoto una vijineno weye, kama kurumbizi!

Japokuwa hii sio simulizi,Nashukuru sana laaziz
Huu ni msimu wa sisimizi,ni vizuri ukivaa shumizi
Wapo waliokuja na kizizi,kukukaribisha hawana ajizi,
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko.
 
Zinduna na Heart

mwanivutia maneno hadi na picha
nilitaka kukacha lkn sasa nimefika

Mtu chake mtu chake,usitake nikukate mtama
Mie sio wa chakechake,ni wa hapa hapa daresalaama
Kama unatafuta mke,sisi tuache kwa wako usalama
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko
 
kuna kadem flani kafupi short cheses nilikutana nako kibondo pale sankere lodge wakati nilipoenda kufanya kazi huko sijui ndo wewe?? Make nako kanaitwa zinduna..kachesh kinyama..
 
Mtu chake mtu chake,usitake nikukate mtama
Mie sio wa chakechake,ni wa hapa hapa daresalaama
Kama unatafuta mke,sisi tuache kwa wako usalama
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko​

Jamani Heart..wala usihofu
nimekuona wewe...ila kwa zinduna mm kipofu
natoka kivu..mpk bandari ya salama
 
Jamani Heart..wala usihofu
nimekuona wewe...ila kwa zinduna mm kipofu
natoka kivu..mpk bandari ya salama

Sio kwamba nalia,nina machozi ya furaha
Kama zinduna karidhia,basi mchukue kwa raha
Mimi hilo nimefurahia,sisikii kinyongo wala karaha
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko
 
Sio kwamba nalia,nina machozi ya furaha
Kama zinduna karidhia,basi mchukue kwa raha
Mimi hilo nimefurahia,sisikii kinyongo wala karaha
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko​
wala bado hajaridhia..ndio kwanza namlilia
dua yako iwe ya heri..kilio changu kusikia
zinduna uko wapi..au ndio umenunaa
 
Kimya changu, hakika kinamshindo,
Msijedhani nikimya, milele hata dahali,
Kuwa kwangu kimya, ni sawa na ada ya mja,
Ukimya wangu

Ada ya mja hunena, walisema wahenga,
Kwa muungwan ni vitendo, walimalizia malenga,
Kukaa kwangu kimya, hakika ni uungwana,
Ukimya wangu
Karibu zinduna.
 
wala bado hajaridhia..ndio kwanza namlilia
dua yako iwe ya heri..kilio changu kusikia
zinduna uko wapi..au ndio umenunaa

Sijanuna wallahi, na katu sitonuna
kuinunia bahati, ya mtende, na simchongoma,
kwa weye mtu chake, karibu kwetu chakechake
nimekupenda wallahi, lete posa tapokelewa
 
Back
Top Bottom