Ukimya wa upinzani katika Matukio yanayotokea nchini, kulikoni?

Tofauti yako na yule bi mkubwa aliyekuwa akilia barabarani kuwa kitabu cha allah kimedhalilishwa ni kwamba wewe unajua typing.

Sasa CHADEMA wameshindwa nini?

Na najua mlikuwa na hamu kweli kweli CDM waseme kitu, ndio kwanza Dr.Slaa yuko Shinyanga anakamua M4C kwenda mbele. Majungu yenu na ujinga ni mzigo kwa Taifa

Nasikia yule ninja aliyelia barabarani siku ile ni dadake ZOBA! alituchekeshaje! kama jini juha vile, manake kilikuwa kituko kulia kivile hahahhahahahah!
 
Mi naomba mheshimiwa akitoka oman alikoenda kutembea aitishe mkutano na wazee wa dsm km anavyofanyaga siku zote kunapokuwa na matukio mabaya kwa nchi. Maana wazee wengi wanaohuzuriyaga vkao ni waislam. Watapeleka aman kwenye misikiti yao. Baada ya kikao.
 
Hivi kwanini sisi hatutaki kuzipa ushirikiano akili zetu?

-Wapi CHADEMA waliweka mkataba na wananchi kuhusu mustakabali wao wa Taifa, kuhusu amani na utulivu?

-Okay, Let's say wametoa tamko, halafu?

-Wakati wakiwa wanatoa "tamko", Serikali inafanya nini? ---Kama wananchi Tunafanya nini?

-Hili suala chanzo chake ni mambo ya kidini, so litasuluhishwa kwa njia za kidini! CHADEMA,au chama chochote cha siasa kuongea (kwa watanzania sisi wenye kuwa na ugumu wa kuzishughulisha akili zetu tutasema, Chama fulani kipo nyuma ya jambo hili)..Acha nao(Hao CHADEMA)wajisafiahe kwa njia hiyo, maana kila vurugu wao ndio wamesababisha!

Kwani siyo serikali hii hii, ilikuwa iko tayari kuingia vitani kwa gharama yeyote kwa ajili ya mpaka?..Ikisema "NGUVU ipo"!!?..Kwanini nguvu hiyo hiyo isitumike kuwadhibiti hao waandamanaji(bila ulinzi), ina maana haiwajui?

Rais yuko wapi?Makamu wake? W/mkuu? Waziri wa Mambo ya ndani? Waziri wa Ulinzi? Wasaidizi(Manaibu) wao? Mkuu wa Jeshi la Polisi?..wao wamefanya nini?
Hawajui?

Si kila jambo huitaji mazoea, tufanye wajibu wetu kila mtu kwa nafasi yake.
 
cdm wanatoa matamko kila siku lkn wanaishwa kupuuzwa waliongea tokea mauaji ya mwangosi bt nothing has been done xa we unatka waseme nini tena wakati wanapuuzwa kila siku
 
embu m solve tatizo la udini mlilolianzisha mkimaliza na la ukabila litakuja, si mlidhani mnaikomoa chadema?
 
Hizi akili za Madrass taabu tupu! Dunia ndivyo ilivyo tutaendelea kuwaelimisha bila kuchoka.

Kama Matatizo ya Waislamu yametokana na ukandamizwaji wa Nyerere na CCM yake, Sasa hapa CDM inaingiaje? Am I missing something? I hope husomi kutoka kulia kwenda kushota!

Leo umeshakuwa hujui kuwa chadema wana viwanda? si unavijuwa vya nini? au nalo pia hujui?
 
Hizi akili za Madrass taabu tupu! Dunia ndivyo ilivyo tutaendelea kuwaelimisha bila kuchoka.

Kama Matatizo ya Waislamu yametokana na ukandamizwaji wa Nyerere na CCM yake, Sasa hapa CDM inaingiaje? Am I missing something? I hope husomi kutoka kulia kwenda kushota!



Huyu ZOBA madrasa hajakanyaga. Walioenda madrasa ya ukweli hawako hivi, waislam hasa ni watu safi wala hawako kiponda ponda. Hawa hata uwape visa kwenda SAUD ARABIA hawaitaki kwani kule hakuna uhuni waliouzoea.

Jamani waislamu safi mbona tunawaona katika jamii? tusichukulie wahuni na wa vijiweni wasojua hata korani tukawajumuisha na waislam wote. Ila kwa kweli kwa hili kuwe na COLLECTIVE ACCOUNTABILITY
 
ccm iliomba kura kwa misingi ya udini, ilifanikiwa ikapata.

Lakini ilichokihubili ndicho sasa kinarudi nyuma kuitafuna inchi, ni wazi ccm waingie mtaani kwa mara nyingine kuwatuliza

wanachi na kuwaomba radhi kwa kuwaelezi ukweli na uwazi kwamba waliwadanganya watanzani na walifanya dhambi

kubwa kwa kuhubili chuki za kidini kwa urafi wa madarka.

Chadema haina cha kujadili maana kikwete na ccm hawakawii kupindisha ukweli na maana ya msemaji kuwa propaganda

za kuangamiza wapinzania wake, maadam muhalifu yupo madarakani atumie madaraka yake, majeshi na mahakama ni

zake kuituliza inchi si alipata alichotaka kupitia udini.
 
Chadema wakisema mnasema wadini, mmesahau waraka wa lema kwa JK? chadema watapakuaje cha kula cha udini mpishi JK, mpakuaji NAPE, msambazaji chakula cha udini ni LIPUMBA? wakina sita wanahazina ya viongozi ndiyo watoe tamko, usilite mada za ajabu, chadema fucus ni mabadiliko siyo vurugu za kidini
 
Viongozi wenye busara huzungumzia au kutoa tamko mahali na wakati unaofaa hivyo naona kwa viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM na CUF kukaa kimya ni sahihi zaidi kutokana na mazingira ya tukio, wakati na uelewa wa watu katika masuala mbalimbali. Wangekuwa wameshatoa tamko sasa hivi kukngekuwa na matusi, kejeli na maneno kutoka kwa watu mbalimbali kwani tumeona hili kwenye tukio la Morogoro, Iringa na kwingineko. Hata hivyo matamko katika hali hii yanapaswa kutolewa na viongozi wa dini na serikali na si vyama vya siasa, vile vile matamko tu hayasaidii isipokuwa matendo hasa mema.
 
Mtego wa ccm umefeli, wangependa sana cdm watoe tamko ili wawatwishe mzigo huu dhidi ya dini mojawapo..hofu ya kushindwa uchaguzi iliwafanya ccm kutojali athari ya yatakayotokea mbele. Yanayotokeo leo ndiyo yaliyopandwa 2015 wacha wavune wao wenyewe
 
Nimesema haya kutokana na kufuatilia misemo iliyotumika awali kwa viongozi wa pande hizi mbili Cdm na Ccm, Chadema wakiongozwa na mwasasiasa wao maarufu Slaa nanukuu walisema wakitaka Nchi haitatawalika, bila kusema wakitaka kwa njia ipi na haitatawalika kivipi! na Rais Kikwete kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Chama alisema nanukuu; Nchi hii imeanza kuhubiliwa udini. Nalinganisha hizi kauli mbili na baada ya matokeo yanayoendelea naona wazi ni muda mwafaka kwa pande zote mbili kufuta pandikizi zao kwa maneno yaliyo mema ili kuondokana na tuliko sasa. Kiongozi kauli zake huaminiwa sana na wafuasi wake hata kama zitakuwa si za kujenga hivyo waamuke waseme neno kwa wafuasi wao.
 
ni vigumu sana kwa chama cha kisiasa kuingia kati hili jambo......hasa kikiwa cha upinzani......hili jambo kwa nje linaonekana kama ni ugomvi kati ya waislam na serikali......lakini ukichimba ndani inawezekana si hivyo....hivyo kujiimgiza kwa kukurupuka kunaweza kuleta matokeo yasio mema baadaye
 
Zomba wewe ni waajabu sana! Yan una ropoka kiasi hiki, kwakweli hili ni tatizo lako binafsi na huu ni ugonjwa ambao unao siku nyingi sana.

Mtu kama wewe nilitegemea ulete facts with evidence sio haya maneno ya mitaani ambayo una jaribu kuwaaminisha watu!

Weka ushahidi tuone, tuchambue cdm ina husika vipi kwenye hili sio kuandika tu ilimradi umechangia!

Wewe ndio umeshindwa yani umekosa pakuisema cdm umeona uhusishe na hili, hakika kila mwenye utimamu wa akili ana jua wewe ni mchonganishi na unashindwa kila hiitwapo leo.


Chadema wamejaribu kwa wananchi wameshindwa, wamejaribu kwa madaktari wameshindwa, wamejaribu kanisani wameshindwa, sasa wanajaribu kwa Waislaam, watashindwa.

Watshindwa kwa kuwa, matukio yanayohusishwa na Waislaam si ukweli, hata mashtaka aliyofunguliwa Ponda yanahusiana na ukandamizwaji wa Waislaam uliofanywa na Nyerere alipoiua EAMWS na kuunda BAKWATA.
 
Hawa ni watu wa ZOKA. Liko wapi tamko la CCM na NAPE

CDM ni chama Makini. Hawatoi matamko kiholela. HEBU TAFAKARI: Wanaofanya Fujo ni WAISLAMU. Chama kilichoko madarakani kinawapendelea WAISLAMU. Chama shirika cha Chama TAWALA ni cha KIISLAMU ambao wote kwa pamoja "wanaipakazia CDM" kuwa chama cha KIKRISTO. Je wakitoa tamko watasikilizwa na nani?
 
Ukimya wa CHADEMA na chama cha wananchi CUF kutokana na matukio yanayo endelea kutokea hapa nchini ni udhaifu mkubwa sana ktk kuonesha kama hawajali inasibitisha kuwa bado wachanga kwa maswala ya kitaifa. Matukio kama kukojolewa kitabu kitukufu cha waislam ,viongozi kimya si chadema wala cuf. Kuchomwa kwa makanisa viongozi kimya si CHADEMA wala CUF. Kuuawa kwa polisi zanzibar viongozi kimya si CHADEMA wala CUF. Kuwa kimya ktk matukio makubwa kama haya kunaonesha kutokuwa tayari kuwaongoza watanzania. Pia ni ishara ya kukosa huruma huku wanapo kuwa na matukio yao ya kisiasa au kijamii huwataka wananchi kuwaunga mkono.CCM wao wametoa tamko tuwewaona aibu ipo kwa CHADEMA na CUF, mbona kimya kulikoni?
Si walikwisha sema kuwa mkiirudisha tena ccm madarakani mtakuwa mnaiangamiza nchi! Hukuamini? Ndio inakula kwetu sasa!
 
Janja yenu tulishaijua, mnaanzisha upuuzi ili watu waingie kwenye mtego halafu muanze kusema ohh unaona CDM inatetea MAKANISA, brabraaaaa.
Uzuri Wakristo ni watu decent sana. Mnataka kuwa provoke ili mpate sababu ya ugomvi, hawana akili ya kitoto kivile. Hivi mnaombea waguse hata ukuta wa msikiti mjifannye mnatangaza Jihad. Mmenoa.

Mwenye akili huona hatari na kujiepusha, mjinga usonga mbele na kuangamia.( Mithali)
 
Back
Top Bottom